Mama Samia anza kwa kuboresha Baraza la Mawaziri

Safi sana.


Sasa ewe kiongozi was juu wa kiserikali unayepita kimya kimya kwenye huu Uzi na kusoma hii comment, nikuonye kama hauko kwa ajili ya wananchi wa tanzania basi niseme lazima udondoke mana tutapiga maombi ili wale makenge wote wajiuzulu wenyewe au wakubali kuondoshwa, tuweke watu wapya wenye mapenzi mema na wananchi wa Tanzania na maendeleo yao mmoja mmoja.
 
Mama ni wa kumuhurumia na si ajabu ambavyo hapendi makuu akaikataa hiyo nafasi.
Atakayekuwa rais atakuwa na kazi ngumu kuliko marais wote waliopata kutokea tz...
Duuuh, unaweza ku-edit kama umekosea, laa, imani yako itakutendea hivyo
 
Nashauri Makamu wa Rais awe Mkristo Mkatoliki na Waziri Mkuu awe Mkristo Mprotestanti au Makamu wa Rais awe Mkristo Mprotestanti na Waziri Mkuu awe Mkristo Mkatoliki....
Mkuu kama vile unaonekana una busara na akili nyingi
 
Kwa watu waungwana, baraza lote la mawaziri lijiuzuru, limpe nafasi Samia kuunda la kwake from the scratch. Kama wengi mlivyosema, baraza hili liilundwa kwa mahitaji ya JPM, siyo lazima limfae Samia.

Tusiwalaumu mawaziri waliokuwa wa ndio mzee maana hao ndio aliowahitaji. Msisubiri mama aanze kuwatumbua, Chonde chonde kwa heshima mjiuzuru.

Kwa kuwa kuna ving'ang'anizi wasiotaka kujiuzuru basi Waziri mkuu anza wewe na ukifanya hivyo itabidi na wengine nao wote wajiuzuru.
Labda sio bongo waziri kujiuzuru ni ngumu sana ,kwa upuuzi alouongea majaliwa ilibidi ajiuzuru lakini wapi kakomaa
 
Mpaka alipofikia hapo anajua hiyo office vzr tu ni kama..mlivyokuwa darasani mnajua Fulani kichwa,huyu mwizi,yule muhuni nk..mama anajua lkn muda upo wa kushauri for the mean time naomba tuheshimu Marehemu Mzee kipenzi changu walau akipumzishwa basi tuanze na mengineyo tafadhali sana kwa heshima.yake.
 
Safi sana.


Sasa ewe kiongozi was juu wa kiserikali unayepita kimya kimya kwenye huu Uzi na kusoma hii comment, nikuonye kama hauko kwa ajili ya wananchi wa tanzania basi niseme lazima udondoke mana tutapiga maombi ili wale makenge wote wajiuzulu wenyewe au wakubali kuondoshwa, tuweke watu wapya wenye mapenzi mema na wananchi wa Tanzania na maendeleo yao mmoja mmoja.
Cheki hili li mataga
 
Nashauri Makamu wa Rais awe Mkristo Mkatoliki na Waziri Mkuu awe Mkristo Mprotestanti au Makamu wa Rais awe Mkristo Mprotestanti na Waziri Mkuu awe Mkristo Mkatoliki.

Waziri Mkuu awe Mkenda au Kimei kuendana na kama Makamu wa Rais atakuwa Mprotestanti au Mkatoliki.

Kabudi anaweza kuwa Makamu wa Rais na Waziri Mkuu anaweza kuwa Mkenda.

Au Lukuvi anaweza kuwa Makamu wa Rais na Kimei akawa Waziri Mkuu.

Au combination nyingine nzuri za Makamu wa Rais Mkatoliki na Waziri Mkuu Mprotestanti au Makamu wa Rais Mprotestanti na Waziri Mkuu Mkatoliki.

Bunge ndio liwe uwanja mkuu wa kufanya maamuzi haya, kwasababu uwiano wa kidini ndani ya Kamati Kuu ya CCM, hauendani na hali halisi nchini.

Halafu in the future, baada ya Rais Samia kumaliza vipindi vyake vya uongozi, tujaribu kuwa na Rais Mprotestanti, kwasababu Tanzania haijawahi kuwa na Rais Mprotestanti.

Ushauri huu usipofuatwa hakuna tatizo lolote. Maisha yanaendelea kwa amani na utulivu.
We C mtanzania ,nakujua vzr
 
Kwa kuongeza, afuate sheria, mfano ateue wakurugenzi (ma-DED) kutoka Miongoni mwa watumishi wa umma wa nafasi za juu (inakuwa kama promotion) na sio kuokota okota kama mtangulizi wake alivyofanya.

Aanze kumuondoa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, huyu amemdanganya Rais mteule kutamka idadi ya siku za maombolezo tofauti na zilizopo katika Sheria (kama hajatoa ushauri yeye maana yake hajatekeleza wajibu wake)

Auache mhimili wa Mahakama uwe huru. Majaji na mahakimu wawe na amani wanaposikiliza kesi za madai zinahusu serikali, wasiamue kwa upendeleo wakiipendelea serikali sababu tu wanamuogopa Rais. Ateue majaji kwa kufuata sheria, tume ya mahakama ndio ipendekeze majina sio tena kuteuana kiholela holela sababu tu Jaji kaandika hukumu kwa Kiswahili nk, Atarejesha imani iliyopotea ya wananchi kwa Mahakama kama chombo pekee cha utoaji haki.
Hili la ma DED kuchaguliwa amongst wakuu wa idara nakuunga mkono hoja, kwanza zamani huu ndiyo ulikuwa utaratibu.
 
Back
Top Bottom