Muganyizi Jackson
Member
- Aug 11, 2016
- 13
- 3
Halmashauri imeanza kutoa mbegu bure kwa wanakijiji na kuwalimia bure, lengo ni kuwawezesha wananchi na kuupiga vita umaskini kwa vitendo.
Mkurugenzi wa halmashauri amewataka wanakijiji wajikite kwenye kilimo biashara na kuachana na kilimo cha mazoea.
Pia, ameangiza kuhakikisha ukusanyaji wa mapato kutoka kwenye mashamba ya mitiki yanayomilikiwa na Malkia Elizabeth wa Uingereza yaliyopo upande wa halmashauri yake ambapo yameanza kuvunwa.
Kwa ufupi serikali kupitia halmashauri ya inapoteza mapato mengi kupitia mashamba hayo katika maeneo mabalimbali hapa nchini.
Kipekee nampongeza mkurugenzi na wakurugenzi wengine kuiga mfano huu kuwawezesha mwananchi na kuhakikisha hakuna mapato ya halmashauri yanayopotea kwa kisingizio cha mwekezaji mkubwa na hii ndio serikali ya Mheshimiwa Rais na Tanzania mpya inayokusudiwa.