Wasalam wanajamii forum, Mimi ni mwanaume rijali ninayeishi na mama nyumbani. Nina tabia ya kurudia nguo hata siku SITA BIla kubadilisha na nikibadilisha naendelea hivyo hivyo huku nikirundika manguo yawe mengi Ili nije niyafue Kwa pamoja. Mama anapenda Sana kuingia chumbani kwangu na mara nyingi panakuwa sio pasafi.Basi atanidekia choo na kusafisha chumba changu na kutandika kitanda lakini kinachoniuma kwanini ang'ang'anie kunifulia Mimi ni mtu mzima. Kuna muda Hadi tunagombana nakasirika na kulia kabisa.Sijui hata nifanyeje anielewe.