Jembe Jembe
JF-Expert Member
- Jun 9, 2016
- 749
- 1,797
Mama wa Marehemu Bilionea Erasto Msuya ,Ndishu Msuya amesema kuwa yupo tayari kuliondoa kwa muda shauri la mirathi lililopo mahakamani dhidi yake na Mke wa Marehemu Miriamu Mrita ili kupisha mazungumzo nje ya mahakama.
Amesema kuwa iwapo mazungumzo hayo yanayotarajiwa kuongozwa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro hayatafanikiwa,atarejea mahakamani kuendelea na shauri hilo ili kupata haki ya msingi juu ya hatima ya mali za mwanaye.
Akiongea na vyombo vya habari hivi karibuni,Ndeshu amefafanua kuwa alifika mahakamani hapo kuiomba mahakama kuondoa kwa muda shauri hilo ili kutafuta mwafaka nje ya mahakama kuridhia ushauri wa mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Murro.
Alisema amefungua shauri hilo la mirathi kumpinga msimamizi wa mirathi, Miriam Mrita kwa madai ya kushindwa kusimamia,kugawanya na kufunga Mirathi kwa wanufaika katika kipindi cha miaka saba kinyume cha sheria.
"Tulikuja mahakamani kuiomba mahakama kama itapendezwa tuondoe shauri hili kwa muda na sio kufuta kesi ili turejee kwenye mazungumzo nje ya mahakama na tukishindwa kuafikiana tutarudi mahakamani " Amesema Mama Ndeshu
Marehemu bilionea Erasto Msuya aliuawa kwa kupigwa Risasi zaidi 20 mwaka 2013 na kuacha mjane na watoto wanne pamoja na Mali mbalimbali yakiwemo Majumba,Fedha ,Magari Mashamba na Hotel Mali ambazo zinadaiwa kuwagombanisha wanandugu .
Ndeshu aliamua kukimbilia mahakamani kupinga msimamizi wa mirathi hiyo Miriamu Mrita ambaye ni mke wa marehemu akidai kwamba Miriamu ambaye anashikiliwa Magereza kwa mauaji ya wifi yake si mwaminifu na ameshindwa kugawanya mali za Marehemu kwa wanufaika kwa muda wa miaka saba tangu kifo cha Marehemu na kusababisha baadhi ya mali kuanza kupotea.
Amedai kuwa mali hizo zimekuwa zikiwanufaisha upande wa mke wa marehemu(Wajomba)badala ya watoto wake wanne ambao kimsingi ndio wanaostahili kurithi Mali hizo.
Awali mtoto mkubwa wa marehemu,aitwaye Kelvin Saimoni Msuya amesema anamuomba bibi yake Ndeshu Msuya kuridhia Kesi hiyo kuondolewa mahakamani na kukaa Meza moja na yupo tayari kwa mazungumzo na upande wa wazazi wa baba yake na kuwataka ndugu hao kuwa na upendo na mama yake anayesota gerezani kwa kesi ya mauaji kama ambavyo wanavyodai wanaupendo naye.
Naye Mjomba wa watoto wa Marehemu, Mbazi Stephen Mrita aliomba Serikali kuingilia kati mgogoro huo Wa kuondoa Kesi hiyo mahakamani kama walivyo shauriwa na mkuu Wa Wilaya ya Arumeru ,Jerry Muro .
Kesi hiyo inasikilizwa na Jaji Johane Masara wa mahakama kuu na ilikuja mahakamani hapo Novemba 29 mwaka huu na kuahirishwa na Msajili Msaidizi wa mahakama,John Fransis Nkwabi hadi Disemba 13 mwaka huu itakapokuja tena mahakamani hapo.