Mama Tibaijuka kurudisha shilingi bilioni 1.6 za mgawo wa Escrow aliopewa na Rugemalira

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,977
Mbunge wa Muleba mkoani Kagera Prof Tibaijuka amerudisha fedha alizopewa na mzee Rugemalira ili kuondoa sintofahamu iliyokuwepo kwamba fedha zile zilitoka katika account ya Escrow.

Prof Tibaijuka ameitikia wito wa Rais Magufuli kuwataka waliofisadi fedha za umma kukiri na kuzirejesha.

-------
Mbunge wa Muleba Kusini (CCM), Profesa Anna Tibaijuka amesema uongozi wa Shule ya Sekondari Barbro Johansson Model Girls utarejesha fedha za msaada walizopokea kutoka kwa mfanyabiashara, James Rugemarila ili aweze kutoka gerezani.

Profesa Tibaijuka amesema hayo leo Jumanne Oktoba Mosi, 2019 kupitia Kituo cha televisheni cha Azam UTV.

Amesema uongozi wa shule hiyo umekaa kikao na kuamua kurejesha fedha hizo walizopokea ili kumsaidia mtuhumiwa huyo anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi kutoka gerezani.

“Suala hili sio langu binafsi maana fedha hizi ni za shule, mwenyekiti wangu (wenyekiti wa bodi), Salmon Odunga na mwenyekiti wa wazazi, Dk Kiharuzi wamekaa kwenye kikao wakaamua fedha zirudi."

"Nashukuru kwa msimamo huo kwa kuwa ndio msimamo wangu pia kwamba kama itasaidia, tunashukuru Mungu," amesema Profesa Tibaijuka.

Alipoulizwa kama fedha walizopewa msaada zilikuwa hazijatumika hadi sasa, Profesa Tibaijuka amesema licha ya fedha hizo kutumika kulipa deni la kujenga bweni la shule lakini zitatafutwa na zitarejeshwa.

“Fedha zenyewe zilikwenda kulipa deni la mkopo ambao tulijenga bweni lakini taasisi kama hii inapoamua kurejesha fedha zitatafutwa na kurejeshwa” amesema.

Amesema kutokana na Rais wa Tanzania, John Magufuli kushauri watuhumiwa wa uhujumi uchumi waandike barua kukiri na kurejesha fedha na mali, wao watarejesha kiasi walichopewa na Rugemarila.

“Msamaha wa Rais unapotoka ni fursa adimu, sasa fursa ukiichezea utabaki kujuta mwenyewe, kwa upande wangu na shule, sisi tunashughulika na ule mchango tulioupokea tunaurudisha mezani” amesema profesa Tibaijuka.

Profesa Tibaijuka alipokea mchango wa Sh1.617 bilioni kutoka kwa Rugemarila ambazo amesema zilitumika kwa ajili kulipa mkopo waliokuwa wakidaiwa katika Bank M.

Rugemarila anakabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha na uhujumu uchumi Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

-Mwananchi-
 
Kwa Kuendekeza Ufisadi Halafu Watu Wanarudisha Ndio Njia Itakayoongeza Ufisadi Maradufu"

Unaweza Fikiria Unapambana Na Ufisadi Kumbe Ndio Unapalilia Ufisadi Kwanza Mwanasiasa Wa Kawaida Na Mwadirifu Kabisa Mbunge Unatoa Wapi Bil 1.6 ?

Au Unawezaje Kutunza Pesa Iyo Kwa Miaka 5 Bila Kuitumia? Inamanisha Uliiba Sana Ila Walipokugundua Ndio Unarudisha

Ningependa Pia Magufuli, Mkapa Na Sumaye Wakamatwe Warudishe Nyumba Za Serikali.

Pesa Ya Mboga Duh Nikikumbuka Kauli Iyo Uwa Naumia Sana Mwanasiasa Mwadilifu Hawezi Kuita Bil 1.6 pesa ya mboga.
 
Tunasubiri na hizi...
Pesa za nyumba za NHC
Pesa za Wizara ya Ujenzi 234 billion
1.4 trioni zilizo semwa na CAG
Ukaguzi wa ATCL
Kufidia hasara iliyotokana na kununua kivuko kibovu........

Kufidia hasara iliyosababishwa na kugawa kwa "nyumba mdogo" za serikali.......

Kufidia hasara iliyosababishwa na maamuzi ya kukurupuka kwa ukamataji wa meli ya samaki iliyokuwa ikivua........
 
Kwa Kuendekeza Ufisadi Halafu Watu Wanarudisha Ndio Njia Itakayoongeza Ufisadi Maradufu"
Siyo hivyo. Kwanza unakiri kosa na hapo ndiyo unazirudisha hela hizo. Halafu unaahidi kutorudia kosa hilo. Kama utarudia, si tu utahitajika kuzilipa hizo hela bali na adhabu nyingine, kama kifungo, zitaongezwa juu yake.

Hii ni nzuri sana. Tunarudishiwa hela ambazo zilikuwa zimekwenda na maji na nchi haiingii gharama za kuendesha kesi ambazo hata kushinda ni kwa wasiwasi.
 
Hivi 1billion kipindi chote hicho, arudishe toka wapi? Watanzania acheni bumbuazi
 
Back
Top Bottom