Negemu
Senior Member
- Dec 26, 2017
- 135
- 127
Niko kwenye majaribio ya kilimo cha papai,aina ya malkia F1, nilinunua packet moja ya mbegu, ambayo ina mbegu 80, hatua ya kwanza niliziloweka kwenye chombo chenye maji safi kwa muda wa suku 5 na kila suku nilikuwa nabadilisha maji, siku ya 6 nikahamishia hizo mbegu kwenye kitambaa cheupe kisafi kilicholoana nikazifunga kwa pamoja,na kuziweka juu ya sahani kwenye meza kwa siku 5, huku nikiloanisha kwa maji kidogo kila suku kwa muda wa siku 5,siku ya sita nikafungua kikakuta baadhi ya mbegu zimepasuka, nikahamishia kwenye viriba nilivyokuwa nimejaza udongo uliochanganyika na mbolea iliyooza,nilichimba shimo dogo kwa kutoboa na kijiti na kuweka mbegu mojamoja kwenye kila kiriba, nimekuwa nikimwagilia kila siku tangu tarehe 31/5/2019 mpaka leo tarehe 24 sijaona dalili yeyote ya kuota, sijui nilikosea wapi