Malipo ya wahanga wa mabomu Mbagala katika picha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Malipo ya wahanga wa mabomu Mbagala katika picha

Discussion in 'Jamii Photos' started by Fidel80, Aug 25, 2009.

 1. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  Waathirika wa Mabomu wakisubili zamu yao kuitwa kwenda kupewa hundi ofisi za manispaa Temeke.

  [​IMG] Wakihakiki picha zao za majengo na walipwaji halali.

  [​IMG] Wakipokea Hundi zao kutoka kwa maofisa husika wa Manipaa.

  [​IMG] Akionesha hundi yake japo hakuridhika na malipo aliyopata ya sh Milioni 1.6.
  [​IMG] Waliona malalamiko waliwasilisha baada ya kupokea Hundi au kabla.maana wapo wanaolipwa 30,000 wakati alitaraji milioni kadhaa.
   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hapo ma elfu 30 ndo panaponipa headache!something IMPOSSIBLE KABISA
   
 3. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  yani inahuzunisha kweli, huyo aliepewa 30 elfu ina maana makazi yake yalikuwaje awali mpaka wakampa hiyo? hata yawe ya namna gani lakini so ubinadamu kabisa.
   
 4. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  mwingine alikuwa na nyumba nzuri kapewa laki na 65
   
 5. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #5
  Aug 25, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hao wanaolalamika wangekaa kny nyumba zao wapigwe picha then tuliyoko mbali tunaweza kudiscuss vizuri
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Aug 25, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mkuu hata kama kilikuwa kibanda cha miti hakiwezi kufidiwa kwa 30,000/= unajua gharama ya mti mmoja? Unazungumzia 8000-12000 sasa kwa 30,000 utafanyia nini?
   
 7. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #7
  Aug 25, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Poti sikiliza, si rahisi kujua ukweli wa ni madhara gani mtu alipata na amepewa nini kama si kuonyeshwa hali ya mali zake ilivyokuwa mara kabla na baada ya mlipuko mkuu......!

  Unaweza ona ukweli ukawa huyo aliyepewa 30k alipovunjiwa jiko lake la mkaa nje ya nyumba yake or alikuwa kaanika nguo zikapotea wakati wa vurumai.....etc etc etc.....au ikawa kweli kapunjwa kulinganisha na kilichotokea kwa ajili ya mabomu!
   
 8. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #8
  Aug 25, 2009
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hii serikali mbona ya uonevu hivi? hata huyo aliepewa mil 1.5 naamini haitoshi hata kupandisha chumba kimoja, its so unfair
   
 9. PingPong

  PingPong JF-Expert Member

  #9
  Aug 25, 2009
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 933
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 45
  Kwa haraka haraka naona kuna utata ila sijui ugawaji huu unachukua vigezo gani, uzuri,uimara au ukubwa wa nyumba? na je vitu vingine vilivyohalibika navyo vipo humuhumo kwenye hiyo fidia au ndio kila mtu na lake. Haya mambo ya kusema serikali inatoa fidia ni maigizo tu na kuwafumba watu ili waone kuwa serikali inawajali watu wake lakini lazima kasoro zitakuwepo nyingi na kama unataka kuumiza roho yako vizuri wewe jaribu kufuatilia watu waliopewa hizo fidia utakuta wengine walistahiri hawakupewa na wengine hawakustahiri wamepewa tena fidia kubwa zaidi ya waathirika.
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Aug 25, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Jamani na yule aliye kuwa na nyumba ya vyumba 6 unajua alilipwa bei gani??? Sijui wale watathimini nao kuna 20% bila shaka naamini hivyo huwezi mpa fidia mtu mwenye nyumba ya vyumba 4 eti unampa 640000/= hata nyumba ya nyasi na miti hatoweza jenga sijui mnamkomoa.
   
 11. Amigo

  Amigo Senior Member

  #11
  Aug 25, 2009
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35

  Hapa tatizo ninalo liona watu wanalipwa fidia kwa mujibu wa sheria za fidia na ninatumaini kabisa hizi sheria hazijafanyiwa marekebisho kabisa kuendana na wakati, So hatujui wanatumia sheria gani. Je hapa mtu analipwa fidia ya nyumba na thamani ya vitu vilivyo potea? mimi sijui tatizo ni marekebisho ya sheria tu.
   
 12. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #12
  Aug 25, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  elfu 30?
  kwa vigezo vipi vilivyotumika?hata kule kijijini kwetu kilolo hujengi hata kibanda cha nyasi sembuse mbagala hapo?labda nisiseme sana kwakuwa sijui ni vigezo gani vilivyotumika,labda inataka kufanana na ile ya malipo ya wastaafu wa afrika mashariki
   
 13. O

  Omumura JF-Expert Member

  #13
  Aug 25, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  kuna mwingine jengo la choo chake ndo lilibomoka, amelipwa milioni ishirini, is it fair?
   
 14. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #14
  Aug 25, 2009
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Watanzania ni lazima ifike kipindi tubadilike. Ni lazima katika jambo linalotokea maishani mwako zuri au baya ni lazima ujifunze kitu.

  Kwa hawa wahanga wa mbagala, na huu mchakato mzima wa ulipaji -- achilia mbali kama umeenda kwa haki au lah, swali ni "Watanzania tumejifunza nini hapa?"

  Mipango ya miji ipo wapi? Takwimu za wakazi wa eneo zipo wapi? Nani anaweza kujua nani anakaa wapi na nani anakaa wapi - utaratibu haufahamiki.

  Kama kuna mtu amepanga, fidia analipwa nani - mwenye nyumba, mpangaji au wote? Kama mpangaji atafidiwa, we undadhani inaweza fanyika tathmini ya uhakika kwenye mali zake hapo - lazima kutakuwa na utata kiasi fulani.

  Wahanga wa mbagala ni janga letu sote, lakini ni lazima serikali na wananchi tujifunze somo hapa!
   
 15. Buricheka

  Buricheka Member

  #15
  Aug 25, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ofisa anashughulikia watu kumi kwa mpigo, kila mtu anaona faili la mwenzie, ukisema chupi zako zote zimeungua wananchi wanaangalia kwenye komputer zilikuwa zimechoka kiasi gani, za aina gani, halafu mwingine akipewa hela kidogo malamiko yataanza, kumbe mwenzako kaunguziwa makochi, wewe umeunguziwa chupi.

  Kuna vitu Tanzania vimekaa kushotooo....
   
Loading...