Lu-ma-ga
JF-Expert Member
- Sep 21, 2010
- 4,780
- 3,227
Habari zilizoandikwa na Frederick Katulanda wa Gazeti la mwananchi zinasema.
ZOMEA zomea kwenye mikutano ya kampeni ya CCM jana ilimgeukia mpigadebe aliyejaribu kuingiza masuala ya maisha binafsi ili kumponda mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa baada ya wananchi kumzomea mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama tawala, Benno Malisa.
Zomeazomea hiyo imeshawakumba wagombea ubunge wa majimbo tofauti ambao waliteuliwa kugombea nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM baada ya washindi kwenye kura za maoni kuchakachuliwa.
Jana ilikuwa zamu ya Malisa kwenye mkutano wa kampeni wilayani Geita ambako alikuja kumnadi mgombea ubunge wa Geita Mjini, Donald Max. Malisa, ambaye ni mmoja wa vijana walioteuliwa kuzunguka nchi nzima kufanya kampeni za CCM, alitaka kuwapa wananchi hao maana ya neno "fisadi".
Huyu (Dk Slaa) anapita na kuomba achaguliwe, ameshindwa kwenye uparoko sasa ataweza kuongoza nchi," alihoji Malisa. "Kule Kenya ukielezea neno fisadi maana yake ni mtu anayetembea na wake za watu, sasa Slaa amechukua mke wa mtu yeye si ndiye fisadi namba moja? Lakini wananchi walianza kuguna na baadaye kuzomea huku wakinyoosha mikono juu kuonyesha vidole viwili, ambayo ni alama ya Chadema.
Kutokana na kelele hizo, Malisa aligeuza uelekeo wake wa mazungumzo na akaamua kumuita mgombea wa udiwani wa Kata ya Kalangalala, Daudi Ntinonu na kumnadi.
Karibuni wana JF