Malkia wa mahaba

Jomba Wajo

Member
Apr 6, 2012
33
17
ki.jpg




SIMULIZI ZA JOMBA WAJO

MALKIA WA MAHABA.

Sehemu Ya 37.

***

Kwa wasomaji wapya;

Jomba Wajo, ama maarufu kama Joo, kijana mtanashati na mwenye uwezo wa kimaisha, anakumbana na mikasa mikubwa baada tu ya kukutana na kuangukia kwenye penzi la binti mrembo Irene, ama kwa jina maarufu ‘Malkia Wa Mahaba´kutokana na ufundi wake kwenye yale mambo yetu. Mikasa inaanza pale Joo anapotaka kulitetea penzi la Malkia huyo kutoka kwa Mike Tikisa, mtu hatari sana na anayeng’ng’ania penzi la Irene kwa nguvu. Ndani ya mkasa huo, Joo anagundua mambo mengi ya kusikitisha na kuhudhunisha ambayo asingeweza kuyajua kama asingekutana na Malkia Wa Mahaba. Tuendelee tuone ni kitu gani kilichojiri…..


“Ni kawaida yake upandisha presha?” Nilimuuliza Sherieta.

“Hapana. Tangu arudi kutoka Africa kusini amekuwa akihangaika sana.” Alijibu.

“Ndiyo, lazima ahangaike sana. Mwisho wa maovu yake umefika sasa. Hana pa kutokea tena.” Nilikazia.

Tulikuwa tumefika kwenye Morocco, kwenye mataa ambayo barabara ya Kawawa inaanzia na kukutana na Barabara ya Ali Hassan Mwinyi. Wakati tunasubiri zamu yetu ya kupita, niiendelea na mahoiano yangu na yule binti.

“kwanini Mike anapenda sana kutumia madereva wa kike?”

“Kwa sababu hatusumbuliwi sana na matrafiki barabarani. Vilevile anaaminikuwa mabinti ni waaminifu.” Sherieta alijibu bila kusita.

“Kwa mfano, kama Mike atafariki leo, nani atakulipa mshahara wako?” Nilimuuliza swali la kutisha kidogo. Sherieta alifikiri kwa muda kisha akajibu,

“Nafikiri ndiyo utakuwa mwisho wa ajira, kwa sababu mimi nieajiriwa moja kwa moja na Mike, sijaajiliwa na Makampuni yake.”

“Ok. Sikiliza Sherieta. Najua wewe huna kosa lolote na wala sina tatizo na wewe.Nina tatizo ni Mike, na mwisho wake ndiyo umefika. Kama tutaelewana vizuri nitakutafutia kazi nyingine nzuri itakayokufanya ufurahie maisha ya hapa mjini kwa amani, baada ya Mike kuwa aidha kauwawa au anasotea jela.”

Nilitulia ili kumuangalia yule binti atajibu nini.

“Tuelewane ktu gani?” Aliuliza kwa wasiwasi.

“Kuanzia sasa nataka uwe upande wangu na ufanye kila itu nitakachokuelekeza.” Nilimwambia na kushuhudia alivyoipokea kwa shingo upande sana amri yangu. Ikawahi kmpa angalizo,

“Siyo lazima lakini. Kama hujalizika na hili dili unaweza kukataa tu kuliko kukubali kwa shingo upande halafu uje kunigeuka.”

Bado hakuwa tayari kunijibu. Sura yake ilionyesha kuwa kuikuwa na mgogoro kwenye akili yake. Kati ya kukubali ama kukataa hakuua aende upande upi.

“Muda ndiyo kitu adimu sana kwa sasa Sherieta. Nimekupa uhuru wa kuchagua bila shuruti. Kama unakubaliana a mimi basi tuendelee na mpango wetu. Kama haupo tayari basi waweza kutelemka na kwenda zako. Ahadi yangu kwako ni ileile, sitakudhuru.”

Maneno yangu yalizidi kumchanganya yule sherieta na kumweka njia panda.

“Kabla taa hazijaturuhusu kuendelea na safari namba uwe umeshaamua. Lakini kumbuka kuwa Mike hana maisha marefu.” Nilimsisitiza a kumpa nafasi ya kuamua.

“Sawa, nipo tayari?” Sherieta alijibu auku akiwa ametizama chini.

“Vizuri. kumbka kuwa umekubai kwa hiyari yako hivyo sitegemei tena kukuona ukinigeuka” Nilimtahadharisha na kuendelea, “Mike ameambatana na vijana wangapi hapo jhospitali?”

“Wawili.” Aliibu kifupi.

“Tutajuaje kama wapo hospitali ama wameshaondoka?”

“Watakuwa bado wapo hospitalini, vinginevyo wangekuwa wamenipigia simu.”

“Una simu?” Nilimuuliza kwa sababu jioni ile nilkuwa nimemnyang’anya simu yake.

“Yaa, ninayo. Nilipata nyingine.” Alijibu

“Fanya hivo fasta sasa. Ila tumia akili.”

Sherieta alitoa simu yake mfukoni. Alipekua namba fulani isha akapiga.

“Oyaa, Man P, vipi huko mbona imekuwa kitambo sana?”

“Hali ya Boss siyo nzuri huku. Inasemekana alizidisha dozi ya cocaine ndiyo inayomletea shida.” Ilijib sauti ya pili kutoka kwenye simu.

“Kwa hiyo itakwaje sasa?”

“Bado tunamsikilizia dokta anayemshghulikia akitoka atupe jibu.” Sauti kwenye simu ilijibu.

“Poa.” Sherieta alikata simu na kuniangalia.

“Nadhani mmesikia”

“umesikia izri kabisa. Na ni bora akapitiliza ahera kabisa kuliko kusubiri kifo tulichomandalia. Angejua angeliomba asiamke tena.”

Wakati huo taa zilikuwa zimeturuhusu. Nilimwambia baba aliyekua anaendesha lile gari ageuze gari pale kwenye maktano ili turudi tulikotoka. Akafanya hivyo.

“Ulisikia kuwa wale jamaa mliokuwa nao kule kipunguni waliuawa?” Nilimuliza Sherieta.

“Tulizipata kupitia Whatsapp, na ndiyo iliyosababisha hata Mike apandishe presha. Nashukuru sana kwa kuninusuru kaka”

“Waliaribu kuleta ujeuri wakakutana na wananchi wenye hasira kali. Ndiyo maana nakusihi uwe mtii na ufanye kama tulivyoelewana. Wewe bado ni binti mdogo na maisha bado yanakuhitaji. Ila kileta ujanja wowote kuna uwezekano mkubwa sana ukawafuata hao wenzako.” Nilimtisha ili kumuweka sawa.

“Tunaenda nyumbani kwa Mike. Nambie tutaingiaje ili walinzi wasitushtukie.” Niliaka kutumia muda huo ambao Mike alikuwa hospitali fanya uchunguzi wangu nyumbani kwa Mike, ilikujaribu kama nitapata nyaraka zozote zinazowahusu akina Irene na mdogo wake kama nilivyoelezwa na Bi. Mariamu. Pamoja na kumtokomeza Mike, nilipanga pia kurejesha mali zote za akia Irene ambazo Bi. Mariamu alisema Mike alimdhlumu baba yao.

“Kwa hili gari hatutaweza kuingia. Labda tutumie lile ‘Prado tuliloliacha hospaitlini, hilo ndio limezoeleka kwa Mike.”

“Wazo zuri sana Sherieta. Sasa naona utakuwa maswahiba wazuri.” Nilimsifu Sherieta na kushuhudia tabasamu zuri la furaha likichomoza usoni mwake kwa mara ya kwanza. Nikajua tayari nilishamnasa kwenye kambi yangu. Baba aliendesha gari mpaka nje ya geti la hospitali ile. Akasimamisha. Mimi na Sherieta tukashuka na kulisogelea lle Prado lililompeleka pale Mike. funguo nilikuwa nazo mimi, nikalitoa kwenye ‘lock’ na kumkabidhi funguo Sherieta ili aliendeshe, mimi nikakaa pembeni yake. Alilitoa lile gari kwa mwendo wa kasi huku baba akitufuata kwa nyuma.

Tuliondoka moja kwa moja mpaka Ununio, aeneo ya Bunju ilikokuwa nyumba ya Mike. ni siku mbili tu nyuma tulifanya twimbwili pale tukiwa na Tito pamoja na Irene hivyo nilipafahamu vizuri sana tulipokaribia mita kadhaa kufika, nilimsimamisha baba na kumwambia anisubiri pembeni ya barabara. Nilimsihi awe makini wakati anatusubiri. Sherieta aliendesha gari na klipitisha getini kwa Mike bia bughudha yoyote ya walinzi, ambao walimfungulia geti tu na kumruhusu kuingia.

Utaratibu wa ulinzi katika nyumba ile haukuwa umebadilika. Nyumba ile ililindwa sana kwa nje, kwa makamera ya CCTV pamoja na walinzi wakawaida na geti lililozungshwa senyenge za umeme. Ulipoingia ndani uani hakukuwa na mtu na hata wale mbwa tuliowaua ile juzi yake walikuwa hawajaletwa wengine. Palikuwa kimya kabisa.

Sherieta alisogeza gari mpaka mlangoni, nikamtanguliza kuingia ndani nikiamini kuwa hatoweza kunifanyia uhuni wowote. Na kama angeamua kunifanyia janja wowote basi yeye ndiye angekuwa wa kwanza kufa kabla yangu kwani bastola yangu aina ya Taurus PT-92 AF, ilikuwa kamilikamili kiunoni kwangu.

“Nipeleke kwenye chmba cha Mike.” Nilimwamurisha Sherieta abae aliniongoza mpaka kwenye ngazi za kuelekea kwenye ghorofa. Nyumba ile ilikuwa na ghorofa moja tu. Ukitaka kujua uzuri wa nyumba ile fikiria tu nyumba yoyote ambayo aaweza kishi bilionea wa kitanzania. Iliuwa ni nyumba nzuri kwelikweli yenye kila kitu cha kisasa. Tulipofia kwenye mlango wa chumba ambacho Sherieta alinifahamisha kuwa ndiyo cha Mike, alisimama pembeni na kutazama nitachotaka kufanya. Mlango ulikuwa umefungwa. Nakumbuka Irene alishawahi kuniambia kuwa mango ule ulifkwa ukifunguliwa kwa “passoword” maalumu na uliuganishwa kwenye progaramu maalumu kiasi kwamba kifunguliwa tu basi Mike anapokea taarifa kwa njia ya simu.

UNAWEZA KUISOMA STORI YOTE MWANZO HADI MWISHO (VIPANDE 53) KUPITIA LINK HII HAPO CHINI:

https://jombawajo.blogspot.com
 
Back
Top Bottom