Malinyi Ulanga: Mauaji katika mapambano ya jeshi la polisi na wakulima

FDR.Jr

JF-Expert Member
Jun 17, 2008
1,356
1,500
Wiki hii kumetokea mgogoro kati ya wafugaji(Wasukuma) na wananchi wa Igawa-Malinyi; chanzo cha mgogoro huu mpya ni watumishi wetu wa vyombo vya ulinzi na usalama kukiuka maadili ya kutunza identity ya mtoa taarifa/chanzo cha habari.

Tangu mwaka jana kule Ulanga Magharib kulikuwa na zoezi la kuwaondoa wafugaji na kuhakikisha kilakaya inabaki na mifugo yenye idadi ndogo na isiyo na madhara ktk kilimo; eneo la Ulanga Magharibi si eneo la ufugaji bali kilimo....

Kuna mwananchi alitoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuwa licha ya zoezi hili la kuondoa mifugo kuonekana limekamilika lakini bado kuna wafugaji wamehodhi mifugo mingi mno ktk eneo lao....jamaa wa usalama wakarejesha habari kwa wafugaji...

Ijumaa kuamkia Jmosi usiku wafugaji wakamvamia mtoa taarifa na kumuua .....kitendo hicho kikaamsha hasira ya wakulima na wananchi wa Igawa wakawasaka waliohusika na kumpata mmoja wao ambae alikiri kuhusika na jinsi walivyoarifiwa juu ya mtoa habari...kwa bahati mbaya sana wana Igawa kwa uzembe wakamchoma moto Mfugaji yule baada ya kukiri...

Juzi Mkuu wa Wilaya ya Ulanga amabaye naye anatuhumiwa kuwa ni chanzo na msingi wa tatizo hili alikwenda Malinyi Igawa na kuongea na wafugajikwa faragha kisha akaja kuongea na wana Malinyi akikemea hulka za kujichukulia sheria mikononi mwao...akawaambia midhali kila upande umejitwalia sheria mkononi basi anaomba hali hiyoiishe na isijirudie....

Jana akaleta askari na kuwakamata wananchi wanaohisiwa kumchoma moto mfugaji na kuwatupa selo jambo liliowaudhi wananchi wa Igawa ambao tangu jana walimtaka awaachie huru kama alivyowaacha wafugaji....

Leo asubuhi wamevamia kituo cha polisi tarafa ya Malinyi wamekipiga moto, wamewatoa mahabusu wote lakini kuna madhara yamejitokeza ktk vurugu hizo...risasi za moto toka polisi zimetumika na kuna watu takribani watatu wanahisiwa kufa au kujeruhiwa hapo polisi Malinyi....

Tunatoa wito kwa serikali na viongozi wa jamii kulimaliza tatizo hili haraka ili kuepusha umwagaji mkubwa wa damu.

Media houses tusaidieni kuweka wazi undani wa sakata hili ambao tangu 2011 umekuwa ukichukua uhai wa wananchi, jiridhisheni kwa taarifa kwa kuwasiliana na Mh. Mbunge Hajj Mponda na diwani wa Malinyi Mh.Tira 0755397467

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Iponye Malinyi....
 
white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
6,573
2,000
Tatizo kubwa la hii migogoro baina ya wakulima na wafugaji kamwe haiwezi kuisha kwani viongozi ndio wameigeuza vitega uchumi vyao, na hasa upande wa wafugaji wamegeuzwa deal na ndio maana wakulima wanaonewa kwani wanakuwa hawana pa kukimbilia kwani ma OCD wote wako mifukoni mwa wafugaji,na ole wako mfugaji auwawe!hata polisi wa vyeo vya chini wana kili kabisa kuwa hata wao huwa wana hatalishiwa maisha yao kwenda kutuliza vurugu ambazo chanzo ni viongozi wao,.Ila wakulima wanapoamua kuchoma kituo cha polisi kidogo huwa ina tia adabu mfano pale IKWIRIRI baada ya kuchoma kituo cha polisi hadi leo heshima ipo.
 
mgemamkwezi

JF-Expert Member
Oct 11, 2013
445
0
Huyu mkuu wa wilaya anaonekana kuwa mla rushwa kama walivyo wengi katika wilaya zenye matatizo kama hayo,rushwa ni chanda na pete kwa voingozi wa CCM, matatizo ya watanzania hayatakwisha bila magamba kung'oka madarakani
 
Lua

JF-Expert Member
May 19, 2011
704
0
Muda huu nimepata meseji na kupigiwa simu kutoka kwa mkazi aliyopo Ifakara kuwa muda huu kuna mapambano makali kati ya polisi na wakulima katika tarafa ya Malinyi-jimbo la Ulanga Magharibi.

Hii ni kutokana na mgogogro wa uliotokana na mifugo kuingia kwenye mashamba ya wakulima na kufanya uhalibifu mkubwa wa mashamba ya wakulima.

Taarifa za awali zinasema kutoka na hilo ilipelekea mwenyekiti wa kijiji kupoteza maisha na wanakijiji nao kwenda kulipa kisasi kwa kumpiga mfugaji hadi kumsababishia kifo.

Baada ya hapo polisi wakaingilia kati na sasa ivi mapambano yanaendelea na taarifa sio rasmi watu watano wameshapoteza maisha katika mapambano hayo.
Wiki hii kumetokea mgogoro kati ya wafugaji(Wasukuma) na wananchi wa Igawa-Malinyi; chanzo cha mgogoro huu mpya ni watumishi wetu wa vyombo vya ulinzi na usalama kukiuka maadili ya kutunza identity ya mtoa taarifa/chanzo cha habari.

Tangu mwaka jana kule Ulanga Magharib kulikuwa na zoezi la kuwaondoa wafugaji na kuhakikisha kilakaya inabaki na mifugo yenye idadi ndogo na isiyo na madhara ktk kilimo; eneo la Ulanga Magharibi si eneo la ufugaji bali kilimo....

Kuna mwananchi alitoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuwa licha ya zoezi hili la kuondoa mifugo kuonekana limekamilika lakini bado kuna wafugaji wamehodhi mifugo mingi mno ktk eneo lao....jamaa wa usalama wakarejesha habari kwa wafugaji...

Ijumaa kuamkia Jmosi usiku wafugaji wakamvamia mtoa taarifa na kumuua .....kitendo hicho kikaamsha hasira ya wakulima na wananchi wa Igawa wakawasaka waliohusika na kumpata mmoja wao ambae alikiri kuhusika na jinsi walivyoarifiwa juu ya mtoa habari...kwa bahati mbaya sana wana Igawa kwa uzembe wakamchoma moto Mfugaji yule baada ya kukiri...

Juzi Mkuu wa Wilaya ya Ulanga amabaye naye anatuhumiwa kuwa ni chanzo na msingi wa tatizo hili alikwenda Malinyi Igawa na kuongea na wafugajikwa faragha kisha akaja kuongea na wana Malinyi akikemea hulka za kujichukulia sheria mikononi mwao...akawaambia midhali kila upande umejitwalia sheria mkononi basi anaomba hali hiyoiishe na isijirudie....

Jana akaleta askari na kuwakamata wananchi wanaohisiwa kumchoma moto mfugaji na kuwatupa selo jambo liliowaudhi wananchi wa Igawa ambao tangu jana walimtaka awaachie huru kama alivyowaacha wafugaji....

Leo asubuhi wamevamia kituo cha polisi tarafa ya Malinyi wamekipiga moto, wamewatoa mahabusu wote lakini kuna madhara yamejitokeza ktk vurugu hizo...risasi za moto toka polisi zimetumika na kuna watu takribani watatu wanahisiwa kufa au kujeruhiwa hapo polisi Malinyi....

Tunatoa wito kwa serikali na viongozi wa jamii kulimaliza tatizo hili haraka ili kuepusha umwagaji mkubwa wa damu.

Media houses tusaidieni kuweka wazi undani wa sakata hili ambao tangu 2011 umekuwa ukichukua uhai wa wananchi, jiridhisheni kwa taarifa kwa kuwasiliana na Mh. Mbunge Hajj Mponda na diwani wa Malinyi Mh.Tira 0755397467

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Iponye Malinyi....
 
Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
2,435
2,000
Nchi hii kila kitu siasa, na kwa sababu hiyo siasa imeua kila kitu. Wafugaji ni wachokozi. Kwa asili wana maeneo yao. Wameyaharibu na kuamua kwenda kwa wakulima. Wakulima wanapolalamika wanaambiwa kila Mtanzania ana haki ya kuishi anakotaka alimradi havunji sheria. Wafugaji wanavunja sheria. Wanaingiza mifugo kwenye mashamba, lakini wanasiasa na mapolisi wamekuwa wakiwabeba wafugaji kwa sababu wana fedha za kuwapa. Mkulima hawezi kumhonga OCD wala DC kwa sababu watawala hao hawana ujasiri wa kusubiri mahindi yakomae, yauzwe ili waweze kuwapa rushwa.

TUnapaswa kuondoa siasa za kubebana kwenye suala hili. Mauaji makubwa sana yanakuja Tanzania. Mfano wa juzi wa KIsesa ni mdogo tu. makubwa yanakuja. Amina naambia, sioni Tanzania yenye amani huko tunakoelekea.
 
FDR.Jr

JF-Expert Member
Jun 17, 2008
1,356
1,500
[h=5]Ramadhan KidesuWANA MDC-MALINYI-ULANGA-KILOMBERO
[/h]ASUBUHI HII
Wandamba wa vijiji vya ngombo,biro,igawa na lugala wameandamana hadi kituo cha polisi kuja kudai kuachiwa kwa ndugu zao waliokamatwa kuanzia jana usiku na leo asubuhi kuachiwa huru baada ya kufika kituoni hapo polisi walianza kufyatua risasi hewan na baadae waliwafyatulia wananchi na kupiga vijana wapatao 6 na kuwaua palepale hali iliyopelekea wandamba kuchoma moto kituo,magari ya askari,nyumba ya mkuu wa kituo nk hali ni mbaya sana
Like · · 35 minutes ago ·

 • Ramadhan Kidesu likes this.
 • Malinyileo Blogspot Ni hatari sana
  16 minutes ago · Like

 • Diantermo Makolela Mmmh! kisa?
  14 minutes ago via mobile · Like

 • Goldengirl Gulamali Sawa yaani hakukaliki hakupitiki hali ni mbaya sana jamani serikali mko wapi wananchi wanakwisha Malinyi jamani kama tuko Sudani
  14 minutes ago via mobile · Like

 • 203197_100004630294004_345493346_q.jpg

  Write a comment... 

FDR.Jr

JF-Expert Member
Jun 17, 2008
1,356
1,500 • Ramadhan Kidesu vurugu zilianza wiki iliyopita baada ya wasukuma kumuua mwenyekiti wa mazingira wa kijiji kwa madai ya kwamba anawazunguka anawaomba rushwa ili awafiche porini wasifukuzwe na mifugo yao huku akiwaonyesha polisi wakawakamate.baada ya mauaji hayo ya mndamba yaliyofanyika saa 6 mchana wandamba wakaanza kuchoma moto nyumba za wasukuma na kuua kila msukuma wanaekutana nae njiani. Kisa #2 refer status
  5 minutes ago via mobile · Like
 
mgemamkwezi

JF-Expert Member
Oct 11, 2013
445
0
Nasikia kuna mkuu wa wilaya ya Kinondoni Lugimbane naye anakuza na kula mirungura na kukuza migogoro Kinondon, amewapa eneo mafundi gereji kule tegeta wafanyie kazi zao baadaye akauza eneo hilo kwa wahindi na sasa hivi kawageuka mafundi zaidi ya 2000 na anataka kuwavunjia majengo yao, magamba bwana sasa yamefika pabaya kila mmoja anawahi kilicho karibu yake hata kwa kupora
 
TAWA

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,663
2,000
tulia, kama unaenda chooni nenda alafu ndo uandike, haraka ya nini? stori haipo hivyo. mods unganisheni hii thread na ile ya mwanzo ya FDR jr
 
Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,403
2,000
Migogoro ya ardhi Tanzania imemshinda Dr Kikwete, tutegemee damu za watu kuendelea kumwagika kutokana na serikali dhaifu.

Poleni wafiwa, tambueni kuwa CCM imepoteza uhalali wa kuongoza kwa kushindwa kutatua kero zetu. Wanashindwa kununua dawa hospitalini, hata kutatua kero za ardhi wanashindwa?
 
FDR.Jr

JF-Expert Member
Jun 17, 2008
1,356
1,500
Nchi hii kila kitu siasa, na kwa sababu hiyo siasa imeua kila kitu. Wafugaji ni wachokozi. Kwa asili wana maeneo yao. Wameyaharibu na kuamua kwenda kwa wakulima. Wakulima wanapolalamika wanaambiwa kila Mtanzania ana haki ya kuishi anakotaka alimradi havunji sheria. Wafugaji wanavunja sheria. Wanaingiza mifugo kwenye mashamba, lakini wanasiasa na mapolisi wamekuwa wakiwabeba wafugaji kwa sababu wana fedha za kuwapa. Mkulima hawezi kumhonga OCD wala DC kwa sababu watawala hao hawana ujasiri wa kusubiri mahindi yakomae, yauzwe ili waweze kuwapa rushwa.

TUnapaswa kuondoa siasa za kubebana kwenye suala hili. Mauaji makubwa sana yanakuja Tanzania. Mfano wa juzi wa KIsesa ni mdogo tu. makubwa yanakuja. Amina naambia, sioni Tanzania yenye amani huko tunakoelekea.

Manyerere uko 110% sahihi....huyu DC. Mitti ni mpalia bustani aliyoiasisi RC. Rutengwe akiwa Ulanga kama DC....., hali ni mbaya sana mpaka muda huu tunakandamiza keyboard zetu...

Ongea na Diwani huyu 0755397467 mpigie Mh. Mponda na ulifanyie kazi hili jambo anza na Malinyi, anza na DC Francis Mitti anza na OCD na DSO anza na PCCB Ulanga hapo utapata ukweli juu ya mzizi wa haya yote....

Ninyi watu wa Media hapa hampaswi ku balance story ...wekeni mchele pembeni na pumba pembeni....
 
Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,522
2,000
Migogoro ya ardhi Tanzania imemshinda Dr Kikwete, tutegemee damu za watu kuendelea kumwagika kutokana na serikali dhaifu.

Poleni wafiwa, tambueni kuwa CCM imepoteza uhalali wa kuongoza kwa kushindwa kutatua kero zetu. Wanashindwa kununua dawa hospitalini, hata kutatua kero za ardhi wanashindwa?

Jk ndo muasisi wa migogoro ya ardhi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom