Malumbano ya hoja ITV usiku huu, Mada ni Ushoga

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2015
Posts
30,041
Reaction score
47,730
Wakili wa mahakama kuu afafanua kisheria ni kwa namna gani unaweza kumkamata shoga ni shughuli pevu kuthibitisha. Asema hakuna sheria inayozuia watu wa jinsia moja kuoana ila kuna sheria ya kuzuia kitendo ikiwa kuna mtu atalalamika amefanyiwa kitendo hicho. Sheria imetaja watu wasiotakiwa kuoana ila haijataja jinsia moja. Kipindi kinaendelea tuendelee kuchambua michango ya wachangiaji. Chanzo cha mada ya leo ni ile sherehe ya mashoga iliyofanyika hivi karibuni
 
Wakili wa mahakama kuu ni kama ameruka kimanga kuwaadhibu mashoga. Yaani mashoga wako huru hakuna kifungu cha sheria kinachowabana kuhusu kuoana
 
Wakili wa mahakama kuu afafanua kisheria ni kwa namna gani unaweza kumkamata shoga ni shughuli pevu kuthibitisha. Asema hakuna sheria inayozuia watu wa jinsia moja kuoana ila kuna sheria ya kuzuia kitendo ikiwa kuna mtu atalalamika amefanyiwa kitendo hicho. Sheria imetaja watu wasiotakiwa kuoana ila haijataja jinsia moja. Kipindi kinaendelea tuendelee kuchambua michango ya wachangiaji. Chanzo cha mada ya leo ni ile sherehe ya mashoga iliyofanyika hivi karibuni
Hii vita imetushinda tumechelewa kuamka
 
Lindeni watoto wenu, waelimisheni, waepusheni na adhabu kali zinazotweza utu wao, waepushieni na unyanyapaa hasa ngazi ya familia, fatilia miendendo ya mwanao, marafiki zake, mahali anapopenda kwenda kucheza , michezo yake nk.

Pia hakuna ulazima sana kwa mtoto kumiliki simu janja ikiwa mzazi huna uelewa na udhibiti wa maudhui ayaonayo huko.

Weka sheria zako nyumani kusiwe na uhuru wa manyani, mpe mwanao shughuli mbalimbali za kumjengea stadi za aina tofauti tofauti.

Na mwisho kabisa hiyo vita mnayopambana, hilo mnaloombea litokee ati mapunga wafutike kama upepo, wakatwekatwe na kuuawa, wafungwe nk hilo sahau haliwezi tokea abadan hapa Tz.
 
wakili kafafanua sheria, inaonekana hakuna kipengele cha kuwaweka hatiani, mtu akiwashughulikia mashoga anaweza kujikuta matatani
 
Kamanda wa polisi asema ule ukumbi kulikofanyika sherehe za mashoga umefungiwa na watu watatu wamekamatwa.
 
Mada zako hizi pendwa mchungaji loth ukisubiri wahalalishe uanze kuwabariki chooni kwako
 
Kamanda wa polisi kasema kama una ukumbi kuna watu wanautumia wajulishwe ni kina nani hao na wanafanya sherehe gani
 
Back
Top Bottom