Mama alinyanyaswa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama alinyanyaswa.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ziltan, Oct 7, 2011.

 1. Ziltan

  Ziltan JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2011
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,347
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Habari wana jf,
  kwanza nna majonzi kwani yapata wiki tatu sasa tangu tumuage mama yetu mzazi,
  ila jambo linalonifanya niendelee kukosa furaha ni kwamba mama alinyanyaswa na shemeji (mke wa kaka tumbo moja) kwa kumtolea maneno makali na kwa kumnyima chakula kaka akiwa hayupo,
  ni hivi kaka na mkewe(shemeji yangu) wote ni waajiriwa serikalini ila wapo wilaya tofauti ndani ya mkoa mmoja, shemeji ndio anaishi walipojenga na ndipo mama alienda kukaa kwa ajili ya matibabu,
  kutokana na umbali kaka huwa anakaa kituoni kwake na kurudi nyumbani siku ya ijumaa jioni na kuondoka jumapili jioni hivyo wakati kaka hayupo, shemeji alimfanyia mama huo unyanyasaji,
  mchezo wake aliupanga hivi, akiwepo kaka ataonesha upendo wa hali ya juu kwa mama na hata watu wengine waliopo yaani siku hiyo yuko tayari hata kuwabeba mgongoni kuwapeleka popote, pia vyakula na vinywaji vitakavyo andaliwa hapo ntafikiri ni bethdei ya mtoto wa Mengi kwani kaka kabahatika kupata kazi na nafasi yenye pesa achilia mbali pesa ya mkewe,
  huyu shemeji tukipita pale kwake hutuoneshea upendo wa hali ya juu kwa kutuita majina kama vile sweethert,dear nk jambo ambalo ni changa la macho kwa vitendo anavyomfanyia mama.
  Jambo la kumuangalia mama hatukumuachia kaka peke yake
  sote tulishirikiana kwa pamoja kwani kila mmoja katika familia yetu ana ajira yake na hakuna anayemtegemea mwenzie,
  nilipogundua unyanyasaji huu nilipanga kumchukua mama ili niishi naye baada ya kuhitimu chuo kwan ndio nimehitimu mwezi wa saba shahada yangu
  ya kwanza na nilikuwa tayar ni mwajiriwa,
  ila wakati nahitimu mama alikuwa katika kipindi kigumu sana katika maisha yake cha kupambana na maradhi hadi yalipomchukua,
  nyumbani kwetu wote kila mmoja anajitegemea nyumbani kwake mikoa tofauti na hivyo mama alikosa kampani nyumbani na hivyo tulimshawishi sana kuwa anatutembelea na ndipo huu unyanyasaji ulimpata, ingawa aliishi pia kwa kaka zangu wengine hapakuwepo na tatizo lolote,
  huu unyanyasaji ninaouzungumzia ndugu zangu wanautambua isipokuwa kaka
  JAMBO nililoamua ni kwamba ntampigia shemeji simu kumtaka anipe majibu juu ya unyanyasaji alioufanya kwa mama,na kwa kuwa hakutaka mama ale wala kunywa chochote nyumbani kwake basi mimi ntachukua hiyo dhamana ya kutokula ,kutokunywa wala kulala nyumbani kwao,
  sababu pia ni kwamba mimi kama kijana wa mwisho ndio nilikuwa na jukumu la kukaa na mama lakini sikubahatika kufanya hivyo na matokeo yake ndio hayo mama akaishia kunyanyaswa,
   
 2. Laigwanan76

  Laigwanan76 JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 540
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Poleni sana,hao ndio wake zetu mkuu,machoni kama watu mioyoni hawana utu........kuna viumbe wa ajabu sana duniani......mimi nina mke wa marehemu baba yangu mkubwa,baada ya huyu baba kufa,mkewe akasema kilichokuwa kiunganishi kimeondoka hivyo kila m2 aangalie mambo yake,na hayo maneno mlengwa ni mkwewe yaaani mama wa marehemu.....kaazi kweli kweli!........ucjali sana walimwemwengu wanasema malipo hapa hapa duniani kwani naye yatamfika siku yake ikifika,sawa bin sawia!

   
 3. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kwanza pole sana Mkuu kwa kuondokewa na mama. Mungu amlaze pahali pema.
  Nahisi kama umechelewa kuchukua hatua wakati huu mama ameshaondoka. Ulipaswa kuliweka wazi hilo mapema kabla hajaaga dunia, na sio kwa shemeji yako bali kwa kaka yako kama una ubavu; vyenginevyo bora unyamaze. Kumweleza shemeji yako, anaweza kukugombanisha na kaka yako
   
 4. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  pole sana mkuu kwa msiba mzito ulioupata wa kuondokewa na mzazi
   
 5. ENZO

  ENZO JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,057
  Likes Received: 552
  Trophy Points: 280
  Pole sana mkubwa ....... Huyo shemeji yako ni muuaji!!
   
 6. peri

  peri JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Pole sana mkuu. Ndivyo wanadamu walivyo.
  Usiumie sana roho kwani malipo ni hapahap duniani.

  NOTE: Kwa watakao oa/kuolewa wawe makini kuchagua wenza kwani hili linatokan na kuwa na mwenza mbaya maishani.
   
 7. s

  shosti JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2011
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 4,949
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  mbona mmechelewa jamani,saa hizi mnatafutana ubaya tu
   
 8. 1

  1menARMY Member

  #8
  Oct 7, 2011
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana mkuu,ilahamjamtendea haki kaka yenu,mwelezeni ajua mapungufu ya mkewe ili ajiandae kama mama kafanyiwa hivyo haitashindikana kwake pia
   
 9. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,274
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Pole kwa msiba
   
 10. N

  Natalie Senior Member

  #10
  Oct 8, 2011
  Joined: Sep 25, 2011
  Messages: 165
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pole sana Bro, dah, kuna binadamu wa ajabu sana Duniani, asipoomba msamaha, malipo ni hapahapa Duniani.
   
 11. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #11
  Oct 8, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,723
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  pole sana kaka,vumilia mkuu na yote mwachie mungu.malipo ni hapa hapa duniani.
   
 12. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #12
  Oct 8, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  du haya mafindo findo yanaweza kuwasambaratisha aisee
   
 13. Likwanda

  Likwanda JF-Expert Member

  #13
  Oct 8, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 3,854
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Dah, Ubinadamu Kazi Sana, pole sana najua inakuuma sana ingawa yameshatokea. Yaani suala lakumpata mke mwema Mungu Atuongoze Sana.
   
 14. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #14
  Oct 8, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 416,972
  Trophy Points: 280
  Tukumbuke ya kuwa..............................."The righteous perish and no one takes it to heart. The merciful are being taken away and no one considers that the righteous are being taken away from evil." Isaiah 57:1
   
 15. s

  shalis JF-Expert Member

  #15
  Oct 8, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwanza pole kwa msiba mzito uliokupata...
  pili taarifa za kuwa mama yako alipatwa na maswahibu hayo ndio maana alifariki ni nani aliyekueleza
  na kama ni yeye kwann hukuchukua hatua mapema mpaka ameshafariki ,
  kama si yeye huyo aliyekueleza kwann asubiri mpaka mama afariki ndo aseme kama kweli ni mkweli kwako?
  ANGALIZO:Mama ameshafariki ndugu mliobaki ni ww na kak na wengine acheni ya mama maisha yaanze upya
  huku mkishirikiana kwa upendo huku mkijenga familia bora zaidi kwani ufa unaotaka kuujenga hapo unaweza sababisha hata vizazi vyenu kutengana trust me na hiyo ni picha mbaya sna...Nawasilishwa
   
 16. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #16
  Oct 8, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  pole kwa msiba mkuu. ubinadamu kazi watu wengine wanataka choyo na roho mbaya ziwatawale lkn wengine wanjitahidi kucontrol hiyo hali
   
 17. Z

  Zedikaya Senior Member

  #17
  Oct 8, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SHALIS hujaelewe hiyo mada rudia kuisoma,
  hajasema kuwa unyanyasaji ndio ulikuwa chanzo cha huyo mamaao kuaga dunia,
  ila alifanyiwa,
  pia ninavyoamini huyo mnyanyasaji anapaswa kujibu,
  na ni sahihi kufatilia jambo kama hilo,
  pia mtoa mada anadai baada ya kuona tatizo alipanga kumchukua mamaake kama suluhisho salama la tatizo na sio kumwambia kakaake agombane na mkewe ndo mamayao aishipo kwa amani?
   
 18. G

  Gm32 Member

  #18
  Oct 8, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
 19. s

  shalis JF-Expert Member

  #19
  Oct 8, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zedika ok, upo sawa mno
  je akishafuatilia na mnyanyasaji akijibu mashtaka ..whats next either kakataa au kakubali
  naona kama vile ana deal ana vitu vilivyo kwisha muda na atakacho kifanya ni kuongeza ufa na si kuuziba
  awe makini sana jinsi ya ku handle hii ishu unless awa na ushahidi tosha kuwa hata kama hakufa kwa ajili hiyo alinyanyaswa ...mmh mim kwa binafsi siwezi ku deal na hiyo ishu i will leave it na nifnaye mambo yangu mengine ...stop
   
 20. MADAM T

  MADAM T JF-Expert Member

  #20
  Oct 8, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 3,660
  Likes Received: 940
  Trophy Points: 280
  Naomba nikupe pole kwa msiba, lakini mpaka sasa hivi sijakuelewa kama ulikuwa unajua mama ananyanyaswa kwanini ulikuwa humuambiii kakayako? Huoni kama na wewe umeshiriki katika kumnyanyasa mama yako? Naomba majibu tafadhali...maana malalamiko unayoyatoa hapa ni too late ingeleta maana sana kama umngemuambia kaka yako mapema.....
   
Loading...