Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,965
Aliyekuwa mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi mwaka 2015, Maliki Marupu, amemjibu mwanachama mwenzake Humphrey Polepole kufuatia kauli yake kuhusu mchakato wa uchaguzi wa urais ndani ya chama hicho.
Katika majibu yake, Marupu amesisitiza kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hupatikana kwa mujibu wa katiba ya chama, na si kwa kufuata desturi au mazoea kama ilivyodaiwa na Polepole.
Amesema, kunapokuwa na mchakato wa kumpata mgombea wa nafasi ya juu kama ya urais, ni lazima chama kifuate taratibu na kanuni zake kama zilivyoainishwa kikatiba, ili kuhakikisha haki na usawa kwa wanachama wote.
Katika hatua nyingine, Marupu ametoa wito kwa wanachama wa CCM kuacha kumjibu Humphrey Polepole, akieleza kuwa kufanya hivyo ni sawa na kumpa umaarufu usiostahili kwa kauli ambazo hazina mashiko ndani ya misingi ya Chama.