Maliasili hamtutendei haki wauza mkaa

Maliasili hamtutendei haki wauza mkaa

BABA SANIAH

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2013
Posts
4,777
Reaction score
6,268
Iko hivi, wengi mijini hapa tunanunua mkaa wa magunia makubwa then tunauza kwa vipimo angalau kupata riziki.

Sasa mnapotuambia sisi wakala wa wauzaji wa maliasili za misitu tulipie Shilingi 261,000(laki mbili na sitini na moja kama kodi kwa mwaka), uhalali uko wapi?

Mtaji wangu ni magunia 2 sawa na Shilingi 150,000 kwa mwezi na nikiuza faida kwa gunia sana sana napata Shilingi 5,000 au 10,000 na gunia moja nauza mpaka wiki tatu.

Uhalali uko wapi?

> Aliyekata mkaa huko shamba kawalipa maliasili mpaka mkamruhusu kukata.

> Aliyeleta mjini nae kalipa kibali cha kusafirisha mkaa mpaka kaleta mjini

Sasa kwanini mnataka na sisi wamachinga wa mkaa tulipie tena? Yaani gunia moja linalipiwa kodi mara tatu?

Mnataka kipimo tuanzie Shilingi 2,000 baada ya Shilingi 1,000 kwa kifuko kidogo cheusi au kikondom?

Sawa aidha tutafunga au tutalipa then mkaa tutaanzia 2,000 anayetaka anunue hataki aache maana hata hauozi.

Goodbye

Sent using Jamii Forums mobile app
 
iyo kazi unafanya faida 10000 kwa mwezi una mdanganya nan? Kwanza uko wapi nije apo saivi? Na iyo ela utatoa tu!

Tunafanya ivo makusudi ili kupunguza matumizi ya mkaa na watu watumie nishati mbadala!

Kama hutaki acha, kauze gas! Nyooooooo😎😎😎😎
 
Kama hutaki acha, kauze gas! Nyooooooo[emoji41][emoji41][emoji41][emoji41]
Elewa ndugu,gunia moja faida 10000sawa sawa?
Na gunia unauza mpaka wiki 2au tatu sawa sawa?
Sasa he kama kwa mwezi nauza magunia 2 napata 20000 faida, kwa mwaka maana take 20000 *12 sawa na 240000
Hiyo faida
1nile
2nilipe fremu
3nilipe kodi ya nyumba
4nilipe UMEME na maji
5matibabu yanngu na familia
6 maendeleo
Je we we unaweza au unaandika ili watu wakusifie?
Bado maliasili niwalipe 261000 niambie hapo hela natoa wapi?
Usiandike Tu kutaka sifa, watu tunataabika kitaa wewe

Sasa ivi tunataka tupunguze matumizi ya mkaa! Una athari kubwa, kwaiyo ndo maana inafanyika ivo, cha kukushauri tumia njia mbadala
 
Kumbuka hiyo ni hesabu ya gunia moja tu. Kwa mwaka utakuwa umeuza gunia 500 hadi 800.*20000?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa ivi tunataka tupunguze matumizi ya mkaa! Una athari kubwa, kwaiyo ndo maana inafanyika ivo, cha kukushauri tumia njia mbadala

Unashauri watu waache mkaa na hivyo kutumia nishati mbadala; ipi hiyo kwa mfano? maana ukija kwenye mafuta ya taa bei haikamatiki tangu uchakachuaji uanze miaka hiyo na hivyo watu kwa sasa wameachana kabisa na majiko ya "mchina" yanayotumia niahati hiyo; ukija kwenye umeme unit moja ni zaidi ya sh. 300! hivyo watumiaji ni wachache sana, ukija kwenye hiyo gesi; mtungi wa kilo 16 bei yake ni zaid ya tsh elfu 50!

Sasa kwa watu wa mjini kama huko Dar es salaam unategemea watatumia nishati gani? Serikali inatakiwa itengeneze mazingira ya watu kutumia hiyo nishati mbadala maana kwa sasa imekaa kianasa anasa hasa kwa wale wananchi wa kipato cha chini na hivyo kimbilio lao pekee kubakia hiyo nishati ya mkaa.
 
Matumizi ya gas kwa maeneo ya mijini ni cheap juliko huo mkaa. Ninachokiona watumiaji wengi wa mkaa wanakwepa ile initial cost ya vifaa vya gas (mtungi, jiko na viunganisho vyake) ila gas ni cheap zaidi ya mkaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama wanataka wapunguze matumiz ya mkaa wapunguzege bas bei ya gas hiv inakuwaje gas tunayo na bado tunauziwa bei au Mimi chielewi wajameni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wauza mkaa na chain nzima hamutendei haki Mazingira
 
Miti inayotengeneza Mkaa ina thamani kubwa sana kuliko Mkaa wenyewe .
Mkaa upande bei maradufu lakini Gas ishuke bei zaidi. that will value our forests and reduce emissions of Carbon.
 
iyo kazi unafanya faida 10000 kwa mwezi una mdanganya nan? Kwanza uko wapi nije apo saivi? Na iyo ela utatoa tu!

Tunafanya ivo makusudi ili kupunguza matumizi ya mkaa na watu watumie nishati mbadala!

Kama hutaki acha, kauze gas! Nyooooooo😎😎😎😎
Asilimia ngapi wanatumia mkaa na wangapi wanatumia gesi/umeme? Per capita income ni ngapi siku hizi kiasi mkaa tununue japo 2000 kwa kimfuko kidogo?
Gesi na umeme zinarahisisha kazi na usafi, nani hataki unafuu? Mkaa na Kuni biashara kwa mama lishe..Takibir/God bless us
 
Unashauri watu waache mkaa na hivyo kutumia nishati mbadala; ipi hiyo kwa mfano? maana ukija kwenye mafuta ya taa bei haikamatiki tangu uchakachuaji uanze miaka hiyo na hivyo watu kwa sasa wameachana kabisa na majiko ya "mchina" yanayotumia niahati hiyo; ukija kwenye umeme unit moja ni zaidi ya sh. 300! hivyo watumiaji ni wachache sana, ukija kwenye hiyo gesi; mtungi wa kilo 16 bei yake ni zaid ya tsh elfu 50!

Sasa kwa watu wa mjini kama huko Dar es salaam unategemea watatumia nishati gani? Serikali inatakiwa itengeneze mazingira ya watu kutumia hiyo nishati mbadala maana kwa sasa imekaa kianasa anasa hasa kwa wale wananchi wa kipato cha chini na hivyo kimbilio lao pekee kubakia hiyo nishati ya mkaa.
Mkuu gas ni 20000 kujaza iyo 50 ni pamoja na mtungi
 
Asilimia ngapi wanatumia mkaa na wangapi wanatumia gesi/umeme? Per capita income ni ngapi siku hizi kiasi mkaa tununue japo 2000 kwa kimfuko kidogo?
Gesi na umeme zinarahisisha kazi na usafi, nani hataki unafuu? Mkaa na Kuni biashara kwa mama lishe..Takibir/God bless us
Mkuu unashauri nini? Je tutafute njia ili mwananchi maskini aweze ku afford gas,umeme, biogas nk au tuendelee kukata miti yetu
 
Shida ya Tanzania anaetunga sera au utaratibu wa kulipa kodi ni mtu anaevaa tai ofisini hana hata biashara ndogo pembeni...
 
Endeleeni kuwa watulivu, stiglers george itakuwa tayari kabla ya 2020
 
Back
Top Bottom