Mama Kilango jiandae mwisho wako ni 2015

Acheni majungu hata sisi tusiokuwa wa jimbo lake tunajua anachokifanya.......Barabara za Same Mashariki zinapitika mwaka mzima tangu mama huyu amekuwa Mbunge. Vipi barabara za kwenda milimani kama Ndungu-Lugulu uliitengeneza wewe?? Kiwanda cha Tangawizi ulihusika?? Mafisadi Bungeni ulishawahi kuwanyoshea hata kidole?? ........ Hao waliokutuma ulete ***** wako hapa waambie watafute njia nyingine.

Mafisadi kwa sasa wanapambana rais abakiziwe mamlaka makubwa ktk mswada wa mabadiliko ya katiba ili wazidi kunyonya kodi za watanzania, ulimsikia Kilango alichosema kuhusiana na mswada huu wa katiba????
Mpinga mafisadi kawa wakili wa mafisadi.
Kilango kajichoresha kuhusu mswada wa katiba na round hii tunafanya vikao na kila kaya same kuanika uovu wa mama huyu mzugaji mkubwa.
 
huyu mama kigeu geu sana niliona alivyo mtetea ngereja baada ya kamati teule ya bunge ya juzi ndo nikajua ni mtu wa ovyo
Hiyo ndiyo hali halisi ya wanasiasa wetu, wakinunuliwa chai wanakuwa watetezi wa wanaorudisha nyuma maendeleo yetu. Kwa anavyoongea huyu mama utafikili kweli patachimbika lakini baadaye anatetea hao hao aliyosema patachimbika. NAUNGA MKONO KWAMBA NI KIGEUGEU
 
Mh. Anna Kilango ndiye anayekusanya kodi toka kwa wananchi wa Tanzania? Maendeleo yanaletwa kwa kutumia pesa za kodi........labda nyie hamlipi ndio maana hizo barabara hazijengwi au unadhani wanaokusanya kodi wanapeleka pesa mahali bila kuangalia mchango wa hilo eneo katika uchumi wa Taifa? Unafikiria mtavuna tangawizi kiasi gani iweze kutoa kodi ya TShs 900 million gharama ya kujenga kilometa moja ya lami?iwe mwepesi kulaumu bajeti hupangwa na serikali na siyo mbunge.


black acha hizo bana......... mgawo wa pesa za kodi kwa maendeleo ya wananchi
humea jinsi mwakilishi wa wananchi alivyo karibu na mkulu.umesahau jinsi mramba wakati ule akiwa karibu sana na ben pesa zote za bara bara zilipelekwa rombo bila kujali kelele za wabunge wengine ambao majimbo yao hayakuwa hata na meta moja ya lami. huyo mama hafai kuwa mama wewe hujui kuwa mama mkorofi na wanaye hula kwa macho tuu. kalagabahoo.
 
Huyu mama hamna kitu kabisa wale aliokuwa anawalipua ilikuwa ni chuki binafsi kwa ajili ya mmewe.Vinginginevyo si kweli kwamba huyu ni mpambanaji,hata ili suala la kumtetea Ngereja ulikuwa ni ujinga mtupu

Huyu mama kweli ni kigeugeu mara leo ni mpambanaji wa mafisadi lakini kesho anawatetea mafisadi vijana wakina Ngeleja; tatizo lake kubwa ni kwamba she has never been consistent in her entire life history!!
 
huyu mama kigeu geu sana niliona alivyo mtetea ngereja baada ya kamati teule ya bunge ya juzi ndo nikajua ni mtu wa ovyo

huyu mama bure kabisa ..yaani siku ya mjadala wa katiba ndo nilipomuona sifuri anajikamua kamua tu bila hata kuwa na cha maana anachoongea
 
Acha uongo hakuna walichofanya wakati kuna mpango jimbo la mamam huyu kusaidiwa na IRAN wachimbe mafuta au hufahamu mahusiano mazuri ya familia ya mama huyu na IRAN?

irani muda si mrefu itakwenda kuzim ajitahidi atafute friend family mwingine ili aweze kutimiza malengo yake.
 
haya yaliyokwisha kuandikwa humu yangekuwa yanafanyiwa kazi tz ingekuwa mahala furani lakini sasa zimebakia kuwa porojo.
 
Acheni majungu hata sisi tusiokuwa wa jimbo lake tunajua anachokifanya.......Barabara za Same Mashariki zinapitika mwaka mzima tangu mama huyu amekuwa Mbunge. Vipi barabara za kwenda milimani kama Ndungu-Lugulu uliitengeneza wewe?? Kiwanda cha Tangawizi ulihusika?? Mafisadi Bungeni ulishawahi kuwanyoshea hata kidole?? ........ Hao waliokutuma ulete upupu wako hapa waambie watafute njia nyingine.

wewe jamaa unashangaza kweli kweli ..ile barabara ya ndugu lugulu ndio unayoona imetengenezwa? mvua ikinyesha utapita pale?....kiwanda cha tangawizi cha pale miamba unajua hali yake kwa sasa hivi?..barabara ya kwenda miamba unajua ilivyo?? huyu mama hafai kabisa maneno mengi sana bila vitendo kiwanda cha tangawizi alikuja UDSM akachangisha watu pesa pale ..kiwanda kimeisha?
 
Back
Top Bottom