Namjua huyo mama ila huwa anauz mara nyingi urembo wa usoni na sabuni, ila anapenda tu story za aina hiyo ila mkimuuliza huwa hamfundishi mtu lolote labda uanze kujiulizisha mwenyewe
Sahihisho dogo ndugu.
Huyu mama yupo na anafundisha kweli tena kwenye vyuo na hata ukitaka anakufuata nyumbani kwako.
Alianza kwa kuuza vitu vidogo vidogo kwenye vyuo na maofisini huku pia akichombeza kuhusu haya mafunzo ya mambo ya chumbani.Alipoona inalipa basi akaigeuza bishara rasmi japo sijui kama amesajiliwa.
Anachanganya mawaidha na massage/kukandwakandwa na hapa huwahudumia pia wanaume ( alihojiwa kwenye gazeti akadai kuna vishawishi na majaribu mengi na sikuelewa alikuwa na maana gani hapo)
Alipohojiwa na gazeti moja la kiswahili la kila siku alisema wateja wake ni wanafunzi vyuoni, mawaziri, wabunge etc!
Alisema hutoza kati ya sh.100,000/- na 250,000/= na ukitaka kufuatwa ulipo basi itakugharimu zaidi ya hapo - utaongezea kati ya sh 50,000/- hadi 100,000/=!
Alisema pia kuwa mwanzoni alipata shida sana na kilichomsukuma kufanya kazi hii ni manyanyaso ya mumewe lakini sasa mumewe anampenda maana anaona kipato kinachoingia. Ndugu wa mume pia walimletea maneno sana alipoanZA KAZI HII ILA HAKUWAJALI.
Niliposoma makala ya gazeti kuhusu huyu mama, hata mimi nilijuliza maswali mengi sana nikakosa jibu ila nilifanya jitihada huhoji baadhi ya wateja wake na cha kushangaza wanafunzi wa vyuo wanamkubali sana na wanadhani huduma hii inahitajika.
Kadhalika wakina mama wao hawakujali athari kwa watoto bali waliona wao wenyewe wanasumbuka sana kwenye ndoa zao kujaribu kuwamudu na kuwadhibiti waume zao hivyo wakaona bora huyu mama awape ushauri ni vipi wazikinge ndoa zao kwa kupata "maujuzi" haya.
Sijui kama kasajili hii huduma maana pato analolipata ni kubwa na linastahili kutozwa kodi kama wanavyotozwa wafanyabiashara wengine.