Malkia Mbegu ya papai Inachakachuliwa

Malkia Mbegu ya papai Inachakachuliwa

MJIMPYA

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2011
Posts
506
Reaction score
273
Nilinunua pakiti ya gm1 ya malikia na kuipanda mwaka jana. Mipapai imeanza kuzaa ila cha kushangaza ni kuwa matunda ni tofauti.

Mbegu ya malkia imechorwa papai lefu nami nilitegemea matunda yatoke hivyo. Mengi ya matunda yametoka yale mafupi na miti michache imetoa yale marefu.

Najua kuna wakala wao anajiita africasia ndo anaagiza kwa wingi na kupaki. Katika kupaki anachanganya na mbegu nyingine. Huu ni wizi mkubwa na ubabaishaji. Kwa nini mnafanya hivo?
 

Attachments

  • Malkia.jpg
    Malkia.jpg
    20.6 KB · Views: 229
Kilimo kina changamoto nyingi ambazo saa ingine hasara husika hadi kwa mlaji.

Mie ilishanitokea nimenunua embe au nazi au tikiti maji kufika nyumbani unakuta ndani limeoza halifau kutumia ila kwa nje linaonekana vizuri tuu.

Ubovu huu ujiugundua wakati unanunua bidhaa unaikataa na kuchukua mbadala ambayo iko nzima. Kutokujua kwa Ubovu wa bidhaa huko kunaanzia mbali, unaweza kuta yule muuzaji sokoni nae kununua toka kwa mkulima embe nje zuri ila ukikata ndani funza watupu huwezi kula.

Mkulima nae aidha alipewa mbegu hafifu au mbolea iliisha muda wake haikuwa na nguvu au madawa ya kuzuia wadudu hakuweka au alitapeliwa akauziwa maji badala ya dawa..... nani haswa anatakiwa abebe hio hasara ya embe bovu ndani ila nje zima? Ndomaana saa ingine muuzaji anapandisha bei ya bidhaa kufidia zile ambazo hazitauzika zitakuwa mbovu. Mfano nazi ingeweza kuuzwa Tsh 300 hadi 400 na akapata faida,ila kubeba risk ya zilizooza na hazitauzika wakati yeye keshazilipia toka kwa mkulima kila nazi itauzwa Tsh 1000 ukibembeleza Tsh 800. Hapo akikuta zote nzima basi heri kwake muuzaji.

Kilimo kina changamoto nyingi sana, jaribu wakati mwingine kuchukua bidhaa kutoka kwa wakala mkuu yaweza punguza tatizo.
 
Afadhali kuleta mada hii humu jamvini, labda kuna atakaesaidia!! Maana mbegu ni janga nchi hii na wakulima wala hatujui nani wa kumlalamikia!! Mwaka jana nilipata hasara mbaya kabisaa, nilinunua mbegu ya mahindi ya faru ya elf 84, jamani haikuota kabisaa!!
 
Na idadi ya matunda kwa mti Ni kama yalivyo kwenye picha?
 
Picha ya cover huwa n kwa ajil ya kumvutia mteja bila kujua kwa nchi zilizoendelea unashtakiwa kabsia
 
Mimi Nina uzoefu kidogo na hiyo mbegu maana nimeotesha mipapai hiyo kadhaa na ninaendelea kuotesha in bunches!

Na ninauza Miche hiyo MAlkia F1
.nilichogundua ni kweli mbegu zimechanganya yaani mapapai marefu na mapapai ya round yaani matunda hii ni matokeo ya bunche ya kwanza kuanza kuzaa ya Miche 70 hivi....
Pili nimegundua uzaaji wa papai inategemea sana hali ya hewa,aridhi na utunzaji yaani mbolea hasa za chumvi chumvi ni kama ilivyo mazao mengine.
Kingine usikate tamaa otesha mipapai inasaidia kukuza kipato na ni matunda kwa afya.
Mi ninalimia kiluvya gogoni dsm na imezaa vizuri ila haitofikia MTU aiyeko LAbda moshi ,Arusha au Mbeya huko itazaa zaidi
Kwa mahitaji ya Miche na matunda ...piga

0755404226
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom