SoC02 Mama na uchumi wa kati

Stories of Change - 2022 Competition

EAB

New Member
Jul 22, 2022
1
0
Mama ni mwanamke mwenye jukumu la kulea familia. Miaka ya nyuma katika jamii za kiafrika mama alikuwa hapewi kipao mbele katika suala zima la maendeleo, kazi yake kuu ilikuwa Ni kuzaa na kutunza familia jambo ambalo ni yofauti na sasa.

Kutokana na mabadiliko ya kisiasa kiuchimi na kiutamaduni yanayozikabili jamii nyingi za kiafrika Tanzania ikiwa miongoni mwao kumekuwa na mwamko mkubwa wa akinamama katika suala zima la ukuzaji wa uchumi wa familia, jamii na taifa kwaujumla. Mama na uchumi wa kati amekua na mchango katika nyanja zifuatazo;

Kiuchumi; katika suala zima la uchumi akinamama wamekuwa si tegemezi kwa familia Kama mwanzo kwani ukiachana na walioajiriwa serikalini na katika sekta binafsi pia kuna akinamama wengi ambao wamekuwa na uthubutu wa kujishughulisha katika biashara,kilimo,ufugaji na ujasiriamali kitu ambacho huwaweka katika kundi la watu wenye mchango wa maendeleo kwa familia zao,jamii na taifa kwa ujumla hivyo kuwaepusha na utegemezi usiokua wa lazima.

Kisiasa; akina mama pia wamekua na mwamko wa kushiriki katika ngazi mbalimbali za kiutawala Kama vile, serikalin za vijiji, kata na miji kwani ushiriki wao huonekana kwa kupewa kipao mbele kushiriki katika kugombea na kuwapigia kura wagombea wanaotamaini kuongozwa nao hali ambayo huketa usawa katika siasa hivyo kuchochea maendeleo ya serikalin na taifa.

Kiutamaduni; Miaka ya Sasa imekuwa tofauti na zamani kwani mila na desturi potofu zilizokuwa zikiwakandamiza akinamama kushiriki katika shughuli mbalimbali za kuleta maendeleo zimetupiliwa mbali. Kutokana na jambo hilo akina mama wamekua na mtazamo chanya juu ya ushiriki wao katika shughuli mbalimbali za kuwaletea vipato.

Kijamii; Katika jamii nyingi za kiafrika akina mama wamekua na mchango mkubwa katika uchumi wa kati kwani kupitia wao vimeundwa mbalimbali vinavyohamasisha na kutoa elimu ya ujasiriamali jambo ambalo husaidia wanawake kujiajiri katika shughuli mbalimbali kama vile upishi,ushonaji na biashara ndogondogo hata kujipatia kipato chao.

Hivyo; Kutokana na usemi kuwa"Kila palipo na maendeleo mwanamke yupo"Serikalin,sekta binafsi na jamii kwa ujumla hatuna budi kutoa elimu ya usawa katika nyanja za kiuchumi,siasa na kiutamaduni hali ambayo itaongeza hamasa na kuleta mtazamo chanya kwa jamii za kitanzania ambazo akina mama bado wako nyuma katika mchango wa maendeleo.
 
Back
Top Bottom