Malipo ya wema wangu

Habari Wana JF,

Kuna misemo tunaisikia Sana

1. Ukiona mtu ni bahili Sana ujuwe mwanzoni alikuwa ni mtoaji Sana Ila wanadamu tu ndio wamembadili.

2.Ukiona mtu ni katili sana fuatilia maisha yake awali alikuwa MTU wa huruma Sana lakini binadamu walimbadilisha.

Sasa Turudi kwa mada.

Kila mtu katika ukuaji wake Kuna rafiki yake wa karibu ambaye anaweza kushaurina Mambo wa kadha.

Binafsi nimeishi na rafiki yangu tangu tukiwa tukiwa watoto wadogo kutokana na urafiki wa Bibi yangu na Bibi yake huyo kijana walikuwa marafiki Sana zaidi ya Sana nasi tukavutiwa na urafiki huo.

Japo kuwa tulikuwa wadogo sana lakini tulikubaliana kuwa marafiki wa mfano kaka Bibi zetu walivyokuwa.

Ikawa bahati pia shule ya msingi tulibahatika kusoma pamoja japo kuwa tulipishana darasa lakini hiyo haikuwa kikwazo kwani tulikuwa tunaishi jirani sana.

Tuliishi vizuri sana kwa upendo wa Hali ya juu. Ikawa bahati Tena tulipomaliza darasa la Saba tulichaguliwa kujiunga shule ya sekondari Moja hivyo tuliendelea kuwa pamoja na karibu Sana.

Ikumbukwe hapo tulikuwa tunaishi mkoani Tena vijijini Sana. Baada ya kuhitimu kidato Cha nne matokeo yalitoka tukachaguliwa kuendelea na masomo. Site tulipangiwa mjini japo shule tofauti.

Kwa upande wake alikuwa na ndg mjini ambaye alimuita bamkubwa yaani kaka wa baba yake mzazi wa huyo rafiki yangu.


Na Mimi mjini ilikuwepo Nyumba ya mzee. Bahati Nzuri hiyo Nyumba ilikuwa karibu Sana na shule alivyokuwa amechakuliwa rafiki yangu.

Kutokana na mazingira ya kwa mzee wake mkubwa kuwa na watoto wengi vyumba vichache nikamwomba rafiki yangu tuishi wote kwetu maisha yakaendelea kwa upendo kukua siku Hadi siku

Ilifika hatua watu wakajua sisi ni mapacha maana tulianza kufanana hata kisura Siri zangu akawa anazifahamu 90% na Mimi pia vivyo hivyo


Nilitokea kumpenda Sana rafiki yangu kwani alikuwa ni mtoto yatima hivyo nikaona tufarijiane maana mwenyewe nilikuwa nimepoteza wazazi wangu woote.

Siku za weekend tulikuwa tunaenda kwao huku Mimi nikijitahidi kadri tuwezavyo kubeba japo kitu mkononi kupeleka kwao hivyo tulikuwa tunapita sokoni na kununua viazi na majimbi then Safari Moja kwa Moja kwao.

Siku Moja walitukalisha kwao na rafiki yangu na kutuhasa urafiki wetu usije ukavunjika tufike mbali zaidi huku walisema sisi tumekutana woote ni yatima hivyo tupendane Sana.

Maneno ya wazazi yaliniingia Sana nami nikiahidi kamwe siwezi kumtupa jamaa yangu.

Wanasema ukikaa karibu na mtu ndio unamfaham huyo mtu ni wa Aina gani. Niligundua rafiki yangu anampenda Sana kusoma na kufika mbali kielimu pia alikuwa sio mtu wa kujichanganya na wasichana.

Lakini pia niligundua ni mtu wa aibu Sana mbele ya wasichana yaani ilikuwa hata ukimuuliza Jambo la maelezo mbele ya wanasicha alikuwa anashindwa kukueleza.

Basi maisha yakaendelea nikijitahidi Sana kumfanya rafiki yangu awe nafuraha ilifika hatua niliomba pesa kwa baba yangu ilimradi niweze kumsaidia rafiki yangu na familia yake kutokana na Hali halisi ya kuwa baba yake mkubwa alikuwa na familia Pana sana mbaya zaidi wote walikuwa wanaishii nyumbani pale.

Pale kwao kulikuwa na binti mmoja yaani mtoto wa baba yake mkubwa kwa umri alikuwa na miaka 16+ ambaye aligundulika kuwa na ujauzito.

Sikuamini niliyoambiwa na rafiki yangu kuwa ndiye muhusika wa ule ujauzito yaani shetani alimpitia mpaka akalala na Mdogo wake.

Katika kumuuliza kwanini alifanya hivyo Jambo la aibu Sana. Alifanya bila kukusaidia kwani siku hiyo hisia zilimzidi na hakuwa na msicha/menzi yeyote wala kuwahi kukutana na msichana yeyote kimwili.

Bahati mbaya ni kwamba matokeo ya kwenda Chuo yalikuwa yametoka na alikosa mkopo kabsa kutoka bodi ya mkopo. Hivyo Ada ilitakiwa itoke mfukoni kwa baba yake mkubwa.

Wakati huo huo binti akabanwa kwao kumtaja muhusika wa ujauzito, rafiki yangu alichanganyikiwa Sana kwani wazazi wake wangejua kwanza wangemfukuza na kumtamkia maneno mabaya pamoja na kushindwa kuendelea kumsomesha ikizingatiwa ni yatima na mkopo alikosa.

Nililazimika kubeba mzigo ili rafiki yangu awe na amani kwani ilikuwa ni kitendo Cha aibu Sana.

Tukaongea na Yule binti kuwa anijate Mimi ndiye muhusika na sio kaka yake, japo ilikuwa ngumu Sana lakini sikupenda ndoto ya rafiki yangu kusoma iishie njiani pia atengwe na ndugu zake.

Basi nikatajwa mimi, kutokana na ukaribu niliokuwa nao kwa upande wa ndugu wa rafiki yangu pamoja na kuwajali kwa kidogo kilichowezekana waliamini 100% kuwa Mimi ndiye muhusika.

Bahati mbaya Sana wazazi wa yule binti walisema nimchukue yule binti na kuenda kukaa nyumbani kwetu. Sikuwa na namna ilinibidi nikubali maana nilikiri kuwa Mimi ndiye muhusika wa ule ujauzito.

Basi rafiki yangu akaenda Chuo tayari kwa masomo. Mimi nilishindwa kuenda Chuo kwa wakati ule kutokana na lile tukio pia nilikosa msaada kutoka kwa ndugu zangu kwani malichukia Sana.

Niliishi na Yule binti nyumbani kwetu nachoshukuru nyumbani kulikuwa na vyumba vya kutosha japo nilikuwa kwenye wakati mgumu lakini nilipambana kadri nilivyoweza.

Yule binti akajifungua kwa operation watoto mapacha. maisha yakaendelea huku ndugu zangu na ndugu wa rafiki yangu waliamini Mimi ndiye muhusika wa wale watoto.

Kadri watoto walivyokuwa wanakua likaonekana tatizo kwa wale watoto wana uzezeta. Maisha yakaendelea.

Lakini rafiki yangu alivyokuwa Chuo urafiki ulidrops down asilimia kadhaa nilipomuuliza akasema busy ya masomo.

Ikanibidi nimtafutie nafasi ya Chuo veta Yule mama wawili akasoma na kupata cheti.kisha akapata sehemu ya kujishikiza wakati huo huo rafiki yangu Chuo alikuwa amechange kabsa mpaka wiki inaipita no mawasiliano.

NB: samahani wadau naomba nimalizie kesho Mimi ni mvivu wa kuandika hata hapa naona nimejitahidi Sana.


ITAENDELEA KESHO.....

Shukrani Sana kwa kuwa pamoja nami. kuna kitu mtajifunza yawezekana likawa funzo kwa wengine wengi.
Malipo ya wema.
 
Back
Top Bottom