Mama aua bintiwe kwa kupata mimba

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054
Mama aua bintiwe kwa kupata mimba
Written by Administrator
Wednesday, 15 July 2009 15:05
Na Stella Shoo

MKAZI wa Kijiji cha Kilemfua Mokala wilayani Rombo, Kilimanjaro anayefahamika kwa jina la mama Kubwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi Wilayani Rombo kwa tuhuma za kumuua bintiwe kwa kuwa na ujauzito.

Akizungumza na gazeti hili jana asubuhi kwa njia ya simu, Diwani wa Kata ya Kemfua Mokala, Bw. Festo Kilawe alisema tukio hilo lilitokea Jumamosi saa 3:00 usiku.

Bw. Kilawe alimtaja marehemu kuwa ni Bi. Lilian Mrema ambapo
alisadikiwa kuwa na ujauzito wa karibu miezi 6 na kuwa mama mzazi wa Bi. Liliani alikuwa hataki ujauzito wa mawanae huyo.

"Ndugu mwandishi huyu mama alikuwa na ugomvi wa mara kwa mara na marehemu huyu baada ya kuona kuwa ana ujauzito,sasa ilipofika usiku huo wa Jumamosi alimfuata marehemu chumbani kwake na kuanza kumshambulia kwa mwiko hapo marehemu alipiga kelele majirani walipofika alikuwa ameumia vibaya,sasa wakati anapelekwa hospitali ndipo alipofariki, " alisema Bw. Kilawe.

Alisema baada ya kutokea kwa tukio hili ndio majirani walipotoa
taarifa katika Kituo cha Polisi cha Rombo na mtuhumiwa alikamatwa na kutiwa mbaroni kwa tuhuma za mauaji.

"Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Huruma na mtuhumiwa amekamatwa na Polisi na sasa yupo chini ya ulinzi na kuwa upelelezi unaendelea utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu shitaka la mauaji"alifafanua Bw. Kilawe
 
Huyo mama afungwe tu angezaaje huyo mtoto bila kufanya mapenzi na kupata mimba?
 
Huyo mama afungwe tu angezaaje huyo mtoto bila kufanya mapenzi na kupata mimba?

Labda mama huyo alimzaa mtoto wake kwa kufanya mapenzi na kupata mimba ya kihalali (kwa ndoa), lakini mtoto wake kapata mimba kiharamu bila ya ndoa.

lakini hata mimi simsapoti kumuuwa mtoto wake huyo, yeye angemcharaza viboko tu bila ya kumuuwa, kwa kweli mama huyu amekusea
 
Labda mama huyo alimzaa mtoto wake kwa kufanya mapenzi na kupata mimba ya kihalali (kwa ndoa), lakini mtoto wake kapata mimba kiharamu bila ya ndoa.

lakini hata mimi simsapoti kumuuwa mtoto wake huyo, yeye angemcharaza viboko tu bila ya kumuuwa, kwa kweli mama huyu amekusea
Ndugu kitanda hakizai haramu.Huyo mama ni katili sana na lazima aadhibiwe kwa kifungo cha maisha kwa kuua kwa kukusudia.
 
Jela tu ndio inamfaa huyo mwanamke,na kifungo cha maisha ndo adhabu yake kuu...Naomba Mahakama imjutishe vile inavyotakiwa,atauwaje mwanae wa kumzaa mwenyewe?!Kama kuna adhabu nyingine kali aongezewe ili ajutie lile alilolifanya huyo gaidi.
 
Kwa kweli inauma sana mtoto wako awe wa kike au wa kiume kuzaa mtoto/watoto kabla ya kuwa na formal marriage, na inauma na kuharibu zaidi pale ambapo anakuwa na several kids with several men/women!!!! Hata hivyo, makosa haya siyo justification ya kumuua mtoto!!! hapo ameua watu wawili, mtoto na mjukuuu!!! Jamani ukiwa na hasira sana usifanya jambo la hamaki,, utakuja juta baada ya kitendo!!! Imagine huyu mama atakavyoishi maisha ya kilio cha moyo kwa maisha yake yote na pia mtizamo wake kwa jamii kama ataachiwa huru!!!! Hii ni social problem ambayo inaweza pia msababishia suicide!!!!!
 
Mama inabidi kutumia hekima..maana hata Obama mama yake alipata mimba akiwa 18!

Hakuna mtu Mkamilifu!
 
"Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Huruma na mtuhumiwa amekamatwa na Polisi na sasa yupo chini ya ulinzi na kuwa upelelezi unaendelea utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu shitaka la mauaji"

sidhani kama kesi kama hii inahitaji upelelezi, mtu amekamatwa anapiga na kusababisha kifo lakini polisi wa bongo utakuta upelelzi miaka sita
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom