Ni simple na yenye muelekeo wa uhalisia yaani kuhakikisha jamii inaunganishwa na mfuko wa bima ya afya.Nani anakumbuka manifesto ya CCM kwenye sera za Afya 2015?
Hivi elfu 10 yako ndio inaweza kulipia mshahara wa daktari?Kwa utaratibu uliosema basi hospitali zisipewe pesa za bajeti, zijitegemee. Hakuna sababu tumlipe mshahara halafu tulips kumuona, hospitali za praiveti hazina hii kitu wao pesa unayolipa ndiyo itakwenda kwenye mshahara wake, fullstop.
Sion tatzo kwa hospital kuweka mabango ya gharama kwa sababu inaonesha hospital saivi zinatakiwa kujiendesha kwa mapato yake kwa baadhi ya mahitaji muhimu kama umeme, dawa n.k
Ni jukumu la serikali kutamka wazi kuwa tumeshatoka kwenye mfumo wa ujamaa ambapo serikali ilikuwa ikigharamia social services na kuhimiza kila mwananchi kujiunga na huduma ya bima na wale wasio na uwezo serikali iwalipie kwa mfuko maalum wa afya kwa wote! Hii itapunguza watu kwenda kwa sangoma na matapeli kina Dr. Mwaka na pia itaboresha huduma hospitaln kwa sababu hospital zitaweza kujiendesha kwa kuwa na uhakika na vyanzo vya uhakika.
Bima iwe universal(kila mmoja) na iwe rahisi kwa kila mwananchi kwa mfano kila mwenye leseni ya biashara alipe elfu hamsini n.k
Serikali iajiri wataalam wa afya wenye ujuzi na kwa sababu kila mtu atakuwa na bima watumishi hawa wataweza kulipwa mishahara na posho husika. Pia sioni mantiki ya hospital za mikoana wilaya kuwa na clinical officers hawa wapelekwe kuanzia ngaz za vituo vya afya kurud chini huku kukifanyika utaratib wa kuifuta fani hii isiyokuwepo baadhi ya nchi.
Mwisho serikali ibadili sera ili kuweza ku retain brains(hii sio katik sekta ya afya pekee) kwa kutoa competitive salaries and incentives. Wale watu wanaomfuata daktari mzuri private wamfuate hospital ya serikal ili kuongeza mapato serikalini, hili linawezekana kwa kuboresha maslahi na kulipa incentives km performance related bonuses n.k
Naona unaongea bila kufanya utafiti,na labda wewe una huduma ya afya ndiyo maana unaongea juu ya wazee,kwamba hawalipii walemavu nk.Ukienda hospttali utaliapia gharama za matibabu mfano dawa na procedures mbalimbali ikiwamo na operation na vipimo mbalimbali .Mfano kama hukuitajika kufanyiwa vipimo ,procedure yoyote au kupewa dawa Ila daktari alikupa ushauri wa kitaalam kama ndiyo tiba yako yaani consultation je hupasi kulipia huo ushauri ? Sidhani consultation fee ni kwaajili ya kulipia karatasi au kufungulia file ,kupata ushauri wa kitaalam ni huduma hivyo kulipia siyo kosa .Malipo kwa Huduma ktk hospitality za zerikali ni cost sharing ndiyo maana zipo chini kulinganisha na uhasilia wa gharma yenyewe kama mgonjwa anashindwa hizo gharama upo utaratibu wa kupatasamaha wa matibabu ila tatizo wahudumu wa afya wanashindwa kutoa Maelezo kwa mgonjwa jinsi ya kupata Huduma hiyo bila malipa labda kwa kutokujua au makusudi au jamii wanaweza kutumia vibaya fursa hiyo .Pia kunamakundi serikali imewapa msamaha wa matibabu kama utafanya utafiti utagundua makundi haya ya msamaha ndiyo yenye gharama kubwa sana serikali ktk kuwagharamia ,mfano wa makundi hayo ni wazee zaidi ya miaka sitini,watoto chini ya miaka mitano mama mjamzito,wenye magonjwa sugu na baadhi ya walemavu hawa wanapewa Huduma bure .Mimi siyoni shida kuchangia Huduma za afya kama zitatolewa kwa ubora wake .Kuhusu kodi ni kuwaomba viongozi wetu waisimamie vizuri urudi kwa wananchi ktk mfumo wa Huduma iliyobora hii itasaidia wananchi kuhamasika ktk kulipia kodi na wala hatutasikia mwananchi anakwepa kulipa kodi ,lkn kama tutaona wabunge mawaziri wanashindana kutembelea magari ya gharama kubwa na mishahara minono huku Huduma za jamii zimezorota niwazi wananchi tutalalamika hadi kupitiliza .Wito hicho kidogo kinachokusanywa kifike kwa walipa kodi.Rasilimali tulizonazo zinufaishe taifa zima isiwe kwa kikundi cha watu wachache