Jipatie mbegu ya papai za kisasa (malkia F1)

Mosses Anney

Mosses Anney

Member
Joined
Sep 2, 2015
Messages
8
Points
45
Mosses Anney

Mosses Anney

Member
Joined Sep 2, 2015
8 45
  • Papai hizi ni papai za mda mfupi miezi sita tu unavuna, papai hizi ni tamu na nyekundu ndani ina zaa mpaka papai 105,
  • Soko lake ni kubwa sanaa,
  • Eka moja inauwezo wakukupa mpaka milion 100.

Tufanye hesabu kidogo:
1 acre =1000/1200 miche ya papai
kila mti wa mpapai unazaa 105
kila papai ni Tsh 1000 japokua inaweza kuwa zaidi kulingana na ukubwa.

kwahiyo =1000miche X 100papai/mti X 1000Tsh =100,000,000Tsh

Mche Tsh 3500
Mbegu Tsh 30,000 kwa pakti inakuwa na mbegu 70/80


Tuwasiliane:
0752972727
 

Attachments:

mbinde

mbinde

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2015
Messages
772
Points
1,000
mbinde

mbinde

JF-Expert Member
Joined Mar 12, 2015
772 1,000
Jamaa anataka Pesa ya miche na Pesa ya mbegu
100M anakuachia ukatafute mwenyewe
Me nakukumbusha tu kunagharama ya dawa hujaziingiza hapo.
 
Karucee

Karucee

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2012
Messages
14,065
Points
2,000
Karucee

Karucee

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2012
14,065 2,000
Jamaa anataka Pesa ya miche na Pesa ya mbegu
100M anakuachia ukatafute mwenyewe
Me nakukumbusha tu kunagharama ya dawa hujaziingiza hapo.
Hajaweka allowance ya natural occurances mfano losses as a result of recent floods.

Papai zinalipa yes, but lets not get carried away na kuanza ku overstimate profits.
 
M

Magazine Fire

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2011
Messages
692
Points
500
M

Magazine Fire

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2011
692 500
  • Papai hizi ni papai za mda mfupi miezi sita tu unavuna, papai hizi ni tamu na nyekundu ndani ina zaa mpaka papai 105,
  • Soko lake ni kubwa sanaa,
  • Eka moja inauwezo wakukupa mpaka milion 100.
Tufanye hesabu kidogo:
1 acre =1000/1200 miche ya papai
kila mti wa mpapai unazaa 105
kila papai ni Tsh 1000 japokua inaweza kuwa zaidi kulingana na ukubwa.

kwahiyo =1000miche X 100papai/mti X 1000Tsh =100,000,000Tsh

Mche Tsh 3500
Mbegu Tsh 30,000 kwa pakti inakuwa na mbegu 70/80


Tuwasiliane:
0752972727
Kilimo hakiko hivyo mkuu, uwezi piga hesabu za hivyo. Kila mtu angekuwa tajiri.
 
Lady Ra

Lady Ra

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2014
Messages
831
Points
1,000
Lady Ra

Lady Ra

JF-Expert Member
Joined Mar 23, 2014
831 1,000
  • Papai hizi ni papai za mda mfupi miezi sita tu unavuna, papai hizi ni tamu na nyekundu ndani ina zaa mpaka papai 105,
  • Soko lake ni kubwa sanaa,
  • Eka moja inauwezo wakukupa mpaka milion 100.
Tufanye hesabu kidogo:
1 acre =1000/1200 miche ya papai
kila mti wa mpapai unazaa 105
kila papai ni Tsh 1000 japokua inaweza kuwa zaidi kulingana na ukubwa.

kwahiyo =1000miche X 100papai/mti X 1000Tsh =100,000,000Tsh

Mche Tsh 3500
Mbegu Tsh 30,000 kwa pakti inakuwa na mbegu 70/80


Tuwasiliane:
0752972727
Mkuu kwema?
We Ushawahi kulima hata heka moja tu ya hizi Mbegu?
Unaweza kutupa mrejesho?
 
Tatigha

Tatigha

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2017
Messages
1,769
Points
2,000
Tatigha

Tatigha

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2017
1,769 2,000
Mnatulisha sumu mpate utajiri Dunia kweli inaelekea ukingoni...! Mpapai gani una kimo cha sturi lakini unazaa namna hiyo
 
Uchira 1

Uchira 1

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2017
Messages
1,689
Points
2,000
Uchira 1

Uchira 1

JF-Expert Member
Joined Oct 9, 2017
1,689 2,000
mkuu mpango wa biashara si rahisi hivyo, hizo hesabu ni rahisi kupita kawaida, mchanganua wa soko pia nao ni rahisi sana watanzania wanauwezo wa kuzalisha vile wawezavyo ila kinachosumbua huwa ni soko la uhakika
 
Tajiri Kichwa

Tajiri Kichwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2017
Messages
2,158
Points
2,000
Tajiri Kichwa

Tajiri Kichwa

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2017
2,158 2,000
Peleka pale magogoni ... utapata mteja wa mbegu na papai zake
 
R

Rotomoto

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2017
Messages
604
Points
1,000
R

Rotomoto

JF-Expert Member
Joined Aug 22, 2017
604 1,000
Kilimo cha kwenye makaratasi kama anavyaosoma kwenye vitabu, ajaribu tu hata kutumia mtaji wa milioni 1 aone atakavyohaha kuirudisha. Zao lenyewe halitunziki yangekuwa mahindi, mpunga au maharage kama soko haliko poa unaweza ukapaki stoo
 
Turnkey

Turnkey

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2013
Messages
4,644
Points
2,000
Turnkey

Turnkey

JF-Expert Member
Joined Jul 9, 2013
4,644 2,000
Watanzania kwa ubishi ingia shambani Fanya kazi...Mapapai yapo aina tatu, jinsia ya kiume, kike na jinsia zote (Hermaphrodite papaya).

Hata hivyo, aina zote tatu zinategemeana katika uzalishaji.

Mpapai wenye maua ya kiume uhitajika katika urutubishaji wa mpapai wenye maua ya kike ili kupata matunda, ingawa wenye maua ya jinsia zote hujirutubisha wenyewe.

Zipo za aina mbili za mbegu: mbegu za kawaida ambazo huweza kupatikana popote kwenye papai lililoliwa. Changamoto iliyopo ni ugumu wa kubaini mbegu zipi ni za aina gani ya mpapai.

Aina ya pili ya mbegu ni chotara , mbegu zote huwa ni ya mipapai nyenye maua ya kike na ya kiume pamoja. Hii hukua haraka na kutengeneza miti mifupi yenye uzao mkubwa ukilinganisha na ile ya kienyeji.

Upandaji

Panda mbegu moja tu kwa kila kiriba chenye udongo uliochanganywa vizuri na kujazwa robo tatu. Kisha viweke chini ya kivuli umwagilie maji.

Mbegu huchukua siku nane hadi 15 kuchomoza, hivyo hakikisha unamwagilia maji kila siku ila yasiwe maji mengi. Hamisha mche toka kwenye kitalu baada ya wiki ya sita hadi nane.

Hakikisha kazi ya uhamishaji mimea inafanyika wakati wa asubuhi sana, jioni ama kukiwa na mawingu ili kuzuia madhara ya jua kwa mimea.

Wakati wa kuhamishi miche shambani, hakikisha nafasi kati ya mmea na mmea ni mita 2 hadi 2.5 na kati ya mstari na mstari ni mita 2.5 hadi mita 3.

Andaa mashimo yenye upana na urefu wa sentimita 60, tenga udongo wa chini na wa juu kisha changanya udongo wa juu na mbolea ya samadi.

Unaporudisha udongo kwenye shimo tanguliza udongo uliochanganywa na mbolea ya samadi na juu malizia udongo ulioutoa chini wakati wa kuchimba shimo.

Kwa wale wenye mashamba makubwa, mipapai huingia kati ya miche 1000 hadi 2000 kwa hekari moja. Pia, 400 hadi 800 kwa ekari moja.

Mmea ukishahamia shambani bado kutahitajika matumizi ya mbolea, wiki moja baada ya kuhamishia shambani weka mbolea gramu 28 kila mmche lakini usitumie mbolea yenye Chlorine bali tumia yenye Phosphate, mfano; - 12:24:12. (NPK).

Baada ya hapo kila baada ya wiki mbili weka mbolea yenye Nitroni kwa kiasi kikubwa kiasi cha gramu 56 kwa mmea. Mfano, 20:10:10 (NPK).

Kisha tumia mbolea yenye Potassium kiasi cha gramu 114, baada ya maua na matunda kutokeza. Kisha fanya hivyo kila baada ya mwezi. Mfano wa mbolea hii ni 12:12:17 +2 (NPK).

Weka mbolea ya majani yenye virutubisho vidogo vidogo ikiwemo boron kila mwezi. Boron ni mbolea ya muhimu katika kupata matunda mazuri. Ukifuata utaratibu huu baada ya wiki 37 tangu kupanda mbegu utaanza kufaidi matunda hadi mpapai utakapochoka kuzaa.

Kwa mpapai uliotunzwa vizuri kwa msimu huweza kutoa matunda 80 hadi 120. Ikiwa umepanda mipapai 1000 kwa ekari maana yake utakua na mapapai 96,000 hadi 120,000
 

Forum statistics

Threads 1,326,022
Members 509,361
Posts 32,209,126
Top