Mama amuua 'House Girl' kwa kipigo, amfungia chumbani

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina la Mkami Shirima(33) mkazi wa Ilikiurei, nje kidogo ya jiji la Arusha, anadaiwa kumuua mfanyakazi wake wa ndani, Salome Zacharia (17) kwa kumpiga fimbo akimtuhumu kuiba Sh elfu 50.

Mwanamke huyo ambaye anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa, anadaiwa kutenda tukio hilo siku ya Alhamisi wiki iliyopita na baadaye alimfungia katika chumba kimoja wapo katika nyumba yake kwa muda wa siku mbili bila kumpatia chakula wala maji ya kunywa huku akiendelea kumchapa.

Akielezea tukio hilo mtoto wa mtuhumiwa huyo aitwaye, Sonia Bakari (17) amasema siku ya Alhamisi mama yake alikuwa anatafuta kisanduku cha kuhifadhia fedha (Kibubu) kilichokuwa na kiasi cha shilingi milioni 1.

Amesema kuwa mara baada ya kukikosa kisanduku hicho katika chumba chake alimuuliza marehemu pamoja na mtoto wake (Sonia) iwapo kama wamekichukua hata hivyo wawili hao walikana kukiona ndipo mama huyo alipoanza kumpiga marehemu.

Hata hivyo Sonia alimwambia mama yake kwamba aache kumchapa marehemu kwa kuwa yeye ndie aliyekichukua kisanduku hicho na kukivunja na kutoa shingi laki moja na kumpatia sh. elfu 50 marehemu ili amtumie mama yake aliyeko kijijini Singida.

Sonia anadai kwamba licha ya kumweleza mama yake asiendelee kumwadhibu marehemu bado aliendelea kumchapa mfululizo huku damu zikimchuruzika na kisha kumfungia katika chumba kimoja wapo bila kumpatia huduma yoyote ya chakula.

"Nilimwambia mama asimpige Salome kwa kuwa Mimi ndie niliyekichukua hicho kisanduku na kukificha chumbani kwetu nilikivunja na kuchukua sh. laki moja na kubakiza sh. laki tisa na nilimpatia elfu 50 Salome ili amtumie mama yake na Mimi nikabaki na Elfu 50" Amesema Sonia.

Amesema kuwa siku ya Jumamosi wifi yake (jina limehifadhiwa) alimweleza mama huyo kwamba marehemu alikuwa akitapika damu ndipo mama huyo aliamua kumpeleka katika hospital ya mkoa ya Mount Meru na marehemu alifikwa na mauti siku iliyofuata Jumapili.

Kamanda wa polisi mkoani Arusha Jonathani Shanna amethibitisha tukio hilo na kueleza kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospital ya mkoa Mount Meru ukisubiri uchunguzi wa daktari.

Mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu shtaka la mauaji linalomkabili.

Ends..



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Oh hell no.

Didn’t she fight back?

Sijui kwa nini mambo kama haya huwatokea watu wasioweza kupigana!!

I’m thankful to the way I grew up.

We resolved beefs by shooting the fair one.

You hit me, I hit you right back to knock you the fcuk out.

Your chin is my target. And I never miss.
 
Pole sana Shirima the boss lady. Uchumi mgumu mpaka 50k tunaiona like 500k. sema ndio hivyo, hasira mwenzake hasara.

Ma haus girl ni moja ya vitu ambavyo tulishakataa vituumize kichwa home. Acha tubadil tu hata 10 kwa miezi mi3 (maana hapa ndio majirani huwa wanaongea kweli kuwa huyu hawez ishi na watu). Nikishakusoma tu umeanza kuwa hueleweki sichukui hata sekunde ku risk maisha ya watoto na family well being kwa ujumla kisa house girl.

Mabosi hasa wanawake wana ukorofi sana kwa mabinti lakini hawa mabinti pia wengi wao ni pasua kichwa mno

Jana tu hapo tar 09 march 020 napigiwa simu na ya home nikiwa njiani toka job kuwa binti haonekani home toka saa tisa alasiri kaenda kusuka. Mpaka saa 3 hajarudi. Ghafla inapigwa simu na jirani yetu wa mbali kidogo ana wafanyakazi vijana kumbe house girl wetu kaenda kudinywa huko na imagine hajamaliza hata week 3 toka afike home.

Niliporudi home sikuchelewesha. Mahojiano mawili matatu friendly kabisaaaaa halafu baada ya hapo SHE GOT FIRED..

Na huwa nahakikisha mtoto wa watu naishi nae vizuri na nampa mahitaji yote. Sipigi mfanyakazi mimi. Ila ukizingua siwezi kukuchelewesha unaondoka tu

NB
simple like that.
Tusije uana bure kwa mihasira
 
Oh hell no.

Didn’t she fight back?

Sijui kwa nini mambo kama haya huwatokea watu wasioweza kupigana!!

I’m thankful to the way I grew up.

We resolved beefs by shooting the fair one.

You hit me, I hit you right back to knock you the fcuk out.

Your chin is my target. And I never miss.
Kwanini mkuu amewaza kama mimi eti.

Walai mimi kuna scenario zinaweza nifanya nikauwa mtu kirahisi tu especially uyi mama ndio anaifanyie Mimi hivyo Haaa i'cant imagine.

Kwanza nawaza unufungie ndani nahisi utakuwa huutaki mlango wako iyo mishinso utayosikia sekunde tu utatafuta fundi mlango.

Portfolio | 2020
 
Maskini binti wa watu alikuja kufanya kazi asizo stahili kwa umri wake ila amelazimika tu kutokana na hali halisi. Anakuja kuuliwa na mtu mwenye umri mkubwa tu, mwanamke mwenzake, ambaye angepaswa amchukulie kama mdogo wake, ila amempiga, kumfungia chumbani na kuendelea kumpiga. Hii ni roho mbaya na ukatili, kisa elfu hamsini tu? Kina mama acheni kuwachukua hawa watu, mara nyingi wakina mama ndani ya nyumba wanakuwa wajeuri sana kwa hawa wasaidizi. Baba akiingilia yanazuka maneno. Mtu kuja kukufanyia kazi sio kuwa awe mtumwa wako. Fikiria ukifariki mtoto wako akija kupitia madhila kama hayo, wengi hawa ni mayatima na watu wa mazingira magumu wanaotafuta kujikwamua. Wanawake acheni ukatili, tunawasemaga waarabu hili leo limetokea kwetu. Chuki ni mzigo.
 
Back
Top Bottom