Kima mdogo
JF-Expert Member
- Sep 17, 2011
- 303
- 46
Habarini waungwana,.. Kwa muda mrefu nilikua nikielezwa kuwa mama mkwe wangu hataki niishi na mwanae na alikua anamshawishi mume wangu aniache na amuoe mwanamke aliyemtafuta yeye kwa madai alimzaa mume wangu ili akija kuoa mwali wake akaenaye,Jambo ambalo kiukweli alishanieleza kw napaswa kumuacha mume wangu dar.Nikaish naye Machame na nililipinga,Hvy akaamua kumshawish mume wangu aniache lakini mume wangu alikataa katakata.wiki 2 zilizopita nilipewa taarifa na shangazi wa mume wangu kuwa mama mkwe wangu kaenda kwa mganga kumtafutia mume wangu dawa ili aachane na mimi,Na anapanga safari ya kuja dar ili akamilishe mia yake...Nilipokea niliyoelezwa na kunyamaza kimya na siku 2 badae mama mkwe wangu alinipigia simu kuwa anakuja kututembelea,alipokuja nilimpokea vizuri na baada ya siku 2 kupita nilimfuma mezani akiweka dada dawa nyeusi kwenye chai niliyokua nimemuandalia mume wangu,nilishtuka na yeye alishtuka sana,Sikumuuliza chcht.Niliamua kupika chai nyingne na kuimwaga ile.Je nifanyaje waungwana?