Mama mkwe na mke wangu


Daa! Pole sana Mkuu hii inaumiza sana. Na ukute kwa wakwe zake hata kuwajulia hali haja wahi.
 

Ndiyo uchelewe kurudi home kisa mama halafu akiwa hanatatizo kabisa. Na unashindwa kutimiza majukumu yako kisingizio mama hivi na mume akiamua kushinda kwa wazazi wake kila wikiendi hiyo itakua ndoa? Ndoa nyingi wanawake ni tatizo.
 
Hii yote Inaelekea bado hamjapata watoto. Mke akishazaa taratibu atamsahau mama yake na ataamishia ukaribu kwa mtoto.... we mpe mimba ndio dawa.
 
Ishi na mwanamke kiakili

sasa si bora awe close na mama yake kuliko apate shosti shangingi amuuunganishe na vibuzi?

jaribu kumnunulia mama mkwe zawadi umpe mkeo ampelekee uone utakavyo pendwa zaidi..........

Could you pls tell the day you were born mkuu? That was a super click to the situation.

Mtoa hoja atakuwa amepata alili sasa
 
We jamaa unanishangaza sana. Sasa ulitaka wachukiane? Au unampenda pia mkweo kiaina wanakubana kupata kitoweo cha kuku na yai lake? Hujasema kabisa kinachokufanya wanakuboa ni nini hasa? Kupigiana simu? Ulitaka akupigie nawe hapohapo kitandani?
 
Pole mkuu. Nachokushauri hapa sidhani kama sahihi ila ningefanya mimi. Nakushauri usimwambie siri zako za ndani na mitikasi,punguza kufanya mapenzi na yeye,tafuta marafiki au kama una mtoto spend time nayeye. Mwache afanye atakalo. Wanawake wasikuumize kichwa kabisa mkuu. Mwache ajifukuzishe .hapa naloona huwezi hua ni lipi wanalipanfa yeye na mama yake. Wanawake nj watu very dangerous mkuu. Usione huruma. Keep distance as well.
 

Nahisi unakula ugoro, ndo ushauri gani huu? yaani mtu kuelewana na mamaake atafutiwe nyumba ndogo? Bado si solution.
 
Bunyu,
Mtu kuongea na mama ake mzazi hata mara nne kwa siku ndio chanzo cha nongwa yenyewe au kuna lingine? Mara nne? Unaposema hata mara nne ni kwamba maximum kwa siku wanaweza kuongea kwa simu hata mara nne lakini wakati mwingine chini ya hapo! Kwani hizo mara nne kwa siku watatumia muda gani? Heri basi ingekuwa hizo mara nne ni kuongea na dada zake ambao ungehisi labda wanamtafutia mabwana lakini mamake! Kama ana tabia ya kwenda kwenda kwao bila sababu za msingi hapo ningekuunga mkono kwa 100%!

Hilo la kwamba kikwenu jina la mwisho la mke wako linapaswa kuwa lako hilo wala sio suala la kikwenu... hayo ni mambo ya kizungu.
 
Last edited by a moderator:
naona wachangiaji wengi wanachokiona sana hapa ni simu kati ya mke na mkwe/mama,japo mleta mada amekuja mara 2 hapa naamini bado hajafunguka vya kutosha kuhusu matatizo anayoyasababisha huyu mkwe ktk ndoa yake.Aliporejea mara ya pili ameonyesha tatizo la mazoea mke kurudi kwake usiku tena pasipo taarifa za kufanya hivyo na kinga ya huyu mke kufanya hivyo ni mkwe,sasa kitu anachotaka mleta mada kusaidiwa ni kumuonyesha ni nafasi ya huyu mke ktk ndoa yake.Kuoa hakumaanishi tu kulala na mke usiku km walivyoshauri baadhi ya wachangiaji kuwa km unapata haki yako usijali mengineyo,tunaweza kuta mleta mada ana upweke wa hali ya juu hivyo muda mwingi anamwitaji mkewe awe mtu wake wa karibu lkn badala yake ukaribu upo kwa mkwe.
Mkuu tumia muda mwingi kumsoma mkeo kitu ambacho pengine haukukifanya wakati wa uchumba,pengine mkeo hana mapenzi na wewe
 
We jamaa unanishangaza sana. Sasa ulitaka wachukiane? Au unampenda pia mkweo kiaina wanakubana kupata kitoweo cha kuku na yai lake? Hujasema kabisa kinachokufanya wanakuboa ni nini hasa? Kupigiana simu? Ulitaka akupigie nawe hapohapo kitandani?

Nilipokuwa sijaoa, nilikuwa naangalia matatizo ya ndoa za rafiki.zangu, ndugu zangu ili nijifunze lkn siyo kutoa maoni nikiwa na attitude kama yako, you are not in my shoes, na nadhani haujaoa, kama umeoa wewe ni aina ya wanaume wanaokubali kwenda kuishi seating room ya nyumbani kwa wakwe au ktk baadhi ya vyumba under the ver same roof na wakwe zako!! Au inawezekana ww ni mwanamke so, haufahamu how it feels like!!!

Na hata kichwa chako na mdomo wako na vidole vyako vinaonesha ww ni mtu wa aina gani, hadi kunambia au nataka kulala na mama mkwe wangu!!!! Mungu akusamehe but you better learn good manners!!!!!
 

mmmmm. ok ongea na mkeo ikishindikana ongea na mama yake coz mama wa mkeo ni mama yako pia.
 
Hili suala linaumiza bana unaoa lkn mkeo masaa 24 ni mamaa,Mnapanga kitu pamoja then baadaye anamwambia mama yake,kupiga piga simu kila mara kwa mama, Sio poa hii.Mpe mumeo nafasi ya kwanza thn wengine later.
 

Isiwe too much sasa,
 
Kwanza mkuu, nikiri kwamba siwezi kuingia kwenye kiatu chako wewe uliye na fikra kama hizo ambazo wenye akili timamu hawawezi kumsema mke na mkwe kwenye jamvi la kadamnasi. Sithubutu oooh! Asante kulitambua hilo mwanzoni kabisa. Pili, mimi ni kidume ninayejua raha na karaha za ndoa lakini naegemea kwenye raha zaidi, kwa kuwa ukitaka kuona raha ya ndoa unapaswa kuepuka fikra za kipuuzi kama ulizo nazo. (Darasa hilo usichukie samahani). Kubali kujishusha ufanane na interest za mwenza wako, uwe mume au mke - wote jitahidi sana kubalance interest hata kama kwa maumivu Fulani, kwa kuwa mume namke sasa ni mwili mmoja japo akili tofauti. WEWE ndiye kichwa cha familia na unapaswa kuwa na control ya mwenendo wa maisha ya kifamilia. Mambo mengi yaliyo matatizo ya wanandoa hayasuluhishwi JF bali kitandani kwenu 6x6. Unazo namna nyingi za kusyaendea hadi achievement. Mtu ----- anatarajia jamaa wa nje ya familia kutatua matatizo ya familia yake bila kuona impact hasi atakazokumbana nazo kusimulia mambo ya familia yake. Kila familia inazo adha zake na raha zake. Jirani yako unapomwona anafurahia sana ndoa yake usidhani yeye ndo kapata sana kukuzidi na kwamba hana adha. Matatizo ndani ya familia yako ndio kipimo cha ukomavu wako na mapenzi uliyo nayo kwa mkeo au mumeo.

Unajuaje, labda wewe ndio unamboa zaidi mkeo hata anaona aliwazwe na mama yake? kama angekuwa lofa kama wewe akapeleka kwenye majamvi ya kusuka nywele na kupaka rangi vidole na makucha, unadhani ingekuwa vipi? Nakuhakikishia ungepata wasaidizi kibao wale wapaka rangi wangekuwa wa kwanza. Au hujui wanawake wanapenda kupakwa rangi na vijana wa kiume? Huyo mkeo nahisi ulitafutiwa na au mlikutana chapchap, maana ungeshawajua wanavyopendana na mama yake hata kabla hajaingia ndani. Au labda ni mshikaji wako tu concubine unaishio naye ukambatiza title ya mkeo. Maana Mke au mume wa ukweli hawasemani nje ya familia ati? Unyago mnafundishwaga kwenu? mapungufu ya unyago ndo haya hapa. Unyago sio lazima kukatwa ngozi, ni mafunzo muhimu juu ya namna ya kuishi na watu mbalimbali, kukomaa katika maisha, uvumilivu na utu wema kwa wengine, kupevushwa akili, elimu ya kufikia kiwango cha utu uzima. Siamini wewe umepitia mafunzo hayo digital.com wewe. kama ulipitia, basi wewe kilaza sana hukushika uliyofunzwa, au ndio wale ambao anaandika notes na hazisomi bali anaweka kwenye mkoba anatembea na begi la kila alichokiandika tangu day one mpaka siku ya mwisho lakini hajawahi kusoma alichokiandika yeye mwenyewe, Division 6 yaja kwa ajili yao (special, ngoja tupige debe kwa Kawambwa awakumbuke kuwatungia sera na watu wa aina yako)

Sikutaka kuingia ndani sana lakini umenichokoza kwa kuwa umekuwa toto tundu. Mtoto Zero. Nimeamua nikupe kionjo kidogo upevuke akili. Huenda hutanielewa na hapa, utalalama tu maana vijana wa kurapu hamchelewi kuanika upuzi wenu ndo maana suruali zenu zinavaliwa mwisho magotini kutoka juu mkituanikia masaburi yenu hata kuyafanya yashuke thamani na kukaushwa na jua kwa kuanikwa sana. Haya, nimalize kwa kukushauri umheshimu mkeo na mkweo, domo hilo liko wazi kwa sababu wao wamekuheshimu sana. Jifunze kuwa na subira, kabla hujaanika mambo ya ndani tafakari kwanza au basi kamuulize best man wako (kama unaye, nina shaka hapo) atakuambia nini kinafaa kuanikwa na nini hakifai. Sawa kijana?

Byeeee.
 
to me naona si sawa anakosea ila usijaribu kumwambia apunguze karibu italeta shida
 
huna heshima ww wala hujui maana ya ndoa ww
 
km unataka akudekee ww piga mashine sawasawa sio mchezo mchezo
 
hapa issue so kuongea na mama yake Mara ngapi kwa siku... Issue ni kwamba anatumia muda mwingi kwa mama yake mzazi kuliko kwa mmewe kitu ambacho sio kizuri kwa ustawi wa ndoa yao. Haiwezekan unaenda kwa mama yako unakaa mpaka saa tatu usiku... bila shaka hii tabia inajirudiarudia. Kama mke lazima ujue wajibu wako vivyohivyo kwa Mme. Ongea na mkeo mwambie hupendezi na tabia na tabia take, asipobadilika inanidi uhame uende sehemu ambayo si rahisi kwenda kwa mama au mama kuja. Wabaki wakipigiana simu tu.
 
na uwe mahaba unayajua km huyajui ww unafkiria ndoa ni heshima tu imekula kwako akija akikutana na sharukan ndo utakimbiwa kabisaa
 
ujue nashangaa sana wakuu yani mm nije nimuoe dada yako then nimpige marufuku mazoea na mamaake inaingia kweli akilin?huyo mkwe ndo kakutunzia leo hii marufuku ustuzingue kabisaaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…