Malumbano ya hoja ITV jana walishiriki watu 12 tu, je hoja siku hizi hazina mvuto?

dataone

Member
Jul 7, 2017
44
77
Jana nikiwa naangalia malumbano ya hoja kupitia ITV nikashangaa kuona washiriki wako 12 tu kitu ambacho siyo kawaida. Je siku hizi hoja mnazotoa ITV hazina mvuto kwa watanzania au kitu gani kimewapata .

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Kwa kasi hii ya Rais Magufuli hoja zitatoka wapi?

Walizoea awamu iliyopita walikuwa wanapata vya kuongea.
 
Nadhani jana watu wengi walichelewa kwenda kumuona Rooney

Sent from my TECNO-Y3+ using JamiiForums mobile app
 
Hoja ya jana ilikuwa nzito/ngumu mno kiasi kwamba hata wale wachache walioshiriki walikuwa wanapayuka tu bila kuwa na weledi kuhusiana na mchakato mzima wa wa vituo vya tiba kuagiza na kupokea dawa....

Wengi wao hasa yule bwana aliyeketi meza kuu,Bwana Bante aliishia kuwatupia lawama watoa huduma wetu huko kwe vituo.

Hata waongoza kipindi,mada iliwazidi kimo,mbwembwe zote wanazokuwaga nazo zilikuwa mfukoni jana
 
siku hizi itv, wanataka watu angalau wawasifie watawala, kitu ambacho wengi wao hushindwa na kuishia kunyang'anywa maiki
 
Jana nikiwa naangalia malumbano ya hoja kupitia ITV nikashangaa kuona washiriki wako 12 tu kitu ambacho siyo kawaida. Je siku hizi hoja mnazotoa ITV hazina mvuto kwa watanzania au kitu gani kimewapata .

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app

Kila mmoja atajikomba, hakuna ayakayesema ukweli toka rohoni. Watu waoga, ukisema kinyume unapotezwa ya nini kwenda huko

Sent from my HUAWEI G730-U10 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom