Mall mpya Jijini Mwanza ni kituko cha karne

Hakuna tatizo mkuu. Daima kinachopopolewa na kufananishwa huku na kule kinawawashawasha wakosoaji in JPM voice
Hata sisi tunaiombea Mwanza ipige hatua kwa kuwa iki-aibika Mwanza inaadhirisha Tanzania nzima. Sasa jiji gani kubwa lakini hadhi yake ni ya kumulika kwa tochi mara ifananishwe na Kisumu, Jinja, Toro,Bukavu, Nakuru, Bujumbura n.k wakati mji unapaswa kuwa kwenye rank sawa au zaidi ya kigali, Kampala n.k
 
Hivi hilo jengo la sijuwi gorofa 9 (mall) mnalo lilia ,litawapa ugali wa kula na familia zenu?,acheni malalamiko pesa za maboto yaye mwenyewe ndiyo anaamua afanye nini ata angejenga vyoo vya kulipia ni fedha zake.Na hiyo mall si mnataka kwenda kupiga picha tu kwani kuna cha zaidi ya hicho.

Unachowaza ni kula tu Mr. Pesanyingi, nikwambie tu hata kama tunaingia kwenye Malls kupiga picha, Wakenya husema "sisi ndiyo hao tuko" na hao wanaotupiga picha tukishangaa-shangaa tiyari wamejiajiri, ikiwa hujui hata kama Mall ni fursa inayoweza kutuajiri watanzania wenzio tukalisha familia zetu kwanini ulifungua akaunti JF?
 
mwamza Mall bado mno mno, Ile Mall sijui Rock City Mall nia aibu tupu pale. MWanza mambo ya Mall bado mno, Mall iachiwe Dar na Arusha pekee.
Ile haiitwi rock city mall...
Huwa ni imeandikwa rock city more.....(halafu kuna maneno mbele)..ila tumezoea kuiiita mall
 
Anatuchafulia jiji tu
Kulikua na vibanda kavunja kajenga vingine sa ndo nn
Yaani zile ni akili za kilevi na wote walioruhusu kitu kama kile kifanyike hawako sawa upstairs, hata kama ni maokoto wakati mwingine common sense ni muhimu ikitumika.
 
"Eneo la Maboto",walipo bomoa vibanda pale National ndipo wakaweka Mabango yaliyosomeka hivyo...nikawa natamani kumfahamu huyu Maboto,pale Mtaa wa Lumumba Kuna jengo Limeandikwa Maboto enterprise....Je? Huyu Maboto Ni Nani?
 
Mkurya 1 hivi wa huko Bunda mwenye elimu kama ya msukuma ila pesa ako nayo japo waalim hawana ham nae kawanyosha wakanyoka vilivyo!
 
Hiyo ngoma ilikuwa ni proposed kabisa na ilikuwa na mchoro wake kabisa ilikuwa imebaki tu utekelezaji, sasa sijajua ni mdudu gani aliingia kwenye kichwa cha investor mpaka akapindua plan na kufanya yake.
Wacha maneno mengi. Weka michoro.
 
Malls zinafanya vizuri Dsm pekee
Hata hiyo DAR bado ni tia maji tia maji, kiufupi utamaduni huo kwetu bado ni kizungumkuti japo tunapaswa kuendelea kujenga hizo malls kila mahali ili kubadili consumers buying behavior badala ya kupendelea shopping za barabarani tuanze kuona Malls ni mahali pia pa kuhemea mahitaji yetu ya kila siku.
 
Hata huko Dar, ni upuuzi mtupu, ndio maana kampuni zote za South Africa zimekimbia..
Nchi masikini halafu imejaa biashara ya wachuuzi, , ni vigumu sana kuwa na modern consumer power.....
mtu hata kama ana kipato kizuri, ameshazoea kugalaliza bei, kwahiyo atanunua kwa machinga au gengeni,
huko mall wanaona ni kwa wadosi na wazungu
 
Unachosema ni kweli, kutokana na umasikini wa nchi yetu hatuna purchasing power, hatuna viwanda vya ndani ambavyo vingeweza ku-harmonize soko na kuleta affordable price kwa walaji.

Hatujawa na mikakati mizuri katika ku-link cultural preference ya walaji na huduma mf. kuwapa options za kubargain bei, promotions,kunadiwa bidhaa, burudani, michezo n.k huko kwenye Malls ili kuwavutia zaidi.

Unafikiri kwanini mtanzania huyu huyu uudhuria maonesho ya Sabasaba au Nanenane na ununua bidhaa ila katika Malls haendi?

Malls hazitoi varieties ambazo ni adimu kwa kiasi kikubwa huku mitaani ili watu walazimike kuwafuata na cha mwisho ni Serikali na wawekezaji inatakiwa kupunguza kodi (kuwepo na punguzo maalumu) wanazotoza katika bidhaa na majengo ya mall ili kuipa biashara hii ahueni na ari ya kushindana na rundo la biashara zisizo rasmi katika mitaa ambazo uuza bidhaa zile zile kwa bei ya chini.

Na kama Serikali itataka kodi stahiki basi na yenyewe iwajibike kwanza katika kukuza uchumi au vipato vya wananchi wake hili Malls ziweze kujiendesha kwa faida kuepuka biashara za namna hii kufungwa mara kwa mara kwa kukosa wateja.
 
Kodi kubwa ya pango na bado kodi za TRA......
 
Back
Top Bottom