Umenikumbusha pia kuna majani fulani ya porini pia tulikuwa tunatumia kama majani ya chai.... siku moja majani yameisha nikaenda kuyachuma nikanywa chai nyingine nikabakisha kwenye sufuria, dada yangu akaikuta akaniuliza haya majani umechemsha ya nini nikamweleza matumizi yake hakuamini kaenda kumuuliza rafiki yake eti kweli haya ni majani ya chai? Akaambiwa ni majani ndio kwani we hujawahi kuyatumia? Alikuwa ameshafikiria makubwa sana