Mama mdogo amegoma kutumia ARV, nifanyaje?

Mama mdogo amegoma kutumia ARV, nifanyaje?

Huo umri wa miaka 27 bado anahitajika sana kwa malezi ya mwanae na taifa kwa ujumla.Mtieni moyo,na mfate shauri mbalimbali zinazotolewa na wadau humu,hasa lile la waathirika wenzake wanaotumia dawa.
Ana nafasi nyingine ya kutengeneza maisha yako.Pole sana kwa yanayokukuta
 
Kama vipi mbadilishieni lishe ya kula chakula awe anakula vizuri mlo kamili wa protein, wanga na vyakula vya mafuta kwa wingi i.e asubuhi chai ya maziwa, mayai, sausages, karanga, mchana ugali wa dona, samaki, nyama, kuku, matunda i.e parachichi, tikiti, ma apple, machungwa jioni juice safi, salad salad kwa wingi yani kwa kifupi awe mtu wa misosi mingi maana asikwambie mtu huu ugonjwa hata wanaotumia ARV chakula chao cha asubuhi mtu uliemzima huwezi kukila unakuta mtu anakula chai vikombe 5 mkate mzima, chapati 8, mayai, sambusa matikiti makubwa mawili akimaliza anameza dawa yani breakfast yao mtu anatumia saa nzima kula
Acha uongo Mkuu.
Lishe ya mtu anaetumia dawa ni sawa tu na mtu was kawaida.
Habari ya vikombe vitano umetoa wapi?
 
Kwasasa wameshatoa sindano ya ArV ambayo ukichoma unakaa wiki 8 ndio unachoma tena.. zimeshafika Rwanda, yamkini hizo atazikubali
 
5EF988DB-1C85-4F64-88B4-9045FB52943A.jpeg
2CFCD9D8-C5AB-405D-B228-846FCA112DBA.jpeg
1A2BB572-EFAC-4099-B370-FD3E12938490.jpeg
 
Sababu ya kuacha ni nini?
Hataki watu wajue kama ni muathirika. wakati tushajua na ni mtu mzima kweli bora angekua msichana tungesema anahofia vidole ...
mtihani unakuja kuuguza sasa[emoji22]
Ngoma ikishaanza Nyonde nyonde, nyonde nyonde kuchiwileeeeee... na sio Ukimwi tu sikuhizi maradhi tu mengi hayana kurudi nyuma ukishavuka week3 unaumwa
 
Hizi mada za HIV/AIDS sasa siku ya UKIMWI imepita mtaziendeleza au tungojee tena siku ya UKIMWI 2020?
 
Kwa mtu ambaye kaupata kwa kufanya zinaa kwa makusudi kabisa huku akijua UKIMWI upo na hakutaka kujali hawezi kukataa kunywa dawa,ila sababu nyingine yoyote kinyume cha hapo huweza kumfanya mtu akakataa kuacha kutumia dawa kwakuwa anaona kwamba kaupata kwa hali ambayo alijitahidi kujiepusha lakini bado kaupata au wengine ni wale waliotumia dawa muda mrefu ikafikia haoni nafuu zaidi ya mateso ya kumeza hizo dawa......
 
Mwambie ale vizuri, vyakula kama chapati, maandaz, wali, ugali soda aachane navyo. Afya yake itakuwa nzr.
Aanze siku kwa kula supu badala ya kula chai na chapati. Apendelee kutumia Mayai, Nyama mboga za maji kwa uwingi.
 
Huyu dada inaonekana ana hasira amepewa ugonjwa bila kutegemea au amepewa na mtu wake wa karibu hivyo ana hasira.
Jaribuni kutumia watu wa coucelling.Pia ajue ukimwi hauui kinachoua ni magonjwa nyemelezi.Nina ndugu yangu mwaka wa 20 sasa ndugu yangu aliupata anatumia vidonge ana afya huwezi jua awali ya yote kamrudia mungu wake.Mungu ni wa mijiza.Ndugu yetu ana miaka 65 sasa kasomesha wanawe wote ni watu wazima wanajitegemea.Mshaurini kiimani anachofanya ni dhambi hata akitangulia mbele za haki atahukumiwa kwa kutesa wanawe.
Tafuteni washauri wa kidini pia
 
Magonjwa nyemelezi yakimvagaa atakumbuka tu ARV...
 
Back
Top Bottom