HorsePower
JF-Expert Member
- Aug 22, 2008
- 3,612
- 2,566
Ni kijana wa umri wa miaka 28, nimeajiriwa ktk shirika moja kubwa la umma na recently nimehamishiwa mkoani Dar. Nilipata shida sana kupata nyumba, na kwa msaada wa rafiki yangu, aliniunganishia nyumba (Vyumba viwili na sebule hapa Sinze kwa Remmy) kwa huyu mama. Ni nyumba aliyokuwa anaishi yeye rafiki yangu lakini sasa amejenga yake na kunisaidia kuipata kwa kodi ile ile aliyokuwa analipa yeye.
Ni takriban mwezi wa tatu sasa, mama mwenye nyumba amekuwa akijizungusha kuchukua kodi yake ... Kila nikimwambia nimkabidhi amekuwa hayuko siriaz akisisitiza nisiwe na wasi wasi ataniambia lini nimpe. Amekuwa mchangamfu sana, na ananizoea kwa kasi mno na wakati mwingine kadiriki hata kuniletea chakula cha jioni.
Nimeingia na hofu kwa hii speed yake, sijui nia yake, nahisi kumuelewa tofauti. Naomba ushauri, nihame?
****** Email ya mdau mmoja toka Sinza kwa Remmy anaomba ushauri ****