Malipo ya tiba hospitali za Serikali

Malipo ya tiba hospitali za Serikali

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
24,368
Reaction score
29,894
Hospitali za serikali zimeweka mabango makubwa yakionesha gharama za tiba, gharama hizo zinaashiria kuwa serikali imejitoa kwenye huduma ya tiba kwa wananchi wake.

Moja ya jambo ambalo sikubaliani nalo ni malipo ya kumuona mganga ambaye no mwajiriwa wa serikali kama walivyo waajiriwa wengine, mahakimu, wakuu wa mikoa na wilaya, wabunge,mawaziri na wengine wengi ambao tunagharamia mishahara yao, kwanini waganga tuwagharamie mara mbili! Kupitia mishahara ambayo ni kodi zetu na pesa taslimu kupitia hospitali! Hii siyo sahihi.

Jambo jingine, kwanini tulipie karatasi za kujiandikisha (kadi)! Hizi zinanunuliwa kutokana na kodi zetu, mbona TRA, jiji, biashara na kwingineko hatulipii? Ninadhani gharama hizi zimepangwa kwa kufananisha na hospitali binafsi.

Mwisho, serikali inatakiwa iwe na sera ya afya kwa wananchi badala ya kutumia sera ya chama kwani kitakachotokea sasa ni wananchi kushindwa kumudu gharama za tiba na kutumbukia kwenye vikombe vya babu jambo litakaloleta usugu wa maradhi, pia kuwatelekeza wagonjwa waliolazwa kwa kushindwa kulipa deni la tiba na kususa kuchukua maiti kutokana na gharama za mochwari.

Sijui uchumi utakuwaje kwenye taifa la wagonjwa! Tuachane na mtindo wa sera za vyama tuwe na sera za taifa ingawa vyama tawala havipendi kwani vinataka vionekane vimeleta maendeleo matokeo huwa havifanikiwi.
 
CCM na serikali yake ni wachawi wanataka wananchi tufe watule nyama waridhike,maana haiwezekani hao madokta tuwaajiri na salary tuwape halafu watake na pesa nyingine ya kwenda kuonana nao huu ni uchawi dhidi ya wananchi
 
Sion tatzo kwa hospital kuweka mabango ya gharama kwa sababu inaonesha hospital saivi zinatakiwa kujiendesha kwa mapato yake kwa baadhi ya mahitaji muhimu kama umeme, dawa n.k
Ni jukumu la serikali kutamka wazi kuwa tumeshatoka kwenye mfumo wa ujamaa ambapo serikali ilikuwa ikigharamia social services na kuhimiza kila mwananchi kujiunga na huduma ya bima na wale wasio na uwezo serikali iwalipie kwa mfuko maalum wa afya kwa wote! Hii itapunguza watu kwenda kwa sangoma na matapeli kina Dr. Mwaka na pia itaboresha huduma hospitaln kwa sababu hospital zitaweza kujiendesha kwa kuwa na uhakika na vyanzo vya uhakika.
Bima iwe universal(kila mmoja) na iwe rahisi kwa kila mwananchi kwa mfano kila mwenye leseni ya biashara alipe elfu hamsini n.k
Serikali iajiri wataalam wa afya wenye ujuzi na kwa sababu kila mtu atakuwa na bima watumishi hawa wataweza kulipwa mishahara na posho husika. Pia sioni mantiki ya hospital za mikoana wilaya kuwa na clinical officers hawa wapelekwe kuanzia ngaz za vituo vya afya kurud chini huku kukifanyika utaratib wa kuifuta fani hii isiyokuwepo baadhi ya nchi.
Mwisho serikali ibadili sera ili kuweza ku retain brains(hii sio katik sekta ya afya pekee) kwa kutoa competitive salaries and incentives. Wale watu wanaomfuata daktari mzuri private wamfuate hospital ya serikal ili kuongeza mapato serikalini, hili linawezekana kwa kuboresha maslahi na kulipa incentives km performance related bonuses n.k
 
Sijui wana maanisha nini wanavyojitangaza serikali ya wanyonge.!

Ile kusema ni serekali ya wanyonge huwa nafananisha na tangazo la sigara. Wote husema sifa nzuri za sigara lakini kiuhalisia sigara huleta kansa na uharibifu mwingine wa mwili. Hilo neno la serekali ya wanyonge ni kivumishi cha kuteka wajinga.
 
1. Dawa/tiba ni mahitaji ya kawaida na ya lazima kwa binadamu kama ilivyo chakula. Gharama yake kwa wastani yanalingana na gharama ya chakula kwa mwaka. Hivyo kama ilivyo ukweli kwamba serikali haiwezi kuwapa chakula bure wananchi wake, ndivyo ilivyo kwamba serikali haiwezi kuwapa dawa/tiba bure wananchi wake. Usitake kulinganisha gharama ya kutoa elimu bure (shillingi billioni 20 kwa mwezi) na dawa/tiba bure (shillingi trillion 30 kwa mwaka = bajeti nzima ya mwaka).

2. Ili mgonjwa aweze kupata tiba sahihi lazima apitie hatua kadhaa za mchakato (process) au mkondo wa kitaaluma ambao ni standard (wa kimataifa). Mgonjwa hulipia kila hatua ya mchakato huo.

3. Hatua ya kwanza lazima asajiliwe. Akishasajiliwa anapewa kadi kama mfumo wa usajili ni manual (wa makaratasi). Siku hizi mfumo wa usajili katika hospitali nyingi ni wa ki electronic unaotumia komputa. Mfumo huu hauna kadi au makaratasi yo yote: mgonjwa anaingizwa kwenye system ya hospitali. Analipia ada ya kujisajili. Si kwamba analipia gharama ya kuchapisha karatasi ya kadi.

3. Hatua ya pili ni mgonjwa kuonana na daktari ambapo ataeleza matatizo yake yote ya kiafya. Daktari atamsikiliza, atamhoji mambo fulani fulani ili kupata picha halisi ya matatizo ya mgonjwa (kwa kitaalamu inaitwa history). Baada ya hapo daktari atapima mwili wa mgonjwa wake: kwa kuuangalia kwa macho, kuupapasa papasa kwa mikono na vidole nje na ndani kupitia matundu mbali mbali ya mwili, na kusikiliza milindimo mbali mbali ndani na nje ya mwili huo. Hii kwa kitaalamu inaitwa physical examination. Baada ya daktari kupata history na physical examination, daktari atafanya majumuisho na uchambuzi wa kina wa kitaalamu (clinical analysis) na kufanya maamuzi (clinical descion) ya hatua gani zingine zifuate na mpangilio wa hatua hizo. Hatua hizo zingine zinaweza zikawa za maabara, za kiradiolojia, za upasuaji, za madawa, mionzi, physiotherapy na kadhalika.

Hiyo hatua ya history, physical examination, clinical analysis hadi clinical descion ndiyo kwa kitaalamu inaitwa Medical Consultation ambayo mswahili anaita kumwona (to see) daktari. Hatua hii muhimu ndiyo inalipiwa shillingi elfu kumi kama daktari ni wa kawaida (medical officer) au elfu thelathini kama daktari ni daktari bingwa. Pesa hii ni ya hospitali, si kwamba atapewa huyo daktari. Ni pesa ya serikali. Pesa ya daktari ni huo mshahara wake tu. Serikali inakusanya pesa yake kwenye kila mchakato huo wa tiba ie kwenye usajili, medical consultation, maabara, mionzi, upasuaji, dawa, kulala hospitalini, kulala mortuary, na kadhalika. Jumla ya gharama kwa mgonjwa inaweza kuwa mamillioni ya pesa kama tatizo la mgonjwa ni kubwa. Pesa hiyo yote ni ya serikali na hutumika kugharimia huduma hiyo ya afya.

BADALA YA KULALAMIKA, WANANCHI WAELIMISHWE KUJIUNGA NA MFUKO WA BIMA YA AFYA WA TAIFA. NCHI ZOTE ZILIZOENDELEA ZINAFANYA HIVYO, HAZITOI TIBA BURE BURE. SISI TUTAWEZA VIPI KUTOA TIBA BURE?
 
Sion tatzo kwa hospital kuweka mabango ya gharama kwa sababu inaonesha hospital saivi zinatakiwa kujiendesha kwa mapato yake kwa baadhi ya mahitaji muhimu kama umeme, dawa n.k
Ni jukumu la serikali kutamka wazi kuwa tumeshatoka kwenye mfumo wa ujamaa ambapo serikali ilikuwa ikigharamia social services na kuhimiza kila mwananchi kujiunga na huduma ya bima na wale wasio na uwezo serikali iwalipie kwa mfuko maalum wa afya kwa wote! Hii itapunguza watu kwenda kwa sangoma na matapeli kina Dr. Mwaka na pia itaboresha huduma hospitaln kwa sababu hospital zitaweza kujiendesha kwa kuwa na uhakika na vyanzo vya uhakika.
Bima iwe universal(kila mmoja) na iwe rahisi kwa kila mwananchi kwa mfano kila mwenye leseni ya biashara alipe elfu hamsini n.k
Serikali iajiri wataalam wa afya wenye ujuzi na kwa sababu kila mtu atakuwa na bima watumishi hawa wataweza kulipwa mishahara na posho husika. Pia sioni mantiki ya hospital za mikoana wilaya kuwa na clinical officers hawa wapelekwe kuanzia ngaz za vituo vya afya kurud chini huku kukifanyika utaratib wa kuifuta fani hii isiyokuwepo baadhi ya nchi.
Mwisho serikali ibadili sera ili kuweza ku retain brains(hii sio katik sekta ya afya pekee) kwa kutoa competitive salaries and incentives. Wale watu wanaomfuata daktari mzuri private wamfuate hospital ya serikal ili kuongeza mapato serikalini, hili linawezekana kwa kuboresha maslahi na kulipa incentives km performance related bonuses n.k
Umeme, maji, majengo, mishahara na gharama zote za uendeshaji fedha hutoka serikalini wakati wa bajeti.
 
1. Dawa/tiba ni mahitaji ya kawaida na ya lazima kwa binadamu kama ilivyo chakula. Gharama yake kwa wastani yanalingana na gharama ya chakula kwa mwaka. Hivyo kama ilivyo ukweli kwamba serikali haiwezi kuwapa chakula bure wananchi wake, ndivyo ilivyo kwamba serikali haiwezi kuwapa dawa/tiba bure wananchi wake. Usitake kulinganisha gharama ya kutoa elimu bure (shillingi billioni 20 kwa mwezi) na dawa/tiba bure (shillingi trillion 30 kwa mwaka = bajeti nzima ya mwaka).

2. Ili mgonjwa aweze kupata tiba sahihi lazima apitie hatua kadhaa za mchakato (process) au mkondo wa kitaaluma ambao ni standard (wa kimataifa). Mgonjwa hulipia kila hatua ya mchakato huo.

3. Hatua ya kwanza lazima asajiliwe. Akishasajiliwa anapewa kadi kama mfumo wa usajili ni manual (wa makaratasi). Siku hizi mfumo wa usajili katika hospitali nyingi ni wa ki electronic unaotumia komputa. Mfumo huu hauna kadi au makaratasi yo yote: mgonjwa anaingizwa kwenye system ya hospitali. Analipia ada ya kujisajili. Si kwamba analipia gharama ya kuchapisha karatasi ya kadi.

3. Hatua ya pili ni mgonjwa kuonana na daktari ambapo ataeleza matatizo yake yote ya kiafya. Daktari atamsikiliza, atamhoji mambo fulani fulani ili kupata picha halisi ya matatizo ya mgonjwa (kwa kitaalamu inaitwa history). Baada ya hapo daktari atapima mwili wa mgonjwa wake: kwa kuuangalia kwa macho, kuupapasa papasa kwa mikono na vidole nje na ndani kupitia matundu mbali mbali ya mwili, na kusikiliza milindimo mbali mbali ndani na nje ya mwili huo. Hii kwa kitaalamu inaitwa physical examination. Baada ya daktari kupata history na physical examination, daktari atafanya majumuisho na uchambuzi wa kina wa kitaalamu (clinical analysis) na kufanya maamuzi (clinical descion) ya hatua gani zingine zifuate na mpangilio wa hatua hizo. Hatua hizo zingine zinaweza zikawa za maabara, za kiradiolojia, za upasuaji, za madawa, mionzi, physiotherapy na kadhalika.

Hiyo hatua ya history, physical examination, clinical analysis hadi clinical descion ndiyo kwa kitaalamu inaitwa Medical Consultation ambayo mswahili anaita kumwona (to see) daktari. Hatua hii muhimu ndiyo inalipiwa shillingi elfu kumi kama daktari ni wa kawaida (medical officer) au elfu thelathini kama daktari ni daktari bingwa. Pesa hii ni ya hospitali, si kwamba atapewa huyo daktari. Ni pesa ya serikali. Pesa ya daktari ni huo mshahara wake tu. Serikali inakusanya pesa yake kwenye kila mchakato huo wa tiba ie kwenye usajili, medical consultation, maabara, mionzi, upasuaji, dawa, kulala hospitalini, kulala mortuary, na kadhalika. Jumla ya gharama kwa mgonjwa inaweza kuwa mamillioni ya pesa kama tatizo la mgonjwa ni kubwa. Pesa hiyo yote ni ya serikali na hutumika kugharimia huduma hiyo ya afya.

BADALA YA KULALAMIKA WANANCHI WAELIMISHWE KUJIUNGA NA MFUKO WA BIMA YA AFYA WA TAIFA. NCHI ZOTE ZILIZOENDELEA ZINAFANYA HIVYO, HAZITOI TIBA BURE BURE. SISI TUTAWEZA VIPI KUTOA TIBA BURE?
Hata bima ya afya bado kumuona dakitari utalipa, kwanini wakati yeye ni mtumishi wa umma na bajeti yake kuwepo hapo hupangwa na bunge! Hakuna sababu kulipia daktari wala kadi.
 
Umeme, maji, majengo, mishahara na gharama zote za uendeshaji fedha hutoka serikalini wakati wa bajeti.
Na serikali hupata pesa hiyo ya kugharimia huduma hizo kutoka kwenye kodi za umeme, maji, majengo, mishahara, biashara, tiba na kadhalika. Serikali haifyatui tu mapesa.
 
Hata bima ya afya bado kumuona dakitari utalipa, kwanini wakati yeye ni mtumishi was umma na bajeti yake kuwepo hapo hupangwa na bunge! Hakuna sababu kulipia daktari wala kadi.
Nimekuambia hiyo hela si ya daktari. Mbona huelewi? Rudia kusoma nilichoandika.
 
1. Dawa/tiba ni mahitaji ya kawaida na ya lazima kwa binadamu kama ilivyo chakula. Gharama yake kwa wastani yanalingana na gharama ya chakula kwa mwaka. Hivyo kama ilivyo ukweli kwamba serikali haiwezi kuwapa chakula bure wananchi wake, ndivyo ilivyo kwamba serikali haiwezi kuwapa dawa/tiba bure wananchi wake. Usitake kulinganisha gharama ya kutoa elimu bure (shillingi billioni 20 kwa mwezi) na dawa/tiba bure (shillingi trillion 30 kwa mwaka = bajeti nzima ya mwaka).

2. Ili mgonjwa aweze kupata tiba sahihi lazima apitie hatua kadhaa za mchakato (process) au mkondo wa kitaaluma ambao ni standard (wa kimataifa). Mgonjwa hulipia kila hatua ya mchakato huo.

3. Hatua ya kwanza lazima asajiliwe. Akishasajiliwa anapewa kadi kama mfumo wa usajili ni manual (wa makaratasi). Siku hizi mfumo wa usajili katika hospitali nyingi ni wa ki electronic unaotumia komputa. Mfumo huu hauna kadi au makaratasi yo yote: mgonjwa anaingizwa kwenye system ya hospitali. Analipia ada ya kujisajili. Si kwamba analipia gharama ya kuchapisha karatasi ya kadi.

3. Hatua ya pili ni mgonjwa kuonana na daktari ambapo ataeleza matatizo yake yote ya kiafya. Daktari atamsikiliza, atamhoji mambo fulani fulani ili kupata picha halisi ya matatizo ya mgonjwa (kwa kitaalamu inaitwa history). Baada ya hapo daktari atapima mwili wa mgonjwa wake: kwa kuuangalia kwa macho, kuupapasa papasa kwa mikono na vidole nje na ndani kupitia matundu mbali mbali ya mwili, na kusikiliza milindimo mbali mbali ndani na nje ya mwili huo. Hii kwa kitaalamu inaitwa physical examination. Baada ya daktari kupata history na physical examination, daktari atafanya majumuisho na uchambuzi wa kina wa kitaalamu (clinical analysis) na kufanya maamuzi (clinical descion) ya hatua gani zingine zifuate na mpangilio wa hatua hizo. Hatua hizo zingine zinaweza zikawa za maabara, za kiradiolojia, za upasuaji, za madawa, mionzi, physiotherapy na kadhalika.

Hiyo hatua ya history, physical examination, clinical analysis hadi clinical descion ndiyo kwa kitaalamu inaitwa Medical Consultation ambayo mswahili anaita kumwona (to see) daktari. Hatua hii muhimu ndiyo inalipiwa shillingi elfu kumi kama daktari ni wa kawaida (medical officer) au elfu thelathini kama daktari ni daktari bingwa. Pesa hii ni ya hospitali, si kwamba atapewa huyo daktari. Ni pesa ya serikali. Pesa ya daktari ni huo mshahara wake tu. Serikali inakusanya pesa yake kwenye kila mchakato huo wa tiba ie kwenye usajili, medical consultation, maabara, mionzi, upasuaji, dawa, kulala hospitalini, kulala mortuary, na kadhalika. Jumla ya gharama kwa mgonjwa inaweza kuwa mamillioni ya pesa kama tatizo la mgonjwa ni kubwa. Pesa hiyo yote ni ya serikali na hutumika kugharimia huduma hiyo ya afya.

BADALA YA KULALAMIKA, WANANCHI WAELIMISHWE KUJIUNGA NA MFUKO WA BIMA YA AFYA WA TAIFA. NCHI ZOTE ZILIZOENDELEA ZINAFANYA HIVYO, HAZITOI TIBA BURE BURE. SISI TUTAWEZA VIPI KUTOA TIBA BURE?
Kwa utaratibu uliosema basi hospitali zisipewe pesa za bajeti, zijitegemee. Hakuna sababu tumlipe mshahara halafu tulips kumuona, hospitali za praiveti hazina hii kitu wao pesa unayolipa ndiyo itakwenda kwenye mshahara wake, fullstop.
 
Ukienda hospttali utaliapia gharama za matibabu mfano dawa na procedures mbalimbali ikiwamo na operation na vipimo mbalimbali .Mfano kama hukuitajika kufanyiwa vipimo ,procedure yoyote au kupewa dawa Ila daktari alikupa ushauri wa kitaalam kama ndiyo tiba yako yaani consultation je hupasi kulipia huo ushauri ? Sidhani consultation fee ni kwaajili ya kulipia karatasi au kufungulia file ,kupata ushauri wa kitaalam ni huduma hivyo kulipia siyo kosa .Malipo kwa Huduma ktk hospitality za zerikali ni cost sharing ndiyo maana zipo chini kulinganisha na uhasilia wa gharma yenyewe kama mgonjwa anashindwa hizo gharama upo utaratibu wa kupatasamaha wa matibabu ila tatizo wahudumu wa afya wanashindwa kutoa Maelezo kwa mgonjwa jinsi ya kupata Huduma hiyo bila malipa labda kwa kutokujua au makusudi au jamii wanaweza kutumia vibaya fursa hiyo .Pia kunamakundi serikali imewapa msamaha wa matibabu kama utafanya utafiti utagundua makundi haya ya msamaha ndiyo yenye gharama kubwa sana serikali ktk kuwagharamia ,mfano wa makundi hayo ni wazee zaidi ya miaka sitini,watoto chini ya miaka mitano mama mjamzito,wenye magonjwa sugu na baadhi ya walemavu hawa wanapewa Huduma bure .Mimi siyoni shida kuchangia Huduma za afya kama zitatolewa kwa ubora wake .Kuhusu kodi ni kuwaomba viongozi wetu waisimamie vizuri urudi kwa wananchi ktk mfumo wa Huduma iliyobora hii itasaidia wananchi kuhamasika ktk kulipia kodi na wala hatutasikia mwananchi anakwepa kulipa kodi ,lkn kama tutaona wabunge mawaziri wanashindana kutembelea magari ya gharama kubwa na mishahara minono huku Huduma za jamii zimezorota niwazi wananchi tutalalamika hadi kupitiliza .Wito hicho kidogo kinachokusanywa kifike kwa walipa kodi.Rasilimali tulizonazo zinufaishe taifa zima isiwe kwa kikundi cha watu wachache
 
Hospitali za serikali zimeweka mabango makubwa yakionesha gharama za tiba, gharama hizo zinaashiria kuwa serikali imejitoa kwenye huduma ya tiba kwa wananchi wake.

Moja ya jambo ambalo sikubaliani nalo ni malipo ya kumuona mganga ambaye no mwajiriwa wa serikali kama walivyo waajiriwa wengine, mahakimu, wakuu wa mikoa na wilaya, wabunge,mawaziri na wengine wengi ambao tunagharamia mishahara yao, kwanini waganga tuwagharamie mara mbili! Kupitia mishahara ambayo ni kodi zetu na pesa taslimu kupitia hospitali! Hii siyo sahihi.

Jambo jingine, kwanini tulipie karatasi za kujiandikisha (kadi)! Hizi zinanunuliwa kutokana na kodi zetu, mbona TRA, jiji, biashara na kwingineko hatulipii? Ninadhani gharama hizi zimepangwa kwa kufananisha na hospitali binafsi.

Mwisho, serikali inatakiwa iwe na sera ya afya kwa wananchi badala ya kutumia sera ya chama kwani kitakachotokea sasa ni wananchi kushindwa kumudu gharama za tiba na kutumbukia kwenye vikombe vya babu jambo litakaloleta usugu wa maradhi, pia kuwatelekeza wagonjwa waliolazwa kwa kushindwa kulipa deni la tiba na kususa kuchukua maiti kutokana na gharama za mochwari.

Sijui uchumi utakuwaje kwenye taifa la wagonjwa! Tuachane na mtindo wa sera za vyama tuwe na sera za taifa ingawa vyama tawala havipendi kwani vinataka vionekane vimeleta maendeleo matokeo huwa havifanikiwi.
Cheza na vingine lakini sio Afya!
 
Write your reply...Hana habari kama tupo kwenye mageuzi ya kimaisha.
 
Ukienda hospttali utaliapia gharama za matibabu mfano dawa na procedures mbalimbali ikiwamo na operation na vipimo mbalimbali .Mfano kama hukuitajika kufanyiwa vipimo ,procedure yoyote au kupewa dawa Ila daktari alikupa ushauri wa kitaalam kama ndiyo tiba yako yaani consultation je hupasi kulipia huo ushauri ? Sidhani consultation fee ni kwaajili ya kulipia karatasi au kufungulia file ,kupata ushauri wa kitaalam ni huduma hivyo kulipia siyo kosa .Malipo kwa Huduma ktk hospitality za zerikali ni cost sharing ndiyo maana zipo chini kulinganisha na uhasilia wa gharma yenyewe kama mgonjwa anashindwa hizo gharama upo utaratibu wa kupatasamaha wa matibabu ila tatizo wahudumu wa afya wanashindwa kutoa Maelezo kwa mgonjwa jinsi ya kupata Huduma hiyo bila malipa labda kwa kutokujua au makusudi au jamii wanaweza kutumia vibaya fursa hiyo .Pia kunamakundi serikali imewapa msamaha wa matibabu kama utafanya utafiti utagundua makundi haya ya msamaha ndiyo yenye gharama kubwa sana serikali ktk kuwagharamia ,mfano wa makundi hayo ni wazee zaidi ya miaka sitini,watoto chini ya miaka mitano mama mjamzito,wenye magonjwa sugu na baadhi ya walemavu hawa wanapewa Huduma bure .Mimi siyoni shida kuchangia Huduma za afya kama zitatolewa kwa ubora wake .Kuhusu kodi ni kuwaomba viongozi wetu waisimamie vizuri urudi kwa wananchi ktk mfumo wa Huduma iliyobora hii itasaidia wananchi kuhamasika ktk kulipia kodi na wala hatutasikia mwananchi anakwepa kulipa kodi ,lkn kama tutaona wabunge mawaziri wanashindana kutembelea magari ya gharama kubwa na mishahara minono huku Huduma za jamii zimezorota niwazi wananchi tutalalamika hadi kupitiliza .Wito hicho kidogo kinachokusanywa kifike kwa walipa kodi.Rasilimali tulizonazo zinufaishe taifa zima isiwe kwa kikundi cha watu wachache
Hapa nieleze dhuluma niliyowahi kupata Muhimbili, nilimpeleka binti yangu kitengo cha koo ambapo siku ya kwanza nililipa zaidi ya shilingi elfu kumi na tano, walimtazama koo na kutuambia turudi wiki inayofuata ambapo tulitimiza na tukalipa tena pesa kama zile na kuambiwa turudi tena na kulipa tena. Mara zote hizo tatu kilichofanyika ni kumtaka afungue mdomo daktari anachungulia ndani ya koo kisha kumuambia afunge mdomo bila ya kufanya kitu chochote! Hivi kumchungulia mtu kooni kunagharimu kiasi hicho? Easy money! Pesa bila jasho. Baada ya malipo ya tatu niliamua kuachana nao niliingizwa mjini. Hospitali za binafsi hata kama hawakutibu angalau watakudanganya kwa tiba feki. Baadhi ya malipo yaondolewe kwani yanafanyika mara mbili, moja kupitia kodi zetu.
 
Nani anakumbuka manifesto ya CCM kwenye sera za Afya 2015?
 
Back
Top Bottom