mama amwaga radhi kwa manae kisa ukahaba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mama amwaga radhi kwa manae kisa ukahaba

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Jul 25, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,654
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Mama achoshwa ! atoa radhi hadharani[/TD]
  [/TR]
  [TR="bgcolor: #e1e1e1"]
  [TD]
  [​IMG]
  [/TD]
  [TD]Monday, June 20, 2011 4:22 PM
  KATIKA hali ambayo iliwaacha watu wengi wakiwa hawaamini macho yao mwanamke mmoja [51] amejikuta akisaula nguo zake zote na kutoa radhi hadharani kwa mwanae wa kike aliyefahamika kwa jina moja la Feti[22] kwa kile kilichodaiwa kuchoshwa na tabia zake[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"]Tukio hilo la aina yake lilitokea jana majira ya jioni huko maeneo ya Buguruni Mnyamani ambapo imedaiwa mama huyo alichoshwa na vitendo vinavyofanywa na mwanae huyo ambavyo vilikuwa havimridhishi.

  Mashuhuda wa tukio hilo walidai kuwa, mama huyo jana majira ya jioni aliamua kumtolea uvivu mwanae huyo kwa kusaula viwalo alivyokuwa amevaa akiwa na lengo la kumtolea radhi.

  Awali imedaiwa kuwa Feti alikuwa na tabia za kumdhihaki Mungu kwa kufanya matendo maovu yanayodaiwa yanaenda sambamba na ukahaba ambapo mama huyo imedaiwa alikuwa akimpigia kelele kila kukicha mwanae huyo ambaye alikuwa hataki kufuata yale anayoambiwa.

  Pia imedaiwa kuwa Feti amekuwa na tabia za kugombana na wake za watu ikiwa ni pamoja na kufumaniwa na waume za watu mara kwa mara katika mtaa anaoishi hali iliyopelekea kuidhalilisha familia yake.

  Hata hivyo kutokana na vitendo na tabia chafu za Fet, mama huyo alijitoa kimasomaso kumlaani mwanae huyo jana wakati binti yake huyo alipokuwa katika matayarisho ya kutoka safari zake za usiku.

  Ilidaiwa na shuhuda wa tukio hilo kuwa mama huyo alianza hivi” Yaani ukitoka tu hapa ndani kwenda katika biashara zako za kishenzi naomba ugongwe na gari ufe papohapo” hata hivyo imediwa kuwa Fet hakutishika na kauli hizo na alitoka kinguvu na mama huyo alianza kulia kwa uchungu na kuanza kusaula viwalo alivyokuwa amevaa huku akishikwa na baadhi ya majirani zake waliomsihi kuacha kufanya hivyo huku Feti akitimua mbio na kutokomea kusikojulikana.

  Hata hivyo imedaiwa kuwa msichana huyo alikwenda kuomba hifadhi nyumba ya jirani kutokana na aibu aliyoipata kutoka kwa mama yake huyo.[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="colspan: 3"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. pumbatupu

  pumbatupu JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 258
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Umalaya mbaya kumbe...
   
Loading...