Powel Mizengo
Senior Member
- Jan 20, 2014
- 126
- 24
Nilikuwa na mpenzi wangu tulisoma wote chuoni na tulipendana sana kiasi kwamba nilikuwa namgaramia kwa kiasi kikubwa na kuna kipindi aliumwa akalazwa hospitalini mimi nikawa siattend vipindi kwa ajili ya kumuhudumia yeye.
Zaidi nilishaenda nae kwao japo sikwenda kwa utambulisho rasmi lakini wazazi wake walielewa kuwa mimi ni mtarajiwa kwa binti yao!Wazazi wake walitokea kunipenda saana hasa mama mkwe ndiyo alikuwa ananipenda mpaka naogopa yani nikienda kwao napokelewa kama Rais vile sasa sijui ni kwa sababu nilikuwa naprovide mahela sana ila nachojua nilikuwa napendwa na hao wazazi!
Tuliporejea chuoni kwa masomo mwenzangu tabia yake ikaanza kubadilika akawa anaondoka chuoni sometimes haniagi na nikimpigia simu hapokei!mi nikawa nashinda kumtafuta kila kona ya hosteli bila kupata!Nikaja kuambiwa kuwa jamaa yangu wa karibu ambaye ni mfanya biashara alikuwa akitoka naye! Mi sikuamini!Hali iliendelea hivyo mpaka mimi nikaja kuhitimu masomo yeye nikamwacha akimalizia mwaka wake wa mwisho nilipoondoka mambo kwake yakazidi kuwa balaa alikuwa anatembea na yeyote atakayemtangulizia pesa!Nilikuja kusikia kuwa ametembea na mfagia vyoo vya hosteli akampa 60elfu! Hapo mi niliamua kumpiga chini baada ya kugundua ukweli wa mambo anayoyafanya! Sasa wazazi wake bado naendelea kuwa na mahusiano nao mazuri sometimes nawatumia pesa za matumizi licha ya kwamba wanajua binti yao sipo naye ktk mahusiano ya kimapenzi zaidi ya mawasiliano na tunaitana kaka na dada!
Sasa Mama yake alinipigia simu akaniuliza "endapo binti yake atakuwa amebadilika kitabia na akataka turudiane Je niko tayari?" Mi nimemjibu sipo tayari,Basi tokea hapo yule mama ananing'ang'aniza akanambia nimwoe hata mdogo wake na yule mdada niliyekuwa naye! Sasa wadau naomba ushauri nifanyaje manake napatwa na kigugumizi manake hata huyo mdogo wake ni mzuri sana wa umbo ila sijajua tabia yake!Na je ntakuwa sahihi endapo nitaoa mdogo mtu!?