Mama ajifungu mtoto na CHURA huko Mbeya

Mama ajifungu mtoto na CHURA huko Mbeya

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,144
Reaction score
166,079
[h=3]BREAKING NEWSSS MAMA AJIFUNGUA MTOTO WA KIUME PAMOJA NA KIUMBE KINACHOFANANA NA CHURA WILAYANI CHUNYA[/h]



[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Mtoto aliyezaliwa pamoja na kiumbe cha ajabu kinachofanana na chura[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Mtoto akiwa na afya tele[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Hiki ndicho kiumbe kilchotoka tumboni pamoja na mtoto mchanga kwa mama Matrida picha hii mara baada ya kutenganishwa na mtoto huyo[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Kushoto ni Matrida Erick (20) aliyejifungua mtoto pamoja na kiumbe hicho cha ajabu akiwa na mkunga Agripina Sikanyika aliyembeba mtoto wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kujifungua kwa mkunga huyo[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD] [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Hapa ndipo kwa mkunga Agripina Sikanyika Matrida alipojifungulia watoto hao[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


Mkunga huyo akionyesha mkeka unaotumika kuwatandikia wajawazito wanaokuja kujifungulia katika kliniki yake





Mkunga akionyesha vibali vinavyothibitisha ruhusa aliopewa na Serikali kwa ajili ya kutoa huduma ya kuwazalisha akina mama wajawazito.




Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la MATRIDA ERICK mwenye umri wa miaka ishirini mkazi wa magamba ,wilaya ya chunya ,amejifungua mtoto jinsi ya kiume na wakati huohuo na chura.


Mkunga aliyemzalisha bi AGGRIPINA SIKANYIKA mkazi wa MBUYUNI wilaya ya chunya amesema tukio hilo limetokea majira ya saa tisa alasiri agosti 13 mwaka huu,mara mwanamke huyo kufikishwa kwa mkunga huyo na mumewe aitwaye BUNDALA JOSEPHAT ISANDU mwenye umri wa miaka thelathini na tano


MATRIDA amesema huo ni uzao wake wanne na kwamba alishangazwa na kiumbe hicho ingawa wakati anajifungua hakupata tatizo lolote na pia alifurahia kupata mtoto wa kiume mwenye afya na alisikitishwa kupata hicho kiumbe ambacho kilikuwa na miguu ya mbele yenye vidole vinne na miguu ya nyuma vidole vitano vya binadamu.


Kwa upande wake AGGRIPINA amesema mtoto alikuwa katika kondo lake na chura alikuwa katika kondo lake la nyuma la uzazi wa mwanamke huyo na pia ameeleza kuwa hilo ni tukio la tatu ambapo la kwanza mwanamke alijifungua kichwa cha ng’ombe mwaka jana na la pili mwaka huu mwezi wa tano ambapo mwanamke alijifungua chura badala ya binadamu kwa hiyo hili ni tukio la tatu hivyo hakushangazwa na tukio hilo.


Hata hivyo mume wa Matrida amesema katika familia yao hilo ni tukio la kwanza na kwamba limewashangaza.
Baada ya tukio hilo mkunga alimtafuta mwenyekiti wa kijiji cha MBUYUNI bwana CONRAD WAMBOKA ambaye alimtaarifu mtendaji wa kijiji MICHAEL SANZIMWA ambao walishuhudia tukio hilo na walimwamuru mkunga huyo kuondoa kiumbe hicho ‘’CHURA’’ kwenye kondo la uzazi.


Aidha chura hicho kilikufa na ndugu siku moja baadae ambapo ndugu walikabidhiwa na taratibu za mila zilifuatwa.
Baadhi ya ndugu wamehusisha kitendo hicho na imani za kishirikina zilizokithiri huko wilayani chunya.
 
Bujibuji hizo hirizi alizovalishwa tu hicho kichanga inadhihirisha wazi kuwa familia ya hiki kichanga wanapenda ushirikina. Zile ndumba za waganga wa kienyeji mnazokunywa ndizo zinazaa haya mambo. Sijawahi mvalisha mwanangu hata mmoja hirizi na ni wazima na wanangu for sure hakuna atakayevalisha mjukuu wangu hirizi hata aolewe na Maji Marefu. Ukipanda uwele unavuna uwele na si karanga.
 
Mkuu Bujibuji hii habari niliisikia last week ila nilikuwa natamani sana nione picha, asante kwa kutuletea hapa jamvini.

Aione pia Asnam
 
Last edited by a moderator:
Bujibuji hizo hirizi alizovalishwa tu hicho kichanga inadhihirisha wazi kuwa familia ya hiki kichanga wanapenda ushirikina. Zile ndumba za waganga wa kienyeji mnazokunywa ndizo zinazaa haya mambo. Sijawahi mvalisha mwanangu hata mmoja hirizi na ni wazima na wanangu for sure hakuna atakayevalisha mjukuu wangu hirizi hata aolewe na Maji Marefu. Ukipanda uwele unavuna uwele na si karanga.
Zogwale, licha ya kwamba jina lako limefanana na msitu wa matambiko lakini ndani ya moyo wako unamjua Mungu aliye hai, na unajua kuwa amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanamu, amfanyaye kuwa ngao na kinga ya maisha yake
 
Last edited by a moderator:
Zogwale, licha ya kwamba jina lako limefanana na msitu wa matambiko lakini ndani ya moyo wako unamjua Mungu aliye hai, na unajua kuwa amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanamu, amfanyaye kuwa ngao na kinga ya maisha yake

Ha ha ha mkuu Bujibuji, yaani kweli jina letu la wahenga unalitania aisee. Nimecheka sana. Hii ID ni ya kishua sana maana ni ya mzee wetu maarufu sana kwa ufugaji wa sungura na visili!!!
 
ndetichia, hebu mtafutie jina la chura kwa kilatini, ukimuita wa kiingereza akifika darasa la tatu ataonja joto la jiwe

Frog ataonza joto gani ya jiwe akifika la tatu? We si aende tu form one halafu ukute ni boys mazima!!! Atataniwa mpake ahame shule!!!
 
Jamani ina shangaza, Yaani haya matumbo yetu wanawake yanabeba mengi!!!!
 
Mbeya kwa sanaa za kijamii, kwa kweli sidhani kama wana wapinzani hapa Tanzania.
 
Duu! alikuwa anakunywa maji ya bwawani yenye viluilui yasiyochemshwa?
Afu hao wamama na kijiji kimechoka, wakipewa kanga na vilemba wanasahau shida zte.


Mkuu kama issue ni kunywa viluilui vya chura basi badala ya kuzaa chura angejisaidia chura, labda useme kuwa wanajisafishia ikulu kwa kutumia hayo maji nitakuelewa kidogo ingawa kwa shida sana.
 
Eeeewwww!!!!! Yuck! Yuck! Yuck! Ptu! Ptu! Ptu!
 
Mkuu kama issue ni kunywa viluilui vya chura basi badala ya kuzaa chura angejisaidia chura, labda useme kuwa wanajisafishia ikulu kwa kutumia hayo maji nitakuelewa kidogo ingawa kwa shida sana.

Duh afu kweli....

maybe alikuwa anajisafisha kwa ndani akaingiza na yai....sasa mabaki ya yai yakwapi?

Au aliingiza kachura kadogo kabisa.

Inamaana huyo chura alipokuwa akichezacheza humo akafkiri ni mtoto?

Uuuuggghhhh unbelievably gross
 
hivi kwenye vijiji vya huko kuna clinic zakueleweka kweli. Kwa hao wajawazito ikitokea mtoto hawezi kupita kwenye nyonga, si anakufa yeye na mtoto wake?
aise hali ni duni mno.
 
Tatizo lipo kwa jina la kijiji alichopo eti MAGAMABA
 
Back
Top Bottom