Omusolopogasi
JF-Expert Member
- Aug 31, 2017
- 7,101
- 18,084
Mnaharibu uzi mzuri kwa kuweka mambo ya hospitali...
Ujumbe murua. Unajitosheleza bila hizo picha. Hizo picha zinadhalilisha na kuharibu uzi huu mzuri. Hongereni mama zetu. Mi ni mhenga. Niko mbali na mama. Mama ni mhenga zaidi. Juzi nimepigia simu mama ananiuliza kama nakula nashiba. Ana wasiwasi kuwa naweza kuwa nimekonda sana! Kweli mama hastaafu.
Hospitali ipo wapi hapo?Mnaharibu uzi mzuri kwa kuweka mambo ya hospitali...
Sana..Umefurahiiii mwenyewe[emoji4][emoji4]
Yaani kumbe sometimes kuzaa si kupata kama unazaa mitoto sampuli hii inayokupenda kwa maneno kuliko vitendoWewe ndo utaki asitaafu. Kama amefikia umri wote uwo nawewe unamwacha afanye kazi zote wakati wewe ni mwanae mkubwa ilibidi umsaidie hizo kazi mwenyewe.
Inaonesha una stress sanaHuwezi kumsifia polisi kukamata mwizi maana ni majukumu yake
Hivi huyo mtoto hawezi ku-drown?!
poa mkuu ujumbe mzuri sana huuBaba yangu amestaafu akiwa na miaka 60.
Mama yangu pia ni mstaafu kazini, lakini kila napoona shughuli za Mama na Baba najifunza kitu kuwa hakuna mwanamke ambaye huwa anastaafu.
Huamka asubuhi na kumuandalia(Mumewe) Baba yangu chai ili hali naye ni mzee sana.
Mara amuandaliapo huingia katika maandalizi ya chakula cha mchana.
Huenda sokoni kutafuta mboga kwa ajili ya kupika, hata mara kadhaa amekuwa akitembea umbali mrefu kwenda bustanini kwetu kuchuma mboga na matunda.
Anapika kwa ajili ya wanae, ahakikishe wamekula chakula, tena huwauliza endapo wameshiba au apike chakula kingine.
Hata wageni wanapokuja nyumbani nyakati za usiku, Baba husema mimi naingia chumbani kulala atawaandalia Mama chakula mtalala “Usisahau kuwaonyesha sehemu ya kulala”
Mama huwaandaa wajukuu zake kwa ajili ya kwenda shule sambamba na kuhakikisha wamekunywa uji kabla ya kuondoka.
Anamjali na kumhudumia kila mwenye uhitaji ajaye nyumbani kwetu.
Hutembea umbali mrefu kwa ajili ya kutafuta kuni, kwa ajili ya kumpikia mumewe na familia nzima inayomzunguka.
Mama mara nyingi.huwa wa.mwisho kulala akihakikisha milango yote imefungwa na watoto wamelala ndani ya neti
Ni mama pekee hajawahi kustaafu.
Umejifunza nini kingine kwa mama?
Wafariji akina Mama kwa kushare ujumbe huu
C&PView attachment 1227943View attachment 1227944View attachment 1227945