Mama mkwe na mwana wote wanapiga mbonji kwangu

5525

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
5,412
6,273
Watu wa ukumbi huu, habari zenu.

Nimeoa na sasa nina watoto 2 alhamdullah, nampenda sana mke wangu lakini kuna jambo hili linaendelea kila uchao nahisi moyoni nimeanza kulichukia chukia.

Kuna muda mamamkwe amekuja kumsaidia ulezi wife wakati wa kujifungua lakini akapitiliza ule muda nilioambiwa na wife kama angekaa, sasa akawa anakaa kama ndio mahali pa kuishi. Yeye ni age kidogo, mama mtu mzima, hana mume.

Kuna kipindi huyu mama anaumwaumwa, mara ikaja ni kuhusu haya mambo yaliyoingia; sijui kapewa jini, mara shetani tafrani nyumbani mpaka sasa amesafirishwa mji wa pili kwa matibabu zaidi lakini nahisi akimaliza matibabu kama aturidi hapa kwangu.

Suala lingine naona shemeji yangu mtoto wa kiume shababi naye amekuja. Siku hiyo wife akaniambia leo shemeji yako, yaani mdogo wake, atalala hapa nikasema safi nikamtolea kitanda na godoro ili achape usingizi kwa siku ile, lakini naona siku ya pili kaendelea mpaka imefika kama wiki akasafiri kidogo kaenda kukaa kama siku 4 karudi yupo tunaendelea naye anachapa usingizi kama kawaida.

Nilijaribu kumuuliza wife ananimbia anafuatilia kitambulisho cha Taifa. Sasa mimi najiuliza, ivi unaweza kuacha shughuli zako siku zote kwa kitambulisho tu? Kuna siku akasema ile namba tayari ashapewa lakini mzee yupo ameganda tu na sasa pale home majukukumu yanaongezeka.

Naomba fatwa watu wa hapa, vipi niendelee kuvumilia maana hata uhuru pale nyumbani naona umebanwa kidogo.
 
je wangekuwa ni mama yako na mdogo wako wa kiume ungeona unabanwa??kama ni hapana basi jua hio ni roho mbaya,lakin kama ni ndio basi ni haki yako kudai uhuru!!

Lakini hapa nmeona kuna mambo mawili unayalalamikia,unakosa uhuru na majukumu yanaongezeka!kwa hali ya sasa ilivyo nakuelewa mkuu unapozungumzia majukumu kuongezeka,japo kuna watu watakuja apa watakwambia "mchoyo" au "unagubu"!!
 
Hautaki ndugu?! Si hua naskia ukioa au kuolewa ndugu wa mwenzio ni wako?!
Ndio maana niliwahi ku suggest humu ndani kuwa serikali ianzishe somo la ndoa mashuleni,tokea primary schools ili watu wajue kabisa kuwa unapo owa nini kinafuata,maana mtoa mada inaonekana hakutegemea haya kutokea,wakati hili kama ni somo lingekuwa ni la darasa la kwanza la mafunzo ya ndoa,yaani haya ni yale mambo mepesi mepesi ya kuanzia na yeye kashaanza kupanic saa hizi...
 
Ndio maana niliwahi ku suggest humu ndani kuwa serikali ianzishe somo la ndoa mashuleni,tokea primary schools ili watu wajue kabisa kuwa unapo owa nini kinafuata,maana mtoa mada inaonekana hakutegemea haya kutokea wakati hili kama ni somo lingekuwa ni la darasa la kwanza la mafunzo ya ndoa,yaani haya ni yale mambo mepesi mepesi ya kuanzia na yeye kashaanza kupanic saa hizi...
Wenzie wengi hawaoi kwa sababu wanaogopa majukumu ya kulea familia 2 yeye alioa akihisi anahangaika na mkewe tu

Yani ni hv ukinyanyapaa ndugu wa mwenzio ndo kumnyanyapaa na mwezio bila kujua
 
Jamani Africa tunakwama wapi? Umeona binti umempenda umeulizia bei gani (mahari) umelipa ili uachane nao kiroho safi! Kumbe ndo unaenda kubeba ukoo na utitiri wa ndugu kisa unaishi nyumba kubwa either umepanga au umejenga. Ungekuwa na chumba kimoja au chumba na sebure wangekuja? Africa! Tunakwama wapi?
 
Slimsalim,
Tayari wewe mwenyewe umeshasema ana roho mbaya, lakini akili zilipokujia kidogo ukasema unaelewa ugumu wa maisha halafu ukaishia kutahadharisha kuwa wengine watasema ana gubu, sasa mbona upo kama sigara kali, hueleweki wapi mbele nyuma wapi?

Waswahili mna shida sana. Na hii ni tabia ya kutopenda kujitafutia kiasi mnaamini akiwa nacho ndugu yako basi mkafunge kambi kwake.
 
Wanakuja tu dar familia ngapi zinaishi chumba na sebule na ndugu karibia watu8 humohumo na maisha yanaenda?!

Tuache utani wangekua ndugu wake yeye mwanaume angelalamika?!
Hii haijalishi ni ndugu wa nani wanazungumziwa hapa, tatizo ni USWAHILI. Unaongea kwa uchungu kwa kuwa hata sasa unaishi kwa shemeji yako eeh? Toka hapo mama nenda kwako, utaharibu ndoa ya dadaako. Tujifunze pia kuzaa kwa mpango
 
Watu wa ukumbi huu, habari zenu.

Nimeoa na sasa nina watoto 2 alhamdullah, nampenda sana mke wangu lakini kuna jambo hili linaendelea kila uchao nahisi moyoni nimeanza kulichukia chukia.

Kuna muda mamamkwe amekuja kumsaidia ulezi wife wakati wa kujifungua lakini akapitiliza ule muda nilioambiwa na wife kama angekaa, sasa akawa anakaa kama ndio mahali pa kuishi. Yeye ni age kidogo, mama mtu mzima, hana mume.

Kuna kipindi huyu mama anaumwaumwa, mara ikaja ni kuhusu haya mambo yaliyoingia; sijui kapewa jini, mara shetani tafrani nyumbani mpaka sasa amesafirishwa mji wa pili kwa matibabu zaidi lakini nahisi akimaliza matibabu kama aturidi hapa kwangu.

Suala lingine naona shemeji yangu mtoto wa kiume shababi naye amekuja. Siku hiyo wife akaniambia leo shemeji yako, yaani mdogo wake, atalala hapa nikasema safi nikamtolea kitanda na godoro ili achape usingizi kwa siku ile, lakini naona siku ya pili kaendelea mpaka imefika kama wiki akasafiri kidogo kaenda kukaa kama siku 4 karudi yupo tunaendelea naye anachapa usingizi kama kawaida.

Nilijaribu kumuuliza wife ananimbia anafuatilia kitambulisho cha Taifa. Sasa mimi najiuliza, ivi unaweza kuacha shughuli zako siku zote kwa kitambulisho tu? Kuna siku akasema ile namba tayari ashapewa lakini mzee yupo ameganda tu na sasa pale home majukukumu yanaongezeka.

Naomba fatwa watu wa hapa, vipi niendelee kuvumilia maana hata uhuru pale nyumbani naona umebanwa kidogo.

Shida ipo wapi? Mama mkwe ni Mama yako, Dogo maisha yamekwama msaidie, ndo tunavyoishi, wewe unapenda tu Dada yao?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom