Mama wa Bilionea Msuya akubali kuondoa kesi kwa Muda Mahakamani

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
Mama wa Marehemu Bilionea Erasto Msuya ,Ndishu Msuya amesema kuwa yupo tayari kuliondoa kwa muda shauri la mirathi lililopo mahakamani dhidi yake na Mke wa Marehemu Miriamu Mrita ili kupisha mazungumzo nje ya mahakama.

Amesema kuwa iwapo mazungumzo hayo yanayotarajiwa kuongozwa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro hayatafanikiwa,atarejea mahakamani kuendelea na shauri hilo ili kupata haki ya msingi juu ya hatima ya mali za mwanaye.

Akiongea na vyombo vya habari hivi karibuni,Ndeshu amefafanua kuwa alifika mahakamani hapo kuiomba mahakama kuondoa kwa muda shauri hilo ili kutafuta mwafaka nje ya mahakama kuridhia ushauri wa mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Murro.

Alisema amefungua shauri hilo la mirathi kumpinga msimamizi wa mirathi, Miriam Mrita kwa madai ya kushindwa kusimamia,kugawanya na kufunga Mirathi kwa wanufaika katika kipindi cha miaka saba kinyume cha sheria.

"Tulikuja mahakamani kuiomba mahakama kama itapendezwa tuondoe shauri hili kwa muda na sio kufuta kesi ili turejee kwenye mazungumzo nje ya mahakama na tukishindwa kuafikiana tutarudi mahakamani " Amesema Mama Ndeshu

Marehemu bilionea Erasto Msuya aliuawa kwa kupigwa Risasi zaidi 20 mwaka 2013 na kuacha mjane na watoto wanne pamoja na Mali mbalimbali yakiwemo Majumba,Fedha ,Magari Mashamba na Hotel Mali ambazo zinadaiwa kuwagombanisha wanandugu .

Ndeshu aliamua kukimbilia mahakamani kupinga msimamizi wa mirathi hiyo Miriamu Mrita ambaye ni mke wa marehemu akidai kwamba Miriamu ambaye anashikiliwa Magereza kwa mauaji ya wifi yake si mwaminifu na ameshindwa kugawanya mali za Marehemu kwa wanufaika kwa muda wa miaka saba tangu kifo cha Marehemu na kusababisha baadhi ya mali kuanza kupotea.

Amedai kuwa mali hizo zimekuwa zikiwanufaisha upande wa mke wa marehemu(Wajomba)badala ya watoto wake wanne ambao kimsingi ndio wanaostahili kurithi Mali hizo.

Awali mtoto mkubwa wa marehemu,aitwaye Kelvin Saimoni Msuya amesema anamuomba bibi yake Ndeshu Msuya kuridhia Kesi hiyo kuondolewa mahakamani na kukaa Meza moja na yupo tayari kwa mazungumzo na upande wa wazazi wa baba yake na kuwataka ndugu hao kuwa na upendo na mama yake anayesota gerezani kwa kesi ya mauaji kama ambavyo wanavyodai wanaupendo naye.

Naye Mjomba wa watoto wa Marehemu, Mbazi Stephen Mrita aliomba Serikali kuingilia kati mgogoro huo Wa kuondoa Kesi hiyo mahakamani kama walivyo shauriwa na mkuu Wa Wilaya ya Arumeru ,Jerry Muro .

Kesi hiyo inasikilizwa na Jaji Johane Masara wa mahakama kuu na ilikuja mahakamani hapo Novemba 29 mwaka huu na kuahirishwa na Msajili Msaidizi wa mahakama,John Fransis Nkwabi hadi Disemba 13 mwaka huu itakapokuja tena mahakamani hapo.

IMG-20191205-WA0001.jpeg
 
Mtoto anamuonea huruma mama yake aliyeko jela, kibinadamu ni sawa ila hajielewi kwamba yeye ni Msuya. Laiti kama angesikilizana na upande wa baba yake. Na kuwa muelewa kukubali tu ukwl kwamba mamake hawezi kuwa na uhusiano mzuri na kina msuya kutokana Na kesi ( mauaji dada Wa marehemu) hakuna mtu anamnyima kumpenda kumsaidia mamake iko uchi hiyo sasa ye kaenda mzima mzima Asimame katikati mimi Binafsi naifahamu familia ya Mume ni kwamba hawana njaa kiukweli kabisa wale hawataki tu. Mali ya ndugu yao iende bila utaratibu unfortunately mtt Mkubwa Wa marehemu hajielewi wala hatambui nafasi yake..kifamilia.
 
Msuya alitegemea hill jembe Lita simama badala yake kumbe Toto lenyewe ni fambaa
 
Mtt anamuonea huruma mama yake aliyeko jela..kibinadamu ni sawa ila hajielewi kwamba yeye ni Msuya..laiti kama angesikilizana na upande wa baba yake ..Na kuwa muelewa kukubali tu ukwl kwamba mamake hawezi kuwa na uhusiano mzuri na kina msuya kutokana Na kesi ( mauaji dada Wa marehemu) hakuna mtu anamnyima kumpenda kumsaidia mamake iko uchi hiyo sasa ye kaenda mzima mzima Asimame katikati mimi Binafsi naifahamu familia ya Mume ni kwamba hawana njaa kiukweli kabisa wale hawataki tu. Mali ya ndugu yao iende bila utaratibu unfortunately mtt Mkubwa Wa marehemu hajielewi wala hatambui nafasi yake..kifamilia.
Na ukiangalia kwa kweli huyu mtoto ni mpumbavu sana maana yeye anataka Mama Msuya ampende mama yake ambaye kwa facts tuu amehusika kwa asilimia mia moja mauaji ya Annety Msuya hivyo familia ya Msuya haiwezi kushirikiana na MTU aliyewaulia mtoto wao. Kijana ajitambue yy ni Msuya na si Mbazi kama anavyofikiri
 
mahakama siku zite ndio zinatuangusha, walitakiwa wawe washatoa hukumu ya kesi ya bibi kupinga usimamizi wa mirathi wa mkwerima wake

mahakama inayosikiliza jinai ya mauaji Dar-es-Salaam, kama ile ya probate Arusha, nayo pia itajivuta vuta miaka 10 kabla ya kumaliza kesi ya mjane mtuhumiwa.

ndo maana jumuiya ya kimataifa imesema imefadhaishwa na Tanzania kujitoa mahakama ya Afrika kwa sababu mahakama zake za ndani hazina uwezo wowote, mbovu kupindukia.
 
Mtt anamuonea huruma mama yake aliyeko jela..kibinadamu ni sawa ila hajielewi kwamba yeye ni Msuya..laiti kama angesikilizana na upande wa baba yake ..Na kuwa muelewa kukubali tu ukwl kwamba mamake hawezi kuwa na uhusiano mzuri na kina msuya kutokana Na kesi ( mauaji dada Wa marehemu) hakuna mtu anamnyima kumpenda kumsaidia mamake iko uchi hiyo sasa ye kaenda mzima mzima Asimame katikati mimi Binafsi naifahamu familia ya Mume ni kwamba hawana njaa kiukweli kabisa wale hawataki tu. Mali ya ndugu yao iende bila utaratibu unfortunately mtt Mkubwa Wa marehemu hajielewi wala hatambui nafasi yake..kifamilia.
Huyo mtoto ni kubwa jinga
 
Mtoto anamuonea huruma mama yake aliyeko jela, kibinadamu ni sawa ila hajielewi kwamba yeye ni Msuya. Laiti kama angesikilizana na upande wa baba yake. Na kuwa muelewa kukubali tu ukwl kwamba mamake hawezi kuwa na uhusiano mzuri na kina msuya kutokana Na kesi ( mauaji dada Wa marehemu) hakuna mtu anamnyima kumpenda kumsaidia mamake iko uchi hiyo sasa ye kaenda mzima mzima Asimame katikati mimi Binafsi naifahamu familia ya Mume ni kwamba hawana njaa kiukweli kabisa wale hawataki tu. Mali ya ndugu yao iende bila utaratibu unfortunately mtt Mkubwa Wa marehemu hajielewi wala hatambui nafasi yake..kifamilia.
Ni kweli huyo mama kamuua wifi yake au ni set up?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom