Mama Mkwe kasababisha nimpe mimba mke wa mtu!

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,566
Miaka michache nyuma, nikiwa ndiyo nimemalizia shahada yangu ya pili na kuanza kazi kwenye kampuni moja ya Insurance, nilibahatika kukutana na dada mmoja, mpole na mwenye muonekano wa unyenyekevu na tabia njema. Nilimpenda, akanipenda tukaamua kuwa wapenzi.

Baada ya miezi kama tisa hivi ya mawasiliano ya karibu mno, niliamua kwenda kujitambulisha kwao na nilipokelewa vzr mno na mama mkwe(bamkwe alitangulia mbele za hakii). Mamkwe aliniambia amefurahi kumpata kijana kama mimi kupitia kwa mwanae. Na pia alisisitiza kuwa mwanae ni binti mwenye tabia njema na hakuwahi kumletea kijana hapo nyumbani isipokuwa mimi. Nilifurahi.
Pamoja na kuwa na uhusiano wa karibu, bado mimi na huyu dada hatukuwa tunaishi nyumba moja ingawa yeye alikuwa akija nyumbani na kukaa hata wiki kabla ya kurudi kwake. Miezi michache baadaye mpenzi wangu alipata mimba. Sikuona kama tatizo sana maana nilijua kuwa hali kama hiyo ingeweza kutokea.

Cha ajabu wiki chache zilizopita, nilipokea ujumbe kwa mtu mwanaume nisiyemfahamu kuwa kuna ishu muhimu mno anataka kuongea nami ana kwa ana. Nilikataa. Baadaye yule kaka aliniletea ushahidi wa cheti cha ndoa na picha za harusi kuwa mpenzi wangu ni mkewe halali wa ndoa. Nilishangaa mno.

Nilipokuja kumbana mpenzi wangu alikiri kuwa alikuwa ameolewa kwa ndoa ila walitengana na mumewe kwa sababu za kifamilia na migogoro. Nilipombana mamkwe naye alikiri kuwa mwanae alikuwa ameolewa na walinidanganya ili wasije kunikosa.

Naomba ushauri jamani maana binti ana mimba, na mumewe naye anataka mkewe! Niwafanyaje hawa mtu na mamaye kwa uovu walionitendea? Ushauri pliz!

**** Haya yamemkuta rafiki yangu mmoja ambaye alinitafuta kuomba ushauri. Nami bila hiana nimeona niwafikishie wana JF wenzangu kupata mawazo yenu ****

Wenu,
HorsePower R. Kufakunoga
 
Alimshikisha nanihii akamsaidia kumwekea huyo mke wa mtu.
Kwa nini asimlaumu huyo dada?
Unadhani loyalty ya yule mama ilitakiwa iwe kwa mwanaume au kwa mwanae?

Wote watatu vichwa panzi. Cha kufanya arudi kijijini kwao akaoe haraka sana.
 
Huyu rafiki yangu, anachosikitika ni kuwa mama mkwe alimdanganya kuwa mwanae hajaolewa wala kuwa na mpenzi hivyo yeye akaamini kuwa ndiyo kijana halali wa huyo dada mpaka kufikia hatua ya kupeana mimba.
Nafiki Kongosho utakuwa umeelewa
 
Utalaumuje third party katika contract ya watu wawili?
Nilitegemea awe na hasira zaidi kwa yule dada kuliko mama mkwe.
Labda wana dhiki mama alliona wamepata mgodi, mwenye shida ni aliyeamua kuuleta mgodi kama Nazir.
 
Ana hakika gani kama hiyo mimba kweli ni ya kwake?
Inawezekana ni changa la macho.....
Anza mbele haraka...
 
Mama anayeshirikiana na mwanae kuficha mambo makubwa kama hayo ni mbaya sana. Asijaribu kulazimisha kuwa na mke wa mtu. Isijekuwa hata hiyo mimba kabambikizwa. Mkwe hafai mdada nae hafai kabisa.

Amwache huyo mke wa mtu, akijifungua wakapime DNA, kama mtoto ni wake amlee manake mtoto hana makosa.
 
mkuu huyo jamaa ako alishindwa kusomaa nyakati,kaambiwa na mama mkwe mwanae hakuanga na mwanaume,je?alimkutaa slidii aka kata yeye utepe,pili iategemea ni ndoa ya kanisani amaa,kwani ndo haivunjiki...je anauwakikaa mimba ni yake?afanye uchunguziiii ajue akiona vipi akimbie harakaa
Huyu rafiki yangu, anachosikitika ni kuwa mama mkwe alimdanganya kuwa mwanae hajaolewa wala kuwa na mpenzi hivyo yeye akaamini kuwa ndiyo kijana halali wa huyo dada mpaka kufikia hatua ya kupeana mimba.
Nafiki Kongosho utakuwa umeelewa
 
Wa kumlaumu ni huyo mdada mke wa mtu,
Kwann akubali kuwa na ww ile hali anajua ana mumewe?
Huyo mama mkwe asingemjua km usingepelekwa na huyo mdada,
Aachane na mke wa mtu,asubiri mtoto azaliwe ndio ujue km ni wake au wa mwenye mke,
Mke wa mtu sumu,jaman!
 
Huyo mwanamke ndio wa kwanza kulaumiwa...pia mama mkwe anafuata kwa kufanya maujinga hayo!
lakini bana mambo mengine huwa ni wivu usioeleweka, unaweza kukuta mtu na mkewe wanaachana for more than ten yrs jamaa wala hana time kabisa. ila mwanamke akishachukuliwa tu ndio utaona ex anarudi sasa ooh alikuwa wangu ooh eti tulikuwa tunapendana na vipicha-picha kibao na vyeti vya ndoa! sasa muda wote ulikua wapi...kama ni mie nakuzibua kwanza makofi
 
HP na wewe una mambo..duh...kwanza vipi yule jirani wako wa jana leo ulimpa lifti tena...!!?
 
Hawana utu hiyo familia.
Cha maana mwambie best yako ajipange tu kulea damu yake. Asijione nimkosaji.nukta
 
Tatizo kubwa hapa ni mwanaume anayetaka kuoa. Sheria inasema uoe kwanza ndio uonje. kama angetangaza ndoa rasmi lazima wasamalia wema wangemtonya. hizi sheria zina maana yake na ukijifanya kukwapua lazima upatikane. POLE CHUKUA ZIGO LAKO NA URUDISHE MAHALI
 
Na pia alisisitiza kuwa mwanae ni binti mwenye tabia njema na hakuwahi kumletea kijana hapo nyumbani isipokuwa mimi. Nilifurahi.
Pamoja na kuwa na uhusiano wa karibu, bado mimi na huyu dada hatukuwa tunaishi nyumba moja ingawa yeye alikuwa akija nyumbani na kukaa hata wiki kabla ya kurudi kwake. Miezi michache baadaye mpenzi wangu alipata mimb

Nilipokuja kumbana mpenzi wangu alikiri kuwa alikuwa ameolewa kwa ndoa ila walitengana na mumewe kwa sababu za kifamilia na migogoro. Nilipombana mamkwe naye alikiri kuwa mwanae alikuwa ameolewa na walinidanganya ili wasije kunikosa.

Mpe pole sana huyo rafiki yako, na kisaikolojia mpaka mtu kukuelezea ishu nyeti kama hizi inaashiria mnaukaribU sana katika urafiki wenu (Mungu awazidishie mapenzi).

Inavyoonesha huyo binti na mama yake hawakuwa na uhakika kama jamaa angeweza kumrudia mkewe, ila ingetakiwa wachukue hatua za kumlazimisha muwewe ampe talaka kabla ya kuanzisha uhusiano na mme mpya.

Pili, nampongeza rafiki yako kwa kwenda kwa wakwe kabla ila ilipaswa wasigongane kwanza kabla ya kufunga ndoa maana lau wangefunga ndoa basi huyu mme mpya angepata sauti kupitia cheti cha ndoa ya kuwa ni mkewe halali.

Kuhusu mtoto subiri kwanza azaliwe then kitachomsaidia ni DNA tuu, ili achukue mtoto wake.
 
Pole sana, wala huyo mtoto huna hakika kama wako au wa huyo jamaa na mke anapokua na mumewe mtoto anakua wa mume alomuoa na kwa unyama alofanya huyo mwanamke na mama yake sidhani kama bado unaamini kama huyo mtoto ni wako. wasikupoteze mda tena shukuru mungu umejua mapema kabla huja aibika siku ya harusi....
 
Back
Top Bottom