Mama Kilango ingekuwa vyema kama pia ungepigia kelele ufisadi unaotokea katika mahospitali yetu, kuna watu wanakufa kwa kukosa elfu tano ya kumpa nesi ili aongezewe damu, kuna watu wanafia hospitali kisa hawana vifaa vya kujifungulia, wananchi wanashindwa kusafirisha mazao yao kwa ajili ya kukosa miundombinu bora itakayowaunganisha na masoko ya mazao yao mijini, Je hili sio la kulipigia kelele kuliko hilo suala la EPA? Je hii ni nguvu ya soda kutuzuga wadanganyika tunyamaze kusema kuhusu mengine?
Nilidhani hapatakalika pale ambao bajeti ilionekana ina mapungufu mengi na sana waziri wa fedha kuonekana incompetent hadi asaidiwe? Je mama hili kwake lilikuwa halina haja ya kupigiwa kelele?
Kuna mwamko wa tofauti miongoni mwa wananchi mchungaji fanya uchunguzi utajua hilo!
Mafisadi hawafai kushirikishwa katika kujadili mustakabali wa taifa and they belong in prisons lakini ni muhimu kupata jibu la swali hili: who is fisadi? the notion that being out of CCM is being non-fisadi is something I just cant agree.
Swala la yeye kuunga bajeti mia kwa mia hilo nalo mie limeniacha hoi kabisa .
Mama Kilango anaweza yote kuunga bajeti kusema kutajaa lakini hawezi kujaribu kujiondoa CCM.Hili hakuna wa kulipinga maana she just can't .
Swala la yeye kuunga bajeti mia kwa mia hilo nalo mie limeniacha hoi kabisa .
JMushi1 nadhani statistically kusema kuna mwamko tofauti kwa wananchi kwa kutumia kipimo cha mijadala ya JF sio sahihi. Kungekuwa na mwamko unaousema then CHADEMA walikuwa na kila sababu ya kushinda Kiteto kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika katikati ya kashfa kibao zinazohusu utendaji wa serikali. Nadhani wewe ndio unahitaji kufanya uchunguzi juu ya hali halisi.
Nashukuru kwa maoni yako lakini this time around there is an EXTREMELY DIFFERENT SITUATION HENCE DEFINING MOMENT IN THE HISTORY OF OUR COUNTRY AND MAYBE THE WORLD!
Kuna mwamko wa tofauti miongoni mwa wananchi mchungaji fanya uchunguzi utajua hilo!
Tumeshajua kuwa BUNGENI MASLAHI YA CHAMA YANAPEWA KIPAUMBELE KULIKO YALE YA TAIFA!
Mifano ni mingi tu kuanzia enzi za Mrema aliyejitoa ccm na Zitto aliyefukuzwa na hao ccm huko bungeni kwa kutetea maslahi ya Taifa.
Mama Killango tunataka tumpe A SHOT...Ila kwa masharti kwamba atoke huko ccm kwani kauli zake ni zile zile za Mwenyekiti wake na chama chao na vile vile hitimisho ni kikao chao cha siri ambcho walikubaliana kwa pamoja namna ya kuingia upya kwenye siasa na mbongo zetu kwa style ya kujisafisha na kauli tata za kisiasa!
Kwa vile ni wazi kuwa alishindwa kupingana na maslahi ya chama kwa kuipigia kura ya NDIYO bajeti ya kifisadi huku akifanya hivyo kwa kushirikiana na MAFIASADI HAO NI JAMBO LENYE KUSUMBUA AKILI PALE TUNAPOTAKA TUMWAMINI!
Ni ushauri wangu wa bure Mama Killango na ninaamini utakaposoma hii makala then utachukua uamuzi wa busara ili tuweze kukuunga mkono moja kwa moja.
Ni matumaini angu utafuata mfano wa MREMA ambaye ghafla walimfanya aonekane kichaa mara baada ya kugundua kuwa hawezi kulipigania TAIFA LAKE AKIWA NDANI YA ccm.
Ni hayo tu kwasasa...
Huu mwamko wa tofauti uko wapi? Umejiuliza ilikuwaje Chenge na Lowassa wakapokelewa kwa Shangwe kama Wafalme katika majimbo yao? Hivi unafikiri na hoja zote za kuwatuhumu Chenge, Lowassa, Mkulo, Karamagi, Msabaha leo kukifanyika uchaguzi mkuu wakakosa kura za kuwarudisha Bungeni?
Umeulizwa swali zuri sana, kuwa kama nyakati hizi ni za mwamko na mageuzi, ilikuwaje Upinzani ukapigwa ngwala Kiteto?
Be realistic my friend. Hizi kelele za kufoka "kamata mafisadi" zinanikumbusha wakati Lyatonga alipokaribia kuondoka CCM na hata alipoondoka.
Kama ulikuwa mdogo miaka 16 iliyopita, nitakupa kilichotokea na huyo Lyatonga ambacho kilifikia mahali kuanguka vibaya katika siasa za Tanzania.
Mrema alipojitoa CCM baada ya kuvuliwa Uwaziri, alianza kuhangaika kama malaya akitaka ukuu kwa kuwa alijiona kuwa ule umaarufu wake ndio ngao pekee.
Mind you this is typical political behaviour ya Wanasiasa Tanzania ambao wana umashuhuri kujiamini kuwa wao ni Alpha na Omega.
Alikwenda Chadema akamwambia Mtei ampishe Uenyekiti kama sharti la yeye Mrema kujiunga Upinzani. Mtei akamwambia, kwanza inabidi uwe mwanachama, pili itabidi upitie kila ngazi zinazotakiwa ukisubiri wakati Chadema ifanye mkutano mkuu ugombee uenyekiti, na kama ni kutaka kuwa mgombea wa Uraisi kwa Chadema, basi ni shurti upitie mchakato kama wengine. Mrema akalikataa hili, akaenda NCCR ambako wale wanausalama wenzake Mabere Marando, Lamwai na wengine ambao walikuwa ni viongozi, wakampa Uenyekiti harakaharaka ili NCCR kipate umaarufu.
Kilichofuata ni mtiririko wa vurugu ndani ya NCCR mpaka akafukuzwa akaenda TLP ambako nako bado hakujawa na salama.
Una lengo zuri kutaka mabadiliko yafanyike, lakini jifunze kuwa Historia inatuambia nini?
Kama unafikiri kujitoa CCM na kukimbilia Upinzani ni kazi rahisi, waulize wazee makini kama Cleopa Msuya, Salim Ahmed Salim, John Malecela na hata Edward Lowasa wa 1995, kwa nini walibakia CCM na hawakukimbilia huko unakosema ndiko kwenye njia pekee.
Unaposema CCM ni mafisadi, je una maana CCM nzima au sehemu ya CCM ina mafisadi? Maana kumbukumbu zangu zinaniambia kuwa CCM ni chama pekee chenye wanachama wengi kuliko vyama vyote vya upinzani vikijiunga. CCM imejijenga mijini na vijijini kiasi kuwa kila mtu anavuta pumzi inaitwa CCM.
Je unafikiri kuhama CCM ndio suluhisho pekee? Mwanasiasa makini wa CCM kamwe hawezi kufanya kosa la kujidhuru na kujitia kitanzi kama alivyofanya Mrema au Tambwe Hiza!
Tumeshajua kuwa BUNGENI MASLAHI YA CHAMA YANAPEWA KIPAUMBELE KULIKO YALE YA TAIFA!
Mifano ni mingi tu kuanzia enzi za Mrema aliyejitoa ccm na Zitto aliyefukuzwa na hao ccm huko bungeni kwa kutetea maslahi ya Taifa.
Mama Killango tunataka tumpe A SHOT...Ila kwa masharti kwamba atoke huko ccm kwani kauli zake ni zile zile za Mwenyekiti wake na chama chao na vile vile hitimisho ni kikao chao cha siri ambcho walikubaliana kwa pamoja namna ya kuingia upya kwenye siasa na mbongo zetu kwa style ya kujisafisha na kauli tata za kisiasa!
Kwa vile ni wazi kuwa alishindwa kupingana na maslahi ya chama kwa kuipigia kura ya NDIYO bajeti ya kifisadi huku akifanya hivyo kwa kushirikiana na MAFIASADI HAO NI JAMBO LENYE KUSUMBUA AKILI PALE TUNAPOTAKA TUMWAMINI!
Ni ushauri wangu wa bure Mama Killango na ninaamini utakaposoma hii makala then utachukua uamuzi wa busara ili tuweze kukuunga mkono moja kwa moja.
Ni matumaini angu utafuata mfano wa MREMA ambaye ghafla walimfanya aonekane kichaa mara baada ya kugundua kuwa hawezi kulipigania TAIFA LAKE AKIWA NDANI YA ccm.
Ni hayo tu kwasasa...
Hana sababu yoyote ya kutoka CCM, wakati mwngine ni rahisi kuleta mabadiliko ndani ya chama kama ukiendelea kuwemo ndani na siyo ukiwa nje. Akitoka atakuwa amewapa ushindi mkubwa mafisadi. Muasisi wa Chama Mwalimu Nyerere alikuwa anawachamba viongozi mbali mbali ndani ya CCM na sirikali na hakutoka CCM.
Mbona akina Mwinyi, Butiku, Warioba, Kawawa, Msuya na wengineo ambao wamewasemea hovyo mafisadi ndani ya chama na serikali hamuwaambii wajiengue ndani ya Chama? Kulikoni?
Mama Kilango huu ni mwanzo tu, endelea na juhudi zako za kupambana na mafisadi ndani ya chama na serikali, Watanzania wengi tuko nawe bega kwa bega katika hili. Uwe makini mno katika movement zako za kila siku na Mungu atakulinda.
JAY EFU PATAMU...OK atueleze atakavyobadilisa ccm wakati yeye na mwenyekiti wake wanaamini haina mafisadi!
Mpe muda!!!!
Kwa uelewa wetu..Ameshakubaliana na mwenyekiti wake na MAFISADI kwa kupiga kura ya ndiyo kwenye bajeti yao ya KIFISADI PAMOJA NA KUKUBALI KAULI ZA M/KITI KUWA CHAM NI SWAFI...SASA HAPO KUNA HAJA GANI YA KUINGIA KWENYE KICHWA CHA MTU...EVERYTHING NI WAZI NDUGU!
Hayo ni mawazo yako lakini kwa maoni yangu bado ana nafasi kubwa ya kupambana na ufisadi, hii si vita ya siku moja eti katika bunge lenye wabunge zaidi ya 250 wa CCM Anna Kilango akipiga kura ya kutosupport bajeti basi ndiyo atakuwa ameshinda katika vita hivyo.
Lazima awe na strategy kali na siyo kukurupuka tu!!! Sasa kama angepiga kura ya hapana na bajeti bado ingepita angekuwa hajafanya lolote katika vita dhidi ya mafisadi bali angekuwa amevuruga mikakati na si ajabu baadhi yetu tungemkejeli sasa hiyo kura yako ya hapana ndiyo imesaidia nini katika kupambana na ufisadi? Mambo hayaendi pupa kaka...mpe mama muda kabla hujaanza kumzodoa!!!
KIKAO CHA SIRI CHA ccm ALICHOSHIRIKI YEYE NA KINA MKAPA NA CHENGE NA KWENDA KUMALIZIA KWA KUJIPONGEZA NA KURA YA NDIYO YA KIFISADI HUKO BUNGENI NDIO MWANZO WA UMAARUFU WAKE HUU WA MOTO WA KIFUU KAMA AKIBAKI ccm TRUST ME ON THIS...THE RESOLVE IS CERTAINLY AT THE HIGHEST LEVEL EVER!
Haya mambo hukurupuki tu bila kuwa na mikakati na kuangalia na wale unaopambana nao wana mikakati gani, vinginevyo zitakuwa ni mbio za sakafuni....
Hebu tueleze kama angepiga kura ya hapana na bajeti bado ingepita angekuwa amefanikisha lipi katika vita dhidi ya mafisadi?
Waulize wale ambao at least wali abstain!
Kwanini hakujiunga nao?
Niliazisha thread na kuwapa ushauri kuwa wasishirikiane na Mafisadi kuamua mustakabali wa nchi wakati hao watu walitakiwa kuwa rokapu aroo!
Tumia akili BUBU.