Malinyi Ulanga: Mauaji katika mapambano ya jeshi la polisi na wakulima

Pompo, usinishambulie kwa hoja nyepesi. Haya mambo sikuanza kuyajua leo. Tangu zama zile za Kilosa, suala la rushwa liko wazi. Rushwa na siasa ni kulwa na dotto. Nikupe mfano mzuri tu. Pale Loliondo suala la matumizi bora ya ardhi lilishaainishwa na kamati zaidi ya nne. Kulianishwa wapi wafugaji wapeleke mifugo, wapi wanyamapori walishe na wapi shughuli za kilimo zifanywe. Kilichotokea baada ya hapo, mwulize Waziri Mkuu wetu kitu gani aliamua miezi michache iliyopita.

Malinyi, Kilosa na kwingineko rushwa inatolewa na wafugaji. Hilo si jambo la kifocho. Tumeandika sana, pengine tatizo lenu mnapenda kusoma nani kamfumania nani. Land Dermarcation ni muhimu sana. Hakuna ulimwengu wa leo wa waungwana ambao mtu anazurura na mbuzi, punda, ng'ombe na kondoo nchi nzima. Watoto hawasomi, wakulima wanaonewa nk. 'Land Dermarcation' ni muhimu hata ndani ya nyumba yako-huwezi kuweka soksi kwenye jokofu, au nguo za ndani ukazianika sebuleni. Vivyo hivyo, lazima wakulima watengewe maeneo, na wakulima iwe vivyo hivyo. KInachokwamisha yote haya si kukosekana kwa wasomi au dhamira, bali rushwa tu. Ufugaji wa kutangatanga haupo katika ulimwengu uliostaarabika. KInachopatikana kwa wafugaji hao hakilingani na adha wanazopata.

Umeanza kulituhumu kundi flani kwa bila ushahidi,

Mwandishi, kama wewe tulitegemea usiwe na upande wowote tena utowe na solution, unalamika?

Pompo, usinishambulie kwa hoja nyepesi. Haya mambo sikuanza kuyajua leo. Tangu zama zile za Kilosa, suala la rushwa liko wazi. Rushwa na siasa ni kulwa na dotto. Nikupe mfano mzuri tu. Pale Loliondo suala la matumizi bora ya ardhi lilishaainishwa na kamati zaidi ya nne. Kulianishwa wapi wafugaji wapeleke mifugo, wapi wanyamapori walishe na wapi shughuli za kilimo zifanywe. Kilichotokea baada ya hapo, mwulize Waziri Mkuu wetu kitu gani aliamua miezi michache iliyopita.

Malinyi, Kilosa na kwingineko rushwa inatolewa na wafugaji. Hilo si jambo la kifocho. Tumeandika sana, pengine tatizo lenu mnapenda kusoma nani kamfumania nani. Land Dermarcation ni muhimu sana. Hakuna ulimwengu wa leo wa waungwana ambao mtu anazurura na mbuzi, punda, ng'ombe na kondoo nchi nzima. Watoto hawasomi, wakulima wanaonewa nk. 'Land Dermarcation' ni muhimu hata ndani ya nyumba yako-huwezi kuweka soksi kwenye jokofu, au nguo za ndani ukazianika sebuleni. Vivyo hivyo, lazima wakulima watengewe maeneo, na wakulima iwe vivyo hivyo. KInachokwamisha yote haya si kukosekana kwa wasomi au dhamira, bali rushwa tu. Ufugaji wa kutangatanga haupo katika ulimwengu uliostaarabika. KInachopatikana kwa wafugaji hao hakilingani na adha wanazopata.

Kweli Tanzania tumepewa " ugonjwa" wa kulalamika. kila mmoja analalamika hadi washauri na watetezi wa jamii mnalalamika?

Ok.
1.Ni kijiji kipi kimetenga sehemu ya malisho ya mifungo?
2.Je, mifugo ukalishiwe wapi?
3.Je, mifugo haina haki?
4.Wafugaji hawana haki?

YES kwa nini wafugaji wasipunguze mifugo, na wakulima wasipunguze mashamba? Tafakari[/QUOTE]
 
  • Changamoto,ilikutetea haki ya uzawa wetu,mambo hayo tulikuwa tunasikia toka mikoa mingine. Tutafunga buti ili tusonge front.
    10 minutes ago via mobile · Unlike · 1

  • Malinyileo Blogspot Ako Kwaang
    Today 12:30
    #36 Report Post
    Malinyi Ulanga: Mauaji katika mapambano ya jeshi la polisi na wakulima

    Kumaliza haya matatizo lazima kuwe na dhamira ya kweli kwa viongozi wetu na sio ujanjaujanja tu na kupokea vi rushwa visivyo na msingi. Maeneo ya kilimo yaheshimiwe na ya ufugaji pia. Wafugaji waelimishwe kwamba mifugo mingi sio utajiri bali mifugo michache lakini iwe productive. Maisha ya kutembea nyuma ya kundi la ng'ombe unanusa K zao muda wote yamepitwa na wakati ati!
    6 minutes ago · Like

  • Kevin Mwisongo Kaka malinyileo,hawa watu wanatafuta nn? Hawakuwepo miaka yetu hawakuwepo hawa
    2 minutes ago via mobile · Like

  • Malinyileo Blogspot Mwisongo uko sahihi sana....mara zote nimewataka wana CCM wenzangu kuja cleanly na kuzungumza mustakabali wa Malinyi hadharani pasipo kuficha dhamiri...viongozi wengi hawana ujasiri wa kuyasemea na kutenda yale anayoamini Malinyi inapaswa nayo....always wako cool eti wanapima upepo wa siasa....nini bora kati ya sisi na Malinyi? Kwanza Malinyi yetu then sisi tufuate....Ndio maana namtaka Khalid Nyalyoto sasa atokeze hadharani na kuwakemea wavamizi, watendaji wabovu ndani ya serikali ya wilaya....awakemee sasa na si kusubiri uchaguzi tunaanza kutoka jasho wakati wachawi tunawaona sasa na kujifanya hatuwaoni.....Come out....Speak out...when we call a spade So be it ....
    about a minute ago · Like
  • 203197_100004630294004_345493346_q.jpg

    Write a comment...
 
Manyerere, hakuna siasa kwenye hili jambo.
It is a simple luck of administration in the part of government. Serikali inatakiwa kusimamia sheria, wafugaji wasiingie kwenye mashamba. SIMPLE. Hakuna siasa hapo.

Mkuu, siasa inaingia sana. Utakumbuka kuwa PInda amefuta uamuzi wa Kagasheki kule Loliondo baada ya kuambiwa kuna Wamasai wamepanga kurudisha kadi endapo utaratibu wa matumizi bora ya ardhi ungeendelea kutekelezwa. Kwa wanasiasa wetu, kuahirisha matatizo, au kuvuruga taratibu za kisheria ni jambo la maana na muhimu sana ili kulinda kura zao. Wafugaji wana fedha. Wakati wa uchaguzi wanachanga fedha za udiwani, ubunge nk. Ukiwaondoa leo, ujue fedha za kuhonga kwenye kampeni hutazipata!
 
Manyerere...uko sahihi sana lakini nini chanzo.....
Architect wa upuuzi huu ni Stepehen Mashishanga then wakarithi waliokuwa ma DC Ulanga -Kilombero ambao wamepewa u RC ni yule Katavi na wa Mwanza sasa, sijui walikuwa na ajenda ipi ya kutuletea dhahama hii.

Kwa sasa huyu DC wa Ulanga na timu yake ndio wako taabani kwa wafugaji....
 
jana niliona itv jamaa wa kiteto na kongwa wanaapa lazima mtu afe kati ya wakulima na wafugaji
 
Hali bado ni mbaya baada ya Polisi kudeploy nguvu mapambano yameongezeka na huenda madhara yakiwa makubwa sana na Vigo vingi hasa kwa watoto
 
kwa hali hii kwa mkoa wa Morogoro ni mbaya kila sehemu. Sisi tuliokolewa na jirani yetu ambaye ni askari wa JWTZ baada ya kuchungiwa shamba lake alipojaribu kuuliza akapigwa na wafugaji ambao wao walikuwa hawana shamba wala kiwanja lakini wenye jeuri na kiburi kikubwa waliyokuwa wanapewa na viongozi na polisi pia, alileta wazee wa kazi JWTZ gari mbili zikawashughulikia kikamilifu wafugaji hao na kuwahamisha kabisa. Sasa hivi tunakaa kwa amani .Rushwa ya wafugaji itamaliza wakulima.
 
Mara nyingi maamuzi yasiyofuata HAKI huwa yanaleta manung'uniko na vilevile VURUGU.
vita ya Wandamba na Wafugaji ilianza miaka mingi sana(Takribani 20) ila bado serikali hua hufanya maamuzi nusunusu kuhusu mgogoro huo.
Haya yote ni Malimbikizo ya HASIRA za Wandamba kwa kuonewa kwa muda mrefu na polisi wa malinyi wanaopokea rushwa kutoka kwa wafugaji.NASHAURI KUWA WATU WOTE WA MALINYI PAMOJA NA WANDAMBA WOTE KUWA KITU KIMOJA KWENYE SAKATA HILI, HAKUNA KUOGOPA MTU hata kama wamepeleka Helkopta mbili kwa ajili ya kuvunja nguvu za wadai haki yao.
 
Morogoro.Watu watatu, akiwamo askari polisi wamefariki dunia na wengine watatu kujeruhiwa baada ya kuzuka mapambano kati ya polisi na raia katika Kijiji cha Igwati, Tarafa ya Malinyi Wilaya ya Ulanga, Morogoro.

Diwani wa Kata ya Malinyi, Said Kila aliwataja waliofariki dunia kuwa ni Leon Chikwita, Andrew Likomoka na Edson Kidunda.

Alisema mmoja wa majeruhi Idelfonce Malenga (35), hali yake ni mbaya baada ya kupigwa risasi shavuni. Majeruhi wawili majina yao hayakufahamika mara moja.

Diwani Kila alisema mauaji hayo yalitokea baada ya kundi la wakulima kuvamia Kituo cha Polisi Malinyi kushinikiza kuachiwa kwa wenzao watatu waliokuwa wanashikiliwa kwa tuhuma za kumuua mfugaji mmoja wa kijiji hicho hivi karibuni.

“Baada ya kupata taarifa za kukamatwa kwa wenzao walifika kituo cha polisi ambako, hawakuwakuta watuhumiwa hao kwani walikuwa wamehamishiwa kituo kingine,” alisema diwani huyo.

Alisema katika jitihada za kulinda kituo, polisi walitoa tahadhari mbalimbali za kuwataka wananchi hao kutawanyika ikiwamo kupiga mabomu ya machozi, lakini waliendelea kukaidi amri hiyo na badala yake walizidi kujikusanya na kukivamia na kisha kukichoma moto pamoja na gari la askari lililokuwapo. Katika shambulizi hilo, ndipo mauaji hayo yalipotokea.

Chagonja eneo la tukio

Kutokana na tukio hilo, Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema ametuma timu maalumu ikiongozwa na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja kwenda kuongeza nguvu katika operesheni ya kuwasaka na kuwakamata wote waliohusika na tukio hilo.

Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Senso ilisema jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa, IGP Mwema ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Morogoro hususan, Kata ya Malinyi kuwa watulivu na kuendelea kutoa ushirikiano kwa Polisi wakati uchunguzi ukiendelea.

Chanzo cha mgogoro

Mgogoro kati ya wafugaji na wakulima wa Igwati ulianza Desemba 13, mwaka huu wakati kundi la wananchi lilipomkamata mfugaji huyo na kumpeleka katika ofisi za kijiji.

Ilidaiwa kuwa baada ya kumfikisha, mtendaji wa kijiji alimfungia mtuhumiwa huyo ofisini kwake na kuanza kuhoji sababu za wananchi kumkamata jambo ambalo linaelezwa kwamba liliwakera na kuanza kumshambulia hadi kuikimbia ofisi na kumwacha mfugaji huyo ambaye alishambuliwa na kuuawa.

Kitendo cha kukamatwa na kupigwa hadi kuuawa kwa mfugaji huyo kinadaiwa kuwa kilikuwa cha kulipiza kisasi baada ya wafugaji kuvamia nyumbani kwa Mjumbe wa Kamati ya Mazingira, Victoria Marietha na kumjeruhi vibaya kisha kufariki dunia katika Hospitali ya Lugala, Malinyi alikokuwa akipatiwa matibabu
 
Muda huu maelfu ya wananchi wako lugala hospital ili wakabidhiwe marehemu wao wakawazike kwa sharti la kuletwa mbele yao dc na ocd wake ili kamishina chagonja aelezwa yaliyowasibu tangu kuanza kwa sakata hili.....

Gazeti la mwananchi sijui kwa makusudi ama bahati mbaya wanasema wananchi wameua askari mmoja!!! Ukweli hakuna askari aliyeuawa na wananchi.....muda huu mji wa malinyi umetulia wakisubiri miili ya marehemu lugala hospital....kwa latest news piga 0787753600 aliyeko ktk eneo la tukio
 
Suluhu ni kutenganisha maeneo ya ufugaji na wakulima na wafugaji wapewe masharti kutekeleza 'zero grazing'. wawatafutie chakula wanakojua na mifugo isruhusiwe kuzurura ovyo. sioni kwanini serikali inaendelea kukumbatia hili tatizo had maafa ya aina hii yanaendelea kutokea.
 
Hivi huyu Chagonja ana mafanikio gani toka aanze kutumwa maeneo ya matatizo..? Walipouawa raia Songea alienda.. Alipouawa Mwangosi Iringa alikwenda.. Arusha akaenda.. Na sasa huko Malinyi..! Ataenda mikoa yote maana wananchi wengi wameamka na kujua haki zao.. watakapoendelea kuhisi wananyimwa haki zao watageukia kwenye vurugu.. Ufumbuzi wa pekee ni kwa serikali kusimamia haki bila ya upendeleo..
 
walitumiwa kisiasa huko nyuma, sasa mambo yanawageuka...waliwasha moto wenyewe (ccm na serikali yake) sasa wameshindwa kuuzima
 
Back
Top Bottom