Maliasili hamtutendei haki wauza mkaa

Maliasili hamtutendei haki wauza mkaa

Hiyo faida ya 5000 hadi 10000 baada ya wiki mbili unawezaje kuishi mjini kama sio udongo?
 
Mkuu gas ni 20000 kujaza iyo 50 ni pamoja na mtungi

Huku mkoani niliko mara zote nimekuwa nikinunua mtungi wa gesi wa kilo 16 kwa elfu 54. Na hapo naenda na mtungi wangu uliokwisha na kupewa mwingine uliojaa! Huenda hiyo ya elfu 20 ni ile midogo.
 
Yah nlikua naongelea mtungi mdogo
Huku mkoani niliko mara zote nimekuwa nikinunua mtungi wa gesi wa kilo 16 kwa elfu 54. Na hapo naenda na mtungi wangu uliokwisha na kupewa mwingine uliojaa! Huenda hiyo ya elfu 20 ni ile midogo.
 
Mkuu unashauri nini? Je tutafute njia ili mwananchi maskini aweze ku afford gas,umeme, biogas nk au tuendelee kukata miti yetu
Serikali kuacha kukusanya tozo katika mkaa maana inapunguza kukata miti katika wastani mdogo mno na kuongeza nafasi ya kula mlo mmoja kwa siku kitu ambacho ni hatari..
Kuwe na uwiano sahihi wa upatikanaji nishati (naona wanajaribu upatikanaji umeme kupitia REA),kuimarisha logistiki ya upatikanaji wa gesi hadi miji midogo pamoja elimu sahihi na sio tu kufanya maonesho miji mikubwa kukiwa na lengo la kukusanya fedha mlangoni.
Kuunda chombo maalum cha kushughulikia usambazaji nishati ya gesi katika miji inayokua..kama katika barabara kuna Tanroad na Tarura basi ewura ipewe chombo rafiki kusaidia upatikanaji wa gesi na majiko ya gesi yafike kwa urahisi katika miji inayokua,pia kuwe na tax relief kwa wakala wa gesi/muuza gesi ili aweze kuuza kwa bei fulani kulingana na uchumi wa sehemu husika.
Kila Wilaya yenye miti michache iwe na misitu ya kupanda na mabwawa ya kuchimba kwa ajili ya umwagiliziaji, yafungwe mota maalum katika gridi ya taifa mkurugenzi,afisa msitu,na wananchi wasiamamie.
Hatuwezi kufuta matumizi ya mkaa na kuni moja kwa moja,tutakuwa tunavunja kanuni ya matumizi nishati asili..
Mishahara ya wakubwa mfano Wabunge na Executives iongezwe kwa kutazama jamii inayowalipa ni masikini..uafahari wote huo wanaoutaka unasaidia nini? pia Rushwa idhibitiwe japo tufikie asilimia 75%
 
Msafwa,heshima ni kitu cha bure,pumbavu ni nani,
ni wewe na familia yako.
 
Matumizi ya gas kwa maeneo ya mijini ni cheap juliko huo mkaa. Ninachokiona watumiaji wengi wa mkaa wanakwepa ile initial cost ya vifaa vya gas (mtungi, jiko na viunganisho vyake) ila gas ni cheap zaidi ya mkaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni cheap kama una kipato cha uhakika mkuu,imagine kipato chako ni cha chini halafu inakukatikia wakati ambao huna ukiangalia mkaa wa sh elf 1 unakutosha kula na familia yako
 
Back
Top Bottom