Malipo ya kisasi ni kisu au risasi

Malipo ya kisasi ni kisu au risasi

nzala_kv

New Member
Joined
May 28, 2025
Posts
4
Reaction score
3
Katika maisha haya tunayoyaishi hapa Duniani Kila bin Adam ni Safi kabisa iwapo tungekuwa hatukutani na binadamu wengine.

Ila kwa sababu tunakutana Sina budi kusema 'The atmosphere is no longer the same'. Na hii kwa sababu katika kukutana kwetu tunakoseana sana.

Na siku zote bin Adam ndiyo hufanya bin Adam wenziye waonekane wabaya. Maana wanapowakosea bin Adam wenzao huweka fikra za kuweza kulipiza kisasi na hata pale wanapowakosa wale waliowakosea,mtu yeyote atakayepita mbele yake huwa ni mkosaji kwake na hulipiza kisasi. Na huo ndiyo 'mwanzo wa ubaya'.

Katika maisha yangu nilishafanikiwa kukutanana au kushuhudia watu kadhaa waliowahi kunikosea lakini pia wapo wanaoendelea kunikosea. Na nilishawahi kuwa mlipaji kisasi mzuri tu lakini ilifika wakati baada ya kukua vema na kuwa timamu yaani 'Highly Maturity Level' nilijikuta hii hali ya ulipizaji kisasi si sawa na haileti Afya kwa ustawi wa Jamii,sababu mwisho wa siku hata Mimi ni mkosaji kwa wengine. Mimi si mkamilifu. Pia kupitia ulipizaji kisasi ni kukosea.

Hekima, busara na upendo vilianza kunijaa japo 'tabia ni kama ngozi' lakini mpaka wale wakosaji wangu walianza kubadilika nao kupitia mfumo mpya wa maisha niliyojijengea kupitia kauli mbiu Moja isemayo;-

Katika Dunia hii ukichukulia Kila jambo kwa uzito mwishowe utajikuta una mzigo mkubwa wa Mambo tatizi unayopaswa kuyatafutia utatuzi/suluhu.

Kulipa kisasi ni nia ovu na ni nia ya kizembe, pia ni sawa mtukana jembe kumbe kwao ndiyo wale vijino pembe maisha yao yatakuwa ni sawa na 'urafiki gani!,kati ya fimbo na ng'ombe?'.
Ni nini nataka kusema,ni hivi tusitafute suluhu katika Mambo tatizi kwa kutumia hisia sababu hisia zitakufanya ushindwe kutulia na kukufanya usipate tafakuri zenye Afya.
Aksante kwa kuzingatia kwako. 🤝🏿

NB: Siku zote watu wema hushangilia na watu wabaya hutamani kulia kwa uchungu.
 
"mtukana jembe kumbe kwao ndiyo wale vijino pembe"........Naona Imekuwia Vema Kutusuta??
 
"mtukana jembe kumbe kwao ndiyo wale vijino pembe"........Naona Imekuwia Vema Kutusuta??
Mkuu halikuwa lengo ila wakati mwingine ili watu wakuelewe ni muhimu kuambatanisha andiko na vionjo vya namna hiyo.

Niwie radhi kama imekuwa kero.
Ahsante.
 
Back
Top Bottom