Mama aua mwanawe Dar kwa kumpiga usiku kucha

Majirani nao hazimo si wangeita polisi kwa msaada zaidi. R.I.P mtoto
Sio majirani Dar es salaam nzima watu wako hibo sjui watu wamekumbwa na tatizo gani unaweza kutwa na tatizo hapo watu wakakuungalia km mzimu
 
Hivi hao Majirani wapo Humu Jamani maana Yake naona Shutuma za Majirani Majirani Majirani Majirani Majirani Majirani Nyuma ya Key Board???

Hii ndiyo Madhara ya Single Mother, Mtakuja Kubisha lakini haya Ndiyo Madhara? Pia Huo ndiyo Ukweli Kuwa Mwanamke anapenda Pesa kuliko Ubinadamu. Huyo Ni Mwanae ambaye amemtoa Roho kwa Kumhisi kuwa kamuibia Hela , Je wewe Mtu wa Kambo? Si Lazima akamtafute Mshana Jr ili amuelekeze kwa Mganga amtoe Roho Kabisa...

Hiyo ndiyo Sura halisi ya Mwanamke akiwa amekasirika...

Kingine, ni nani siku hizi anaweza kuzuiwa kumuadhibu Mtoto wake wa Kumzaa? Tusemee Ukweli tuache kuongea kwa Kujivika Nyuma ya Screen zetu. Let us be honest,

NI NANI KATI YENU ANAWEZA AMBIWA NA MTU BAKI ACHA KUMCHAPA MTOTO NA AKAKUBALI? NI NANI KATI YENU ANAWEZA MCHAPA MTOTO AMBAYE SIYO WAKE HALAFU FAMILIA YA MTOTO IKAWA NA AMANI? NI NANI?

LET US OPEN OUR MOUTH KWA VITU AMBAVYO TUNAVIISHI.

SINGLE MOTHER SIYO WALEZI WAZURI UKWELI NI HUO.....
 
ndo matokeo ya kukosa hekima na busara hayo...akaona kumsulubu huyp mtoto ndo uamuzi sahihi.pamoja na umpiga sana mbona hakusema pesa ziko wapi? this means he was innocent na hajaiba..kama angekuwa kaiba kwa hicho kipigo angesema tu.
na pia huyu mama alishindwa kuwashika hawa wakubwa sababu wana nguvu na akaamua kumsulubu huyo mdogo sababu anamhimili.
hiyo familia nzima imeua..washtakiwe wote sio huyo mama tu.

mungu amrehemu huyo kijana na amsamehe dhambi zake!
 
Hao majirani wana matatizo. Wanamuona mtu anapigwa kipigo cha mwizi wanamuacha ampige mpk kufa?

Mkuu hapa ndipo ninapotamani maisha ya wenzetu wazungu huko.. Maana ingekuwa huko, majirani wangepiga simu police na ndani ya dakika 3 Police wangefika hapo na kumkamata huyo mama.. Hapa kwanza mpaka kupokelewa kwa hiyo simu ni kazi..

Rest in Peace mtoto..
 
Mmh kama ni hivyo wana roho ngumu kweli
Sio majirani Dar es salaam nzima watu wako hibo sjui watu wamekumbwa na tatizo gani unaweza kutwa na tatizo hapo watu wakakuungalia km mzimu
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watu wengine wawili wanashikiliwa na Jeshi hilo pia.

Joshua Benjamin (14) ambaye alikuwa akisoma darasa la Saba katika Shule ya Msingi Ukonga, anadaiwa kupigwa usiku kucha na mama yake huyo ambaye baadaye alimfunga kwa kamba kwenye mti, nje ya nyumba yake, hadi saa 11 alfajiri alipogundulika kuwa ameshakufa.

Tukio hilo, mashuhuda walisema jana, lilisababisha taharuki kubwa mtaani hapo kwani baadhi ya wakazi walitaka kumpiga mama huyo kabla ya polisi kufika na kumuokoa.

Mmoja wa majirani wa mama huyo ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini, aliiambia Nipashe kuwa walianza kusikia kelele za mtoto huyo akiomba msaada tagu usiku huku mama huyo akiendelea kumpiga.

"Tulisogea hadi jirani na dirishani kwake," alisema shuhuda huyo na "tukamkataza."

"Tulimwambia adhabu hiyo inatosha kwa mtoto maana hadi mtoto aliishiwa nguvu, (hakutusikiliza) tukaondoka na kumuacha akimpiga tu.

Mtoto huyo amefariki ikiwa ni miaka miwili tangu kifo cha baba yake, jirani huyo alisema zaidi.

"Mume wa huyu mama tumemzika mwaka juzi, tuliumia majirani tukawaza pengine baba yake angekuwepo angemsaidia kumuokoa kijana yule.

MTOTO MWINGINE
Jirani mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Subira alisema chanzo cha kipigo ni madai ya mama huyo kuibiwa Sh. milioni 1 na mwanawe huyo.

"Cha ajabu ni kwamba ana mtoto mwingine mkubwa, na mle ndani kuna ndugu zake wengine sasa kwa nini asiwafikirie hao?" Alisema Subira.
"Alimpiga vibaya mno, yaani alimpiga utafikiri anapiga kibaka.

"Watu wengi tumeshuhudiia akimpiga na yeye ameokolewa na polisi la sivyo watu wangemmaliza."

Shuhuda mmoja aliliambia gazeti hili kuwa mwanamke huyo ana watoto wanne akiwamo marehemu ambaye ni wa tatu kuzaliwa. Wa kwanza amemaliza kidato cha nne, wa pili kidato cha pili na wa nne anasoma shule ya awali.

Alisema pia kwenye familia hiyo kuna mtoto wa kufikia wa mama huyo, wa marehemu mume wake.

Imeelezwa kuwa mtoto huyo alifariki saa 4 asubuhi baada ya mwanamke huyo kuona mtoto wake haamki, aliamua kupiga simu kwa watu wake wa karibu kuomba msaada.

Kamanda Hamduni aliiambia Nipashe jana kuwa watu wawili akiwamo mwanamke huyo wanashikiliwa na polisi tangu juzi.

"Ni kweli tukio hilo limetokea huko Kinyerezi na tunawashikilia vijana wawili pamoja na mwanamke huyo kwa ajili ya upelelezi," alisema.

Chanzo: Nipashe
Majirani nao wamehusika na hicho kifo...
 
Me Nikiingia Madarakani, Ntakua Zaid Ya Magufuli. Majirani Na Mjumbe Wacngebaki Salama Kwangu. Km Majirani Waliona Kpgo Knatosha Walirudije Kulala Wkt Mtoto Bdo Anapgwa? Hv Na Hao Police Waliokua Wanamhoj Huyo Jrani Cjui Vp! Majran Wote Ni Wauwaj Hpo Walipaswa Kwenda Na Karandnga Wanawasomba. Hii Nchi Imeoza Sn, Magu Anapaswa Kuyaangalia Na Haya Ya Mtaani Kwakwel.
 
Mkuu hapa ndipo ninapotamani maisha ya wenzetu wazungu huko.. Maana ingekuwa huko, majirani wangepiga simu police na ndani ya dakika 3 Police wangefika hapo na kumkamata huyo mama.. Hapa kwanza mpaka kupokelewa kwa hiyo simu ni kazi..

Rest in Peace mtoto..
Wangezunguka nyumba wakapiga mayowe ingesaidia pia
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamduni amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba watu wengine wawili wanashikiliwa na Jeshi hilo pia.

Joshua Benjamin (14) ambaye alikuwa akisoma darasa la Saba katika Shule ya Msingi Ukonga, anadaiwa kupigwa usiku kucha na mama yake huyo ambaye baadaye alimfunga kwa kamba kwenye mti, nje ya nyumba yake, hadi saa 11 alfajiri alipogundulika kuwa ameshakufa.

Tukio hilo, mashuhuda walisema jana, lilisababisha taharuki kubwa mtaani hapo kwani baadhi ya wakazi walitaka kumpiga mama huyo kabla ya polisi kufika na kumuokoa.

Mmoja wa majirani wa mama huyo ambaye aliomba jina lake lisiandikwe gazetini, aliiambia Nipashe kuwa walianza kusikia kelele za mtoto huyo akiomba msaada tagu usiku huku mama huyo akiendelea kumpiga.

"Tulisogea hadi jirani na dirishani kwake," alisema shuhuda huyo na "tukamkataza."

"Tulimwambia adhabu hiyo inatosha kwa mtoto maana hadi mtoto aliishiwa nguvu, (hakutusikiliza) tukaondoka na kumuacha akimpiga tu.

Mtoto huyo amefariki ikiwa ni miaka miwili tangu kifo cha baba yake, jirani huyo alisema zaidi.

"Mume wa huyu mama tumemzika mwaka juzi, tuliumia majirani tukawaza pengine baba yake angekuwepo angemsaidia kumuokoa kijana yule.

MTOTO MWINGINE
Jirani mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Subira alisema chanzo cha kipigo ni madai ya mama huyo kuibiwa Sh. milioni 1 na mwanawe huyo.

"Cha ajabu ni kwamba ana mtoto mwingine mkubwa, na mle ndani kuna ndugu zake wengine sasa kwa nini asiwafikirie hao?" Alisema Subira.
"Alimpiga vibaya mno, yaani alimpiga utafikiri anapiga kibaka.

"Watu wengi tumeshuhudiia akimpiga na yeye ameokolewa na polisi la sivyo watu wangemmaliza."

Shuhuda mmoja aliliambia gazeti hili kuwa mwanamke huyo ana watoto wanne akiwamo marehemu ambaye ni wa tatu kuzaliwa. Wa kwanza amemaliza kidato cha nne, wa pili kidato cha pili na wa nne anasoma shule ya awali.

Alisema pia kwenye familia hiyo kuna mtoto wa kufikia wa mama huyo, wa marehemu mume wake.

Imeelezwa kuwa mtoto huyo alifariki saa 4 asubuhi baada ya mwanamke huyo kuona mtoto wake haamki, aliamua kupiga simu kwa watu wake wa karibu kuomba msaada.

Kamanda Hamduni aliiambia Nipashe jana kuwa watu wawili akiwamo mwanamke huyo wanashikiliwa na polisi tangu juzi.

"Ni kweli tukio hilo limetokea huko Kinyerezi na tunawashikilia vijana wawili pamoja na mwanamke huyo kwa ajili ya upelelezi," alisema.

Chanzo: Nipashe
Kama ndio ivi basi kweli hali ya upatikanaji wa pesa ni mgumu.
 
eti tukaondoka. ..hao majirani jinga kabisa hapo hata mlango unabomolewa anapewa kipondo huyo mama wakati akiburutwa polisi mtoto anaokolewa
 
Hao majirani ni watu wa ajabu sana,mtu amempiga mtoto mpaka kaishiwa nguvu,bado mnamwacha aendelee kumpiga tu.Wangemuokoa mtoto na kumpeleka Polisi,halafu hospital.INASIKITISHA sana.HUYU MAMA NI GAIDI.
 
Majiran wa dar hawana maana kabisa yaan mtoto anapigwa kias hicho afu nyie mnaishia kuchungulia dirishan na kusepa aibuu sana kwa watu wa dar
 
[emoji26][emoji26][emoji26][emoji26]
Na ukute mtoto kasingiziwa jamani!
Huyo mama asiachiliwe hivihivi kabisa!!! Ata kama mtoto aliiba, sio kumuadhibu hivyo....

Kama mtoto hakuiba, huyo mwizi wa kweli humo ndani roho itamsuta milele kwa kusababisha kifo cha mwenzake.
 
Back
Top Bottom