Mama Salma Kikwete anusurika kupata ajali mkoani Mara

Mnampa pole ya nini wakati Sheikh Ubwabwa wa Magomeni karibu na BP alitabiri!

Unamaana sheikh huyu?

sheikh-yahyabc.jpg
 
mkuu nilikuwa nataka kutoa koment kali ila ikabidi nicheke baada ya kusoma atiko yako.
mkuu ulijifunzia kwa yahaya husein lini haya mambo? au ndo mambo ya KAINZI krtu kale kufukunyua kusikofukunyulika?

hapana.. hii siyo suala la inteligensia ni instinct tu. Naweza kukosea kabisa lakini so far sijuii ni kipaji au wherever I have been right most of the time. Siagui, sisomi nyota, sisomi viganya wala kufanya ubashiri wa aina yoyote ile. Ila hisia hiyo ikija ni vizuri kusema maana muda mrefu huwa nakaa kimya na sasa nimeona niwe na toa commentary hizi ndogo ndogo.
 
Kwakweli natatizwa sana na nafasi ya "First Lady" hasa huyu wa sasa katika mpangilio wa serikali yetu. Maana nimeona akisomewa risala na Mkuu wa Mkoa wa Mara na baada ya risala ya mkuu wa mkoa yeye akapewa nafasi ya kutoa hotuba yake ambayo inajumuisha kutolea majibu hotuba ya mkuu wa mkoa. Sijui hapo anaongea kama Mwenyekiti wa WAMA au kama Makamu wa Raisi kivuli katika serikali ya awamu ya nne.

Nafikiri ipo haja ya huu mkanganyiko kurekebishwa haraka ili Mama wa kwanza azungumze wakati wote kama Mwenyekiti wa WAMA au akitoka sana kama atakuwa kwenye ziara za chama cha mapinduzi (ambako ni mjumbe wa mkutano mkuu) basi azungumzie mambo ya chama na aongee na wanachama wa CCM.

Nafikiri Ikulu itazingatia haya maoni na kumtofautisha Rais na mke wa rais katika utendaji wa shughuli za serikali. Nafikiri hili ni muhimu kuzingatiwa wala si suala la ushabiki wa kisiasa.
 
Mwenyezi Mungu atakulinda na kukuepusha na balaaa au Husda za watu.pole Mama kwa Misukosuko.
 
Hiyo biashara ya kupisha misafara ya viongozi au wake zao inatupotezea muda jamani!!! Inaudhi!
Na Ku bore pia...bora hajagongwa kabsaaa..maana Muungwana angekuwa mpweke na safar zake za nje zingeongezeka mra mia
 
Hiyo biashara ya kupisha misafara ya viongozi au wake zao inatupotezea muda jamani!!! Inaudhi!
Moja ya mawazo ya kishetani. Kwahiyo Nkamangi unakubaliana na huyo mvuta bangi aliyetaka kumgonga my wife wa JK. Sidhani kuwa kila mtu anachowaza kinafa kusemwa hadharani hasa mbele ya waungwana kama wa humu jamvini. Hivi unakumbuka ziara ya LAURA BUSH ilikuwaje? Usiwe na mawazo potofu katika vitu vya msingi na vinavyoweza kuleta matatizo makubwa kwa nchi. Plz think twice before press the button on your computer keypad
 
Usinihusishe na shetani tafzali, usiweke maneno kinywani mwangu. Narudia nilichosema, they should join the queue... Wakati mwingine hata foleni hakuna tunaambiwa kuwapisha kwenye highway. Ujinga gani huu?
You're the one who should "double think"
 
Back
Top Bottom