Malinyi Ulanga: Mauaji katika mapambano ya jeshi la polisi na wakulima

Nadhani ipo haja ukafikiri upya mimi kwa mtazamo wangu huyu wanaemwita chagonja huyu mzee huyu atakuwa anaitendea haki nafasi yake kwani katika matukio kama haya yanapotokea mara nyingi mafanikio yanapatikana kwani hadi sasa katika hayo matukio ambayo umejaribu jaribu kuyaelezea kwasasa si dhani kama kunamachafuko ama matukio ya aina hiyo yakiendelea lakini pia nataka kumwambia mtoa mada hakuna askari Polisi aliyeuawa rudia tena hakuna askari aliyeuawa katika tukio hilo la jaribio la kuvamia kituo.
 
Hivi huyu Chagonja ana mafanikio gani toka aanze kutumwa maeneo ya matatizo..? Walipouawa raia Songea alienda.. Alipouawa Mwangosi Iringa alikwenda.. Arusha akaenda.. Na sasa huko Malinyi..! Ataenda mikoa yote maana wananchi wengi wameamka na kujua haki zao.. watakapoendelea kuhisi wananyimwa haki zao watageukia kwenye vurugu.. Ufumbuzi wa pekee ni kwa serikali kusimamia haki bila ya upendeleo..

Haki yao ndio kumtoa mtuhumiwa wa mauaji kituo cha polisi kwa nguvu? Fikiri vizuri wewe!
 
Hawa polisi jamani wanashindwa kudhibiti raia pasipo kuua?

Hivi umesoma vizuri huo uzi? Umeambiwa polisi wametumia kila njia ya kuwaambia watu watawanyike,wakagoma, wakatumia mabomu ya machozi, lakini wapi! Hatimaye wakazingira kituo na kukichoma moto na gari pia! Sasa ulitakaje? Wakae tu nao wauawe? Acha ushabiki!
 
walitumiwa kisiasa huko nyuma, sasa mambo yanawageuka...waliwasha moto wenyewe (ccm na serikali yake) sasa wameshindwa kuuzima

Unavyoongea kana kwamba hali hii haiwezi kukuta hata wewe! Hapa ishu ni kukemea mambo ya kujichukulia sheria mkononi basi.
 
Haki yao ndio kumtoa mtuhumiwa wa mauaji kituo cha polisi kwa nguvu? Fikiri vizuri wewe!

Ungeshirikisha ubongo wako wala usingeijibu hiyo comment.. Ila kwa kuwa kichwani una ubongo wa ndezi nitakusaidia kidogo hata kama utaendelea kuwa mbishi..

Ataenda mikoa yote maana wananchi wengi wameamka na kujua haki zao.. watakapoendelea kuhisi wananyimwa haki zao watageukia kwenye vurugu

soma vizuri hiyo quote hapo.. I dont condone violence lakini inapofika wakati kundi moja likihisi haki yao inaporwa na hakuna hatua zozote za makusudi zinafanywa kuwatetea zaidi ya kukandamizwa ndo wanaingia kwenye vurugu.. Vurugu zitapelekea mauaji na uharibifu wa mali lakin kikubwa zaidi ni tatizo kupata attention kubwa ambayo itawaamsha watawala waliolala.. Siku zote tumesikia kilio cha wakulima wakidai wafugaji wanapendelewa pamoja na kuleta uharibifu kwenye mashamba ya wakulima.. Serikali yako sikivu ilichukua hatua gani..? Acha hizo usilete siasa kwenye maisha ya watu..
 
Back
Top Bottom