Mama mbaroni kwa kumuua mwanaye wa miezi saba

Mama mbaroni kwa kumuua mwanaye wa miezi saba

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
wakuu
======
kuna watu wana roho mbaya sana imagine unamwua malaika kuna dhambi hazina msamaha

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Zuhura Juma Matengo kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa miezi saba aitwaye Shufaa Abdallah, na kujeruhi watu wengine wawili waliofahamika kwa majina ya Agnes Mathias na Suleiman Abdallah.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro, amesema tukio hilo limetokea Juni 30 mwaka huu, saa sita mchana, katika maeneo ya Nyumbanyeupe, Mbagala, Wilaya ya Temeke ambapo inadaiwa kuwa mtuhumiwa alitumia kitu chenye ncha kali kutekeleza mauaji hayo.
 
Back
Top Bottom