Mama mdogo amegoma kutumia ARV, nifanyaje?

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,317
7,509
Mama yangu mdogo tangu ameambukizwa Virusi Vya Ukimwi miaka 2 iliyopita amekataa kata kata kutumia dawa za ARV ili kuongeza maisha.

Amekuwa mbishi, licha ya kushauriwa na madaktari, anadai ni bora afe na ana umri wa miaka 27 na mtoto mmoja wa kike wa miaka 6 ambaye alimzaa kabla ya kuambukizwa HIV.

Afya yake kwa kweli imedhofika hadi huruma, anashauriwa atumie dawa ili amtunze mwanae, anakataa kata kata.

Mwenye mbinu mbadala anisaidie ili huyu ndugu yangu atumie dawa, tangu agundulike hajawahi kutumia dawa za ARV miaka 2 sasa na afya yake ni mbaya sana.
 
Hamna namna hizo dawa zikawekwa kwenye chakula akala bila yeye kujua?, japo dawa nyingine huwa effective zinapomezwa moja kwa moja.
Wataalam wa afya tia neno hapa.
 
Kama vipi mbadilishieni lishe ya kula chakula awe anakula vizuri mlo kamili wa protein, wanga na vyakula vya mafuta kwa wingi i.e asubuhi chai ya maziwa, mayai, sausages, karanga, mchana ugali wa dona, samaki, nyama, kuku, matunda i.e parachichi, tikiti, ma apple, machungwa jioni juice safi, salad salad kwa wingi yani kwa kifupi awe mtu wa misosi mingi maana asikwambie mtu huu ugonjwa hata wanaotumia ARV chakula chao cha asubuhi mtu uliemzima huwezi kukila unakuta mtu anakula chai vikombe 5 mkate mzima, chapati 8, mayai, sambusa matikiti makubwa mawili akimaliza anameza dawa yani breakfast yao mtu anatumia saa nzima kula
 
Hamna namna hizo dawa zikawekwa kwenye chakula akala bila yeye kujua?, japo dawa nyingine huwa effective zinapomezwa moja kwa moja.
Wataalam wa afya tia neno hapa.
Itawezekana kweli
 
Hapo sidhani kama kuna cha kufanya zaidi ya mgonjwa mwenyewe kukubaliana na hali aliyonayo. Ukiangalia kwenye ukweli halisi wa life expectancy ya mtanzania ni miaka nadhani 61 - 64 hivi.Kwa mtu ambaye amekutwa na HIV na anatumia dawa za hospitali,basi kwa wastani anaongeza miaka 40.

Sasa mama yako mdogo ana miaka 27 kama akitumia dawa ataishi mpaka karibia miaka 70 ambayo ni umri wa kawaida kabisa kurudi mbele za haki. Kikubwa hapo ni elimu na ushauri, na afahamu kuwa kwa kutomeza dawa, Ukimwi wenyewe haukuui, ila unasababisha kifo cha taratibu na mateso ya magonjwa nyemelezi.

Nipo kwenye fani ya afya kwa miaka mingi sana,na hizo ARV zinaokoa maisha ya watu wengi. Ukimwi sio ticket ya kufa kama miaka ya themanini na tisini. Akubali hali yake basi maisha yanasonga. Bahati mbaya sipo Tanzania,kama ningekuwepo ningejitolea kuongea naye nione kama kuna mwelekeo.
 
Ni kweli,lakini anashauriwa anakataa anabaki analia tu

Hicho ndio kitamuua na si kingine maana kama analia maana yake ni ana mawazo na kama ana mawazo hali vyemaa na kama hali vyema lazima apatwe na upungufu wa kinga mwilini
Aache mawazo akila vyema asikae peke yake atakuwa poa dawa za Arv ndio zinamaliza watu aiseee
 
Mama yangu mdogo tangu ameambukizwa Virusi Vya Ukimwi miaka 2 iliyopita amekataa kata kata kutumia dawa za ARV ili kuongeza maisha.

Amekuwa mbishi, licha ya kushauriwa na madaktari, anadai ni bora afe na ana umri wa miaka 27 na mtoto mmoja wa kike wa miaka 6 ambaye alimzaa kabla ya kuambukizwa HIV.

Afya yake kwa kweli imedhofika hadi huruma, anashauriwa atumie dawa ili amtunze mwanae, anakataa kata kata.

Mwenye mbinu mbadala anisaidie ili huyu ndugu yangu atumie dawa, tangu agundulike hajawahi kutumia dawa za ARV miaka 2 sasa na afya yake ni mbaya sana.

Mi nashauri kama mngeweza kuwapata watu wengine wenye hali kama yake, ikiwezekana wa rika moja na yeye na waliomzidi au wadogo wanaotumia dawa hizo... washirikishane experiences na walioyapitia mpaka wakawa hapo walipofikia, then wamshauri na yeye.. mkiwa wazima pekee mnaomzunguka na kunshauri anapata feelings kwamba hamuelewi anajisikiaje..
 
Mama yangu mdogo tangu ameambukizwa Virusi Vya Ukimwi miaka 2 iliyopita amekataa kata kata kutumia dawa za ARV ili kuongeza maisha.

Amekuwa mbishi, licha ya kushauriwa na madaktari, anadai ni bora afe na ana umri wa miaka 27 na mtoto mmoja wa kike wa miaka 6 ambaye alimzaa kabla ya kuambukizwa HIV.

Afya yake kwa kweli imedhofika hadi huruma, anashauriwa atumie dawa ili amtunze mwanae, anakataa kata kata.

Mwenye mbinu mbadala anisaidie ili huyu ndugu yangu atumie dawa, tangu agundulike hajawahi kutumia dawa za ARV miaka 2 sasa na afya yake ni mbaya sana.
Anakataa kwa nini hasa? Aliwhi kutumia kidogo kikamletea madhara? Huwa anasema hataki kwa kutoa sababu gani? Kama mdau mmoja alivyoshauri, mngetumia watu waliwahi kuugua,wakatumia na kupata nafuu. Hao watampa moyo zaidi.
 
Akiugua vitu vingine kama malaria anatumia dawa au hataki dawa ya aina yoyote ????
 
Back
Top Bottom