Mama mkwe ni msumbufu, nimechoka. Nifanyeje?

Mama mkwe ni msumbufu, nimechoka. Nifanyeje?

Kuna Besti yangu Tulimaliza nae chuo Mjini hapa Dar yeye akafanikiwa kupata kazi Bank moja ivi ipo Posta ila yeye anakaa Tegeta nyuki. Ana kama miaka miwili toka apate kazi pia akapewa mkopo wa gari IST. Mwaka jana mwezi wa tatu aka oa mke Mtu wa Mbagala alikuwa ni moja wa Classmate wetu..

Ishu ni kwamba mke wake kwa sasa ni mjamzito kama miezi saba hivi. Hivyo anahitaji uangalizi wa karibu sana na yeye mda mwingi yupo kazini anaondoka asubui sana na kurudi usiku. Kila akirudi nyumbani kutoka kazin huwa anamkuta mama mkwe nyumbani kwake (sio jambo baya) na baada ya jamaa kuingia tu mama mkwe huwa anaaga kuondoka hivyo anataka arudishwe kwao Mbagala. Jamaa huwa inamlazimu kumrudisha mama mkwe wake Mbagala na kupelekea kuchoka zaidi na kutumia gharama kubwa za mafuta na kurudi nyumban usiku sana maana Tegeta to Mbagala ni safari.

Jamaa amejaribu kuongea na mke wake amwambie mama mkwe basi awe anakuja hata mara moja kwa week hii ilipelekea ugomvi mke anahisi labda jamaa hampendi mama mkwe wake. Na sababu kubwa mama mkwe anakuja kushinda na mwanae kutokana na hali ya ujauzito hawana hata house girl.

Mara nyingi jamaa ana jaribu kumshawishi basi mkwe alale pale ila mkwe anakataa kabisa anadai hawezi kulala nje ya nyumba yake...

Binafsi nisha wai mshauri jamaa asingizie gari bovu ameliacha garage na alisha jaribu kufanya ivyo ila ili mkost vile vile sababu ilibidi achukue UBER ya kumrudisha mkwe Mbagala..

Sasa jamaa anaomba ushauri afanyaje? Anachoka sana pia anatumia gharama kubwa sana.. Gari yake hawezi kuiuza sababu bado inakatwa ni ya mkopo wa bank..
Kwani lazima ampeleke na gari, ampe pesa ya daladala, jamaa yako anatakiwa awe na misimamo isiyoyumba
 
Mama mkwe wake ni mkorofi.. Huwa anakataa kabisa kulala nje na kwake..
Gharama ya mafuta ya kumpeleka huyo mama Mbagala siku 3 sawa na mshahara wa mfanyakazi wa ndani.
Acheni mambo ya ajabu wekeni mfanyakazi wa kike mkubwa mkubwa amsaidie mjamzito.

Mambo madogo ya kitoto kama hayo yanaweza kuvunja ndoa ya jamaa au kujenga chuki za ndugu wa wana ndoa.
 
Inaezekana ni story ila acha tukujibu ivi...

Kama unaona huyo mkwe anasumbua kaa wewe.

Huyo jamaa atafte mdada wa kumsaidia mkewe kazi. Usumbufu ukiendelea basi itakua ni uchokoz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi Waswahili tuolewe na nani?
Ahahahaaaa [emoji3][emoji23][emoji1787]. Sky bhuaana. Waswahili kwa maana ya tabia za Kiswahili. Wewe huzuiliwi kwenda kumlea mwanao. Lakini ya kulazimisha kurudishwa nyumbani usiku hapana. Mbona anakuja mwenyewe ?!. Iweje kurudi mpaka arudishwe kwa usafiri binafsi ?!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpeleke mke wako kwa mamamkwe wako aendelee kupata uangalizi wa karibu mpaka atakapojifungua.
Mke sio wangu.. Angekuwa wangu mbona ilo swala lingekuwa limeisha kitambo sana
 
Binti arudi kwao,akishajifungua ndio harudi au mama mkwe aamie hapo kwa muda.....wakishindwana hapo waachane tu;watoto wazuri bado wako wengi tu
Wazo zuri ningekuwa mim simple tu..
 
Gharama ya mafuta ya kumpeleka huyo mama Mbagala siku 3 sawa na mshahara wa mfanyakazi wa ndani.
Acheni mambo ya ajabu wekeni mfanyakazi wa kike mkubwa mkubwa amsaidie mjamzito.

Mambo madogo ya kitoto kama hayo yanaweza kuvunja ndoa ya jamaa au kujenga chuki za ndugu wa wana ndoa.
Tatizo sio kila mtu anafikilia kama wew boss.. Wengine akili zao ziko tofauti sana aisee
 
Naomba unijibu maswali haya ndo nitatoa ushauri
1.huyo mama mkwe mume wake yupo?
2.mmeshindwa kutafuta mfanyakazi?
3.kwanini huyo mama mkwe asiondoke mapema asubiri hadi usiku?
4.ana dalili za kishirikina?maana wachawi ndo hiwa hawalali nje ya nyumba yao

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii ni jamaa yangu imemtokea .. Mama mkwe wake hana mume anakaaga na wajukuu wake
 
Very simple, jamaa atoe taarifa kuwa atakuwa na safari ya kikazi mwezi mzima tena nje ya nchi.
Hivyo aandae mchepuko akapumzike mqezi mzima na aweke whatsapp namba tofauti na namaba anayotumia.
Anapoondoka aache bajeti sawa na aiku atakazokuwa nje na balance kidogo.
Hizo siku amblock mke wabaki kuwasiliana whatsapp tena usiku tuu...
U
Mshauri mjinga sawa na ujinga wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahahhahahaha wazo zuri.. Sema hili kwa jamaa aliwezekani kabisa.
 
Hakuna namna zaidi ya kuwaambia wote wawili ukweli tena wakiwa pamoja! Kinachofanyika hapo ni kijana anaingizwa kwenye maisha ya kutawaliwa na familia ya mke wake na akizubaa watampanda kichwani! ameshaolewa atulie na afuate maagizo ya mumewake huyo mama akatulie kwake na kama akija plan ni kulala amasivyo awe amejipanga kwa nauli ya takisii . Kijana ita hata ndugu yako wa kike au hata mama yako huyo mkwe akizingua!
Kuna watu wamezidi sana upole kumchana mtu hawawezi..
 
Back
Top Bottom