Malta Guiness haramu?

PakaJimmy

JF-Expert Member
Apr 29, 2009
16,203
8,724
Wakuu, tuko kwenye sherehe mahali isiyo na kilevi, maana kuna pia Walokole.

Lakini kumetokea mzozo, maana waandaaji wameweka Kinywaji inaitwa Malta Guiness.KunaWalokole wanaosema kinywaji hiki hakina shida maana hakina kilevi, kundi lingine wamegoma hata kuingia hapo ukumbini wakidai kinywaji hicho kinatengenezwa na mitambo ileile inayotengeneza Bia, kwahiyo hi haramu.

Embu wanaJF, tuwekenni sawa hii mambo!
 
Wakuu, tuko kwenye sherehe mahali isiyo na kilevi, maana kuna pia Walokole.

Lakini kumetokea mzozo, maana waandaaji wameweka Kinywaji inaitwa Malta Guiness, ambapo baadhi ya Walokole wanasema hakina shida maana hakina kilevi, ambapo wengine wamegoma kuingia ukumbini wakidai kinywaji hicho kinatengenezwa na mitambo ileile inayotengeneza Bia, kwahiyo hi haramu.

Embu wanaJF, tuwekenni sawa hii mambo!
Wana yao hao. Hiyo mitambo huwa haifanyiwi usafi kabla ya kubadili aina ya kinywaji kinachotengenezwa...????
 
Wakuu, tuko kwenye sherehe mahali isiyo na kilevi, maana kuna pia Walokole.

Lakini kumetokea mzozo, maana waandaaji wameweka Kinywaji inaitwa Malta Guiness, ambapo baadhi ya Walokole wanasema hakina shida maana hakina kilevi, ambapo wengine wamegoma kuingia ukumbini wakidai kinywaji hicho kinatengenezwa na mitambo ileile inayotengeneza Bia, kwahiyo hi haramu.

Embu wanaJF, tuwekenni sawa hii mambo!

This is too much na huu ni unafiki mkubwa. Hivi ni vingapi vichafu kabisa wanavijuwa fika still wanashiriki? Mungu hayuko complicated kiasi hicho wanamwonea kabisa for sure.Lakini pia kwani wamelazimishwa kunywa si wanywe soda au kama hazipo tuwaletee?
 
Yesu wa Nazareth tu alitengeneza mvinyo watu wakanywa wakachamka, alienda kwa watoza kodi watu waliokuwa wanajulikana kuwa wenye dhambi sana enzi hizo, sasa hawa wapendwa wenzangu mmmh akili zao haziko sawa wamemeza mafundisho hawaelewa hata kidogo.
 
Kuna mtu ana tatizo la High BP alikunywa kinyaji hiki --- BP yake ilipanda mno na alikaribia kufa na ilibidi kwenda hospitali ya Rufaa ambako aliambiwa kinywaji hiki kinapandisha BP kwa hiyo ni vema kikatumiwa na wenye low BP.
 
Wakuu, tuko kwenye sherehe mahali isiyo na kilevi, maana kuna pia Walokole.

Lakini kumetokea mzozo, maana waandaaji wameweka Kinywaji inaitwa Malta Guiness.KunaWalokole wanaosema kinywaji hiki hakina shida maana hakina kilevi, kundi lingine wamegoma hata kuingia hapo ukumbini wakidai kinywaji hicho kinatengenezwa na mitambo ileile inayotengeneza Bia, kwahiyo hi haramu.

Embu wanaJF, tuwekenni sawa hii mambo!

Wakishaanza kusema "kinywaji hiki kinatengenezwa na mitambo ile ile inayotengeneza bia" nini kinawazuia kufikiri vyakula vingine vinatengenezwa na mitambo iliyotengenezwa na mitambo inayotengeneza bia?

Kwa logic hii kila kitu ni suspect, itabidi waende kuishi katika community yao tofauti na watu wote, tena walime vyakula vyao wenyewe, kwa kutumia pembejeo watakazotengeneza wao wenyewe, maana wakichukua kitu kutoka nje, kama hakijatengenezwa na mitambo iliyotengeneza bia basi kimetengenezwa na mitambo iliyotengenezwa na mitambo iliyotengeneza mitambo ya kutengeneza bia.

Do you get my point?

Hogwash.
 
two thing mtambo wa bia huwezi ukatengenezea malta hata siku moja, ni sawa na muzi kuzaa kondoo, pia malta imesajiliwa kisheria huwezi ukaweka label kuwa ni alcohol free wakati kuna hata TRACE ya alcohol, kwa hiyo kama wamegoma ni wakati muafaka wa wenguni kukamata kilaji
 
Ili wanajamii tusiogope vivuli vyetu wenyewe ni vyema tuka conclude mambo kwa utafiti. Haiwezekani mtu ukajiongezea hofu bila sababu yoyote na huna taarifa yoyote tata kuhusu wasiwasi wako huo.

Pia kwa suala la sherehe nyingi zinazofahamika na kufanyika mijini siku hizi, huwa zinakuwa na kamati. kazi ya kamati hizi huwa ni maandalizi ya sherehe yenyewe, kwamba shughuli yetu itakuwa MOTO au BARIDI. Matokeo ya kutojihusisha katika kamati za shughuli kwa kusingizia uko busy ndiyo hupelekea kuwepo kwenye sherehe vitu ambavyo sio choice ya kila mwanasherehe.

Kama hampendi kitu fulani ni vyema mkaainisha hivyo kwenye vikao kwamba tunawasiwasi na kinywaji au chakula fulani kwa mujibu wa imani yetu hivyo, kisiwepo kwenye shughuli yetu.

Lakini kugomea kuingia ukumbini kwa sababu kuna kinywaji fulani naona hii kama HAIJATULIA !
 
Hao walokole ni psychotic na wanahitaji msaada wa haraka wa kitabibu!!

  • Basi waache kupanda hata public transport
  • Waache kwenda kumbi za harusi maana sie wengine hunwyea glasi hizohizo, sahani, vijiko nk.
  • wasipokee hata chenji popote maana nyingine zimepita kwa wazinzi na wapishi wa gongo nk

Hawa walokole wa namna hii pia ni extremists kama wale wengine
 
two thing mtambo wa bia huwezi ukatengenezea malta hata siku moja, ni sawa na muzi kuzaa kondoo, pia malta imesajiliwa kisheria huwezi ukaweka label kuwa ni alcohol free wakati kuna hata TRACE ya alcohol, kwa hiyo kama wamegoma ni wakati muafaka wa wenguni kukamata kilaji

NduguAM_07,

Huenda hujabahatika tu kutembelea KATIKA kiwanda chochote cha Breweries, au related. Lakini mimi nikwambie, nimefanya kazi huko muda mrefu wa kutosha.

Mitambo inayotengeneza na kujaza Safari Lager ndiyo hiyohiyo inayotengeneza na kujaza Malta Giuness! Ni kwamba kati ya vitendo hivyo viwili, kuna kitu inaitwa CIP, yaani uoshaji wa uhakika wa mitambo kabla ya kuanza kupitisha jamii nyingine ya Kinywaji!

Jifunze hilo!
 
kama mitambo inatumika ileile halafu ikasafishwa kitaalamu tatizo lipo wapi? kama malta ingekuwa na traces za alcohol si ingeandika kwenye chupa?
kweli kabisa hao ni extremists
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom