Malisa ampinga kwa fact Polepole kuhusu CCM kuiletea maendeleo Moshi

mike2k

JF-Expert Member
May 12, 2016
1,458
3,127
malisa_gj-20180726-0001.jpg

Huyu dogo ameanza kuchanganyikiwa. Moshi ilianza kuendelea zamani za pontio pilato kabla ya ujio wa Dr.Livingstone na Gavana Edward Twining.

Mwaka 1902 barabara zinazounganisha mitaa mbalimbali ya Moshi zilikuwa na lami, enzi hizo CCM haijazaliwa, mama yake TANU wala bibi yake TAA.

Mwaka 1895 Ikulu ya kwanza ya kisasa ya Mangi mkuu wa wachagga ilijengwa eneo la KDC Moshi. Ikulu hiyo hadi sasa ndiyo inayotumika kama Ikulu ndogo ya Rais akija mkoani Kilimanjaro.

Mwaka 1917 dola ya wachagga ilikuwa na mfumo rasmi wa serikali na baraza la mawaziri, ikiwa ni pamoja na ofisi na magari kwa watendaji waandamizi wakiwemo mawaziri. Ofisi za mawaziri ndio zinatumika leo kama ofisi za halmashauri ya wilaya ya Moshi.

Miaka 100 iliyopita Moshi kulikuwa na viwanda mbalimbali kikiwemo kiwanda kikubwa zaidi cha kubangua kahawa eneo la Afrika Mashariki. Mwaka 1940 dola ya wachagga tayari ilikuwa na gazeti lake (Komkya), lililokuwa likisomwa maeneo yote ya wachagga kuanzia Siha hadi Rongai. Gazeti hilo liliandikwa kwa lugha ya Kiswahili.
-
Kufikia mwaka 1950 karibu kila kata au tarafa ilikuwa na shule ya sekondari, zahanati au kituo cha afya pamoja na kanisa la kisasa, kuanzia Siha mpaka Tarakea. Sio zote lakini nyingi zilikuwa na shule zilizojengwa na wamisionari miaka mingi sana iliyopita.

Wakati chakubanga na babu yake wanatembea kilomita 50 kwenda kuchoma chanjo ya tetekuwanga, wazee wa kichagga walikua wakipata huduma za afya kwenye vituo vya afya vya mission vilivyopo kwenye kata/tarafa zao.

Leo mtu mmoja pengine kwa sababu ya kukosa chanjo ya pepopunda anaropoka kwamba maendeleo ya Moshi yameletwa na CCM? What a shame.!!
-
Kimsingi CCM na serikali yake zimezorotesha maradufu maendeleo ya Moshi kuliko wakati mwingine wowote katika historia. Moshi ya wakati ule (kama dola yenye mamlaka kamili), na Moshi ya leo (kama wilaya) ni vitu viwili tofauti. Moshi ingeachwa kuwa dola huru kama ilivyokuwa zamani, ingekuwa na maendeleo maradufu kuliko leo.

Halafu kama kweli CCM inaleta maendeleo, mbona kuna mikoa haijawahi kuchagua upinzani na bado haina maendeleo? Kwanini maendeleo hayo CCM isipeleke kwenye ngome zake? Next time mwambieni kabla hajabwatuka ajifunze historia kdg.!!!!!!!!!
Screenshot from 2018-07-27 12-02-11.png

Source instagram:Malisa_gj
 
Last edited by a moderator:
Wa kwanza seat ya mbele na Bakuli langu la Popcorn...hahahaha.Ndio maana unaambiwa kupata basic education ni jambo muhimu sana na hata kujifunza historia zetu.Kuna watu walishapiga makofi hapo .....Ila vyovyote ni sawa
 
Nikikumbuka nimesoma shule ambayo imeanzaga 1908 alafu kanya boya anasema ccm imeleta maendeleo moshi nashindwa mwelewa. Ni kujipendekeza. Kwao ni dodoma huko wasijipendekeze kwetu

Nashangaa makao makuu ya CCM haina hata stendi juzi nimeona ITV stendi ipo porini wageni wakifika stendi inabidi wasafiri tena km 11 Kutafuta sehemu ya kulala. Hapo mmegonga mwamba
 
Hakuna maendeleo yanayoletwa na chama sehemu flani ila watu wa eneo husika ndio wanaoweza kuleta maendeleo eneo husika kama hao wachaga waliamua kujenga eneo lao. Polepole lazima aongee hivyo ili awapotoshe wale wasiojua historia ya Moshi ili chama chake kipate kura
 
malisa bana!Anazungumzia historia
Lazima amekubali maendeleo bila ya amani na utulivu si lolote,Malisa hakutoa Takwimu mangi aliacha shule ngapi na leo zipo ngapi
Kama barabara imejengwa na mangi 1940,lazima ifanyiwe ukarabati au kujengwa upya
miaka ya 80,malisa alikua hajazaliwa,ilikua kwenda moshi lazima ulale njiani kwa ajili ya kuvunja springi au kupasua tairi kwa ubovu wa barabara,malisa hajui kakuta lami watu wanaenda kwa corolla
 
Hakuna maendeleo yanayoletwa na chama sehemu flani ila watu wa eneo husika ndio wanaoweza kuleta maendeleo eneo husika kama hao wachaga waliamua kujenga eneo lao. Polepole lazima aongee hivyo ili awapotoshe wale wasiojua historia ya Moshi ili chama chake kipate kura
Hapo umenena point mkuu
 
Conspiracy theories zipo nyingi sana za kuwarudisha nyuma kimaendeleo, kila awamu ilikuwa na mkakati wake. Awamu ya kwanza ilivunja nguvu ya chama cha ushirika KNCU, awamu ya pili ikakazia hapo, awamu ya tatu ikawavunjia biashara zao Shekilango na Sam Nujoma road na kauli mbiu ikawa kila anayetaka kuneemeka lazima ajiunge na CCM(Sumaye), awamu ya nne ikaanza kuwapunguza kujiunga na vyuo vikuu na ajira serikalini, awamu ya tano ndio usiseme kabisa.. vunja kimara yote mpaka mbezi bila fidia, ondoa kwenye teuzi zote, kataa pendekezo lolote la kuifanya Moshi jiji, kadiria kodi kubwa kwa wafanyabiashara na mengineyo mengi yaliyo chini ya carpet yakitekelezwa kimya kimya. Lakini kwa msaada wa Muumba watavuka, kwani huwa hawaachi kutoa zaka zao (fungu la kumi) kama walivyoagizwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom